Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka

Hivi tena kama kuna kitu kinachoitwa kustaafu kwa lazima kwa nini mtu uombe tena kibali cha kustaafu? Si angekaa kimya hadi hapo ambapo angeombwa kuongeza muda kwa mkataba maalum. Hapo ndipo angeweza kukataa kuongeza muda. Au waandishi wanataka ku-spin kuonyesha kama vile amelazimishwa? Ninachohisi ni kuwa jamaa alimtaarifu Mkuu kuwa muda wake wa kustaafu unakaribia. Si vinginevyo.

Amandla......
 
Sio Tanzania!
Sio chini ya serikali ya Kikwete!
Sio baada ya kuona kilichotokea kwa watangulizi wa hili saga!

Hakuna mwenye nia wala haja ya kuwachukulia hatua yoyote yenye tija wote wale waliohusika na njama za kuiibia nchi hii kupitia Ricmond, achilia mbali wizi mwingine wowote. Serikali iko macho "kiulinzi" bwana!

Kikwete asema, "Najivunia rekodi yangu ya kupambana na ufisadi nchini." Mnategemea nini Waungwana! ndiyo maana nimesema huyu jamaa hastahili kabisa kugombea 2010. Akitaka kugombea kwa maoni yangu ni namna nyingine ya ufisadi kutaka kugombea kuiongoza nchi wakati uongozi umeshakushinda na kuna ushahidi wa kutosha kuhusu kushindwa kwake uongozi.
 
Naomba kujua wakuu amestafu yeye mwenyewe au ndio umiri wake umefika au amembiwa kufanya hivyo??

"Bw. Mwanyika amekubaliwa kustaafu atakapofikisha umri wa kustaafu kwa lazima wa miaka 60 ifikapo tarehe 6 Novemba, 2009."

Hatua ya Bw. Mwanyika kukubaliwa kutaafu kwa lazima inaibua maswali mengi, hasa kwa kuzingatia kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 59, haina kipengele kinachoeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atastaafu baada ya kufikisha umri wa miaka 60.

Kifungu kidogo cha (5) kinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atashika madaraka yake mpaka (a) uteuzi wake utakapofutwa na Rais au (b) mara tu kabla ya Rais mteule kushika madaraka ya Rais.

Kwa maana hiyo ya katiba Bw. Mwanyika angeweza kuacha kushika wadhifa huo ama kwa kuachishwa na Rais au kusubiri mwakani baada ya Uchaguzi Mkuu, kabla ya Rais mteule kushika wadhifa wa rais."

Majibu ya swali lako yamo katika maelezo hayo. Ukisoma between the lines utagundua kuwa kuna kitu hapo, lakini bado huyo ni samaki wa kawaida na katika kundi lake bado Hosea! Mapapa bado kabisa hawajaguswa na huenda wasiguswe kabisa kwani JK wakati anajibu maswali tulimsikia wazi akimtetea EL; na baadae EL akaibuka na kusema urafiki wake na JK ulianza zamani, hawawezi kuachana maana hawakukutana barabarani! Je walikutana wapi?
 
Kila la heri J. Mwanyika!!! Ukweli ninao ufahamu jamaa hakuwa na raha kabisa na huo wadhifa (from reliable sources). Cheo kile kinakulazimisha kufanya uproffessional decissions!!!! Hakupenda!!! Believe it or not. Ni kwa muda mrefu alitaka ajiuzulu!!! Ingeleta mtikisiko!!!
 
Huyu nae anajipanga kuelekea mahakamani;hamkumbuki mgonja jamani;nyie subirini watastaafu wengi mwezi wa kumi na moja naona walichofanya ni kusoma na kuwahi nyakati mapema wajipange na mawakili wa kuwasimamia kesi zao

kazi unayo jk;fadhila zinakuponza;uliambiwa ukawadharau watu;kitumbua kinakutokea puani liveeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Wewe Congo,
Mimi natamani wote wanaohusika na Richmond waondoke kabisa serikalini. Hata kama Kikwete naye ni mhusika aondoke.

Nina hakika nchi inaweza kuenda mbele vizuri bila wababaishaji hawa wezi wakubwa.

Hakuna lolote litakaloharibika hata kama serikali yote iliyo madarakani ikiondoka. Ilimradi tubaki na serikali safi yenye hofu ya Mungu kwa kuwajibika kwao.

Lakini kwa sababu ya ujinga wao na wa baadhi ya watu wanadhani wakiondoka wao basi nchi haitabaki. Ni uongo na udanganyifu wao tu.
Tumechoka na wezi wa mali za nchi yetu hii tuliyopewa wote na mwenye enzi Mungu wetu.

Maneno haya ni mazito nayameniingia . Hofu ya Mungu na heshima kwa Watanzania walio iweka serikali madarakani .
 
Msije mkashangaa mkisikia kwamba Maria Kejo ndiyo Mwanasheria wa Mkuu Serikali ambaye atajaza nafasi itakayoachwa wazi na Bwana Mwanyika.
 
Labda kuna kitu kinaweza kufuat baada ya huyu jamaa kusitaafu, na ukichukulia kustaafu kweneyewe kumekuwa kwa lazima.
Huyu Mkuu ni bahati mbaya tu kajikuta kwenye mkondo mbaya..otherwise he is A MAN OF IMPECABLE CHARACTER - UPRIGHT IN OTHER WORDS.
Ukikaa kwenye tenga la samaki wabovu nawe utanuka hata kama hujaoza bado.
 
Kila