Kama UVCCM ingekuwa chama ningependekeza kifutwe

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Taifa kama Taifa najua kwa njia mbalimbali huwa lina mipango ya namna ya kutengeneza warithi ( successors) wa nafasi mbalimbali za uongozi na utawala ktk nchi zao .

Na ninajua pia kwamba, vyama vya siasa kwa kuwa ni candidates wa nafasi za kiuongozi na madaraka ya nchi, huwa pia na mipango ya ku groom vijana wanaotokana na vyama vyao kurithi nafasi mbalimbali .

Najua idara za vijana katika vyama mbalimbali, zinafanya kazi hiyo pia ya kuwainua vijana kuwa mbadala wa wale waliopo na wanaoondoka ktk nafasi za kiuongozi.

Wazo la kuwaandaa vijana ni zuri sana na huo ndo mwendo wa dunia. Viongozi mbadala uandaliwa, Ili kuja kuchukua nafasi baadae. Wasiwasi wangu umekuwa tu kwamba ni Je, uandaaji wa hawa vijana kuwa warithi (successors) unafaa.? Na kama ndiyo vijana wa chama Cha mapinduzi, ambao kimsingi ni warithi( power successors) wanakwama wapi?

Idara ya vijana ya chama Cha mapinduzi ni case study ya kwa Nini ninaandika hili andiko.

Idara hii, naweza sema categorically, inabidi ichunguzwe kujua hasa kwa hakika wanaandaliwa kuwa kweli viongozi wa nchi au watu tu wa hivihivi?

Tuna vijana wa zamani ambao walitokana na idara hii, nasema bila kumung'unya maneno, " ulikuwa hasa unawaona ni viongozi na statemen walau". Watu kama Joseph sinde warioba, Salim Ahmed Salim, John Malecela, Abraham Kinana, Jakaya kikwete, Josefu Butiku, Generali ulimwengu, nk, pamoja na mambo mengine, hata ukiwasikiliza Sasa unaona kweli aina ya watu wanaoielewa nchi hasa, siasa yenyewe, sheria za nchi, na ubinadamu ( kumbuka binadamu wote ni sawa na Africa ni Moja).

Ninasema wanaoelewa nchi kwa sababu, limezuka kundi la vijana wanaotokana na Idara hii ya vijana CCM katika nafasi za madaraka na uongozi, ambao naona kwa hakika hawaielewi nchi, hawajui siasa za masuala ( politics of issues), na ni wakereketwa wa chama tu bila mantiki ( fanatics).

Wao wanadhani nchi ni chama Chao Cha CCM, na malengo yao binafsi.

Ebu tuwe wakweli, bado kweli Kuna vijana ndani ya idara hii wanaojua Nini maana ya imani safi ya chama Chao juu ya umoja, amani, upendo, na mshikamano wa wananchi?

Nashuhudia viongozi wanaotokana na Idara hii, wakiwa wababe, wakeretwa wa chama wasiojali maslahi ya nchi na watu wengine, watafuta pesa za aibu, na ku target madaraka ya juu Ili hali hawako vizuri kabisa .

Mie hujiuliza? Hivi mkuu wa wilaya anayenunua nyumba za wageni Ili wageni wa vyama vingine wanaotaka kufanya mikutano ya siasa kwenye eneo lake wasifanikiwe, huyu anajielewa kweli? Ni mzalendo huyu kweli? Ametokea nchi ya ustaarabu kama hii yetu? Au ni mtu aliyekosa maadili na asiyejielewa aliyevishwa madaraka na uongozi.

Kihongosi ,ambaye amelaumiwa juzi na Chadema hajajibu tuhuma zake, na kwa taarifa wale wasiojua huyu hapa nyuma tu kidogo alikuwa katibu wa uvccm Taifa. Haya ni matendo gani kwa watu tunaotegemea wawe warithi wa nafasi kubwa zaidi za uongozi na madaraka?

