Kikwete, Je hawa ndiyo majangili?

....Da!kwa kweli inasikitisha sana,kumbe ukisika tu jinsi ndugu zetu walivyo teswa huamini mpaka uone.Hawa madhalimu ipo siku Mwenyezi Mungu atatuhukumia hapax2 Duniani kabla ya akhera.
Jamani hivi kweli Mh Rais Kikwete hizi picha kaziona?na kama kaziona atachukua hatua gani?asisahau kua kuna Muumba!
Days are Numbers.
 
Wamama kama hao hata kama watakua kwenye ujangili kuna kitu sio bure, what is the main cause wao kuingia huko?
Hawana hata sura za ujangiri, nchi inabidi ianze kujitengeneza from down below, tanzania inazidi kurudi nyuma day by day, not a single step forward..
Ni muda wa Tz wasimame wenyewe na kuinyosha serikali, if something is unacceptable tukikiacha kiprevail tutakua wa mwisho, Yes we want peace ila what is peace without freedom? mtu kama huyo kafungwa hivo hiyo imekua guantanamo bay? mtu kuwekewa chupa n watanzania wamekaa wanaangalia makes me wonder jst what the heck r they afraid of kuanzisha hata a cause haki ifanyike, kupiga kelele to the world, dunia isikie ione kinachofanyika nchini,
Em ngoja tuwatafute anonymous waanze kazi kutuchakachulia information zote waziexpose hapa kutoka kwenye email na simu za hawa jamaa, tujue wanafikiria nini
 
kiukweli inatia uchungu, na inaumiza zaidi kuona binadamu unakosa hata theluthi ya huruma kwenye utu na haki za mwenzako kwa sababu uzijuazo mwenyewe!!
2015 ni mbali mno kwa hizi dhulma! natamani nipande kileleni mwa dunia ni 'scream' kwa Allah..'kwanini unayaruhusu!!??'
Hatuna viongozi bali watawala. Na ubinafsi + uoga navyo vinatugharimu. hatuna budi kusahihisha makosa ifikapo muda husika kama tulivyokariri kua hii ni nchi ya demokrasia.
poleni sana wahanga.
 
Asante mwana JF...tumeipata hiyo tumwache Mungu aitwe Mungu....ila kuna watu wamepoteza maisha na wengine kuwe vilema..... Rest in Piece for those who passed away.
 
Tusipoitoa CCM madarakani kwa sanduku la kura kutokana na wizi wao basi itabidi tutafute njia nyingine huu ****** hakubaliki kamwe, niko tayari kuingia hata msituni kutetea wanyonge...

Msitu wa Mabwepande ndo mpango mzima au vipi? Jamani jamani, vita mvisikie hivyo hivyo kwa redio na TV na magazeti... Kura yako na yake na yangu tu ndizo zitakazowatoa CCM...Vita vya wenyewe kwa wenyewe tuwaachie Somalia na huko kwingine...
 
Ila itauma saana kwa akili za baadhi ya raia kwa kuipa kura ccm pamoja na unyama wote huo.Na ndiyo maana akina kapuya wanatamba kudai wao ndiyo wenye nchi watatuumiza kadiri wawezavyo na sheria kwao haipo. Ee MWENYEZI MUNGU TUONE HURUMA kwa kutuchagulia MUSA wa kuiongoza TANZANIA na siyo mafarao hawa ccm wameua wenzetu na kutunyanyasa vya kutosha. Haya mambo unayasikiage tu kwa wenzio yakikufka ndiyo utajua machungu tunayoyazungumzia. Binafsi mpaka naiona dunia chungu kwa ajili ya unyama wa huu utawala wa ccm
 
Siipendi serikali hii ya Maccm, siipendi Ccm, simpendi Kikwete Rais dhaifu kabisa kuwahi kutokea Tanzania,
Rais ambaye anawajua wauza unga lakini hajawahi kuwashughulikia, Rais ambaye alisema walioiba fedha za Epa akiwakamata Nchi itatikisika hivyo aliwaomba warudishe kidogokidogo tu pesa walizoiba wayamalize.

Raisi dhaifu Jk ameunda serikali dhaifu tangia anaingia madarakani mpaka leo hii,
Rais ambaye anaweza kukushawishi uiibie serikali hata kama wizi haukua tabia yako kabla, maana huwezi kuona wenzio wanaiba mbele ya Rais na hawafanywi kitu na wewe ukabaki tu na umaskini.

,Unaiba na Rais anakuomba urudishe ulichoiba kistaarabu kabisa tena baada ya wananchi pamoja na Wahisani kupiga kelele mno, sasa wananchi wanauwawa mbele yake na hana la kufanya zaidi ya kupangua mawaziri tu.
Ee mungu tuhurumie na ututie nguvu kumudu kutawaliwa na hiki kivuli cha Rais mpaka kimalize muda wake.
 
Sasa ulijua nini kuhusu maana ya tokomeza? wapigwe tu kama wao wanavyoua tembo na askari wanyama pori..
 
Back
Top Bottom