Vijana wa CCM huku mtaani ,huoni kuimarika kwao kisiasa, hawajui siasa za masuala, hawajui nchi kiuhalisia, bali ni wababe, wajeuri walioshiba kiburi, Cha madaraka? Na sijui wanakitoa wapi? Wamejigeuza kuwa Jeshi la akiba la nchi. Maneno yao ni kutishia kupoteza wanaowapinga na kuhakikisha watanzania wenzao hawafaidi keki ya uongozi isipokuwa wao au watu wanaotokana na chama chao.


Katika matembezi yangu ambayo huyafanya kwenye harakati za kuhangaikia maisha, nilishuhudia mkuu wa wilaya Arusha, ambaye ni kijana, akiwaondoa wananchi wadogowadogo walima mchicha, eneo moja pale fire Jiji la Arusha, kwa kisingizio Cha kujenga stand mpya ya magari madogo, kwa nguvu bila hata kuwapa taarifa Ili wango'e michicha yao waliyokuwa wamelima pale.

Ajabu alisikika akisema anafanya hivyo kwa sababu yeye ndo mkuu wa wilaya. Kwa uchunguzi wangu kidogo nilioufanya, mkurugenzi wa Jiji ambaye hakika alitakiwa awe wa kwanza kujua ujenzi wa stendi hiyo hakuwa na taarifa sahihi za ujenzi huo. Hawa wananchi masikini hawakuwa na namna nyingine ya kufanya.

Hawakupatiwa hata fidia ya mitaji yao iliyopotea, achilia mbali kwamba hiyo stendi haipo maana hakuna chochote kinachoendelea,ukiacha choo tu alizozikenga hapo.

Najiuliza? Hawa vijana huandaliwa wapi? Haya maandalizi yao yakoje? Mbona hawajua diplomasia, mbona hawajui uzalendo, mbona siyo viongozi shirikishi, mbona ni wabeba tu?

Achana Sasa na matamko ya viongozi wao wa juu. Humsikii yule mwenyekiti wao kutoka Zanzibar akiongea siasa za masuala. Yeye ni " tutalinda nchi, kwa nguvu zetu zote, anayetaka shali na ajaribu aone nk.

Nilishuhudua mh Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM akiwa Zanzibar wakati fulani akihutubia tukio moja la kichama. Alipokuwa anaongea mambo ya msingi kama, Amani, kujenga Taifa moja, haki za watu kulindwa nk, Shamrashamra zilikuwa kidogo. Sauti kubwa zilikuwa zikisika pale alipokuwa anataja kibwagizo Cha Mapinduziii " Hapo ungesikia daimaaaaaaaaaaaa" ikiashiria wako tayari kulinda mapinduzi, hawataki mchezo , anayetaka kujaribu kuchukua madaraka yao kwa kura na aje na vitu vya mwelekeo huo. Vijana ambao hawajengwi kujua mambo muhimu ya nchi, kujishusha, kuwa na upendo kwa wenzao, na kuheshimu demokrasia watakuja kuwa viongozi wazuri wa nchi?

Ongea Sasa likes za watu kama kina Makonda, Sabaya, kina Gambo hapo nyuma akiwa serikalini, kina mnyeti, kina Mwiguru Nchemba wakati hawajawa na nafasi kama aliyonayo,
Ungeshuhudia tu ubabe, majivuno, kudharau wapinzani, kutishia kuwaondoa wenzao duniani kama wataleta wanayoita shida, utadhani wao ndo Mungu!

Najiuliza? Hawa vijana bado wanapata mafunzo ya itikadi? Na kama ndiyo, mbona hawaishi kwa itikadi yao? Hawa vijana wameona Nini kinachowafanya kuwa jeuri?

Ni ushauri wangu CCM iangalie namna vijana wake Wanavyo behave maana nashawishika wengi wao, siyo wazalendo na wapenda nchi bali watafuta madaraka na interest zao nyingine.

Umoja huu kama kingekuwa chama Cha siasa ningeshauri kifutwe.

Na kwa kuwa Hilo haliwezekani kwa kuwa utakuwa unawafuta CCM basi idara hii itazamwe upya na chama Chao. Maana kwa mwenendo huo, hatukuwa na warithi ( successors) wazuri ambao, God forbid, kama CCM itaendelea kutawala hawa ndo watakuwa viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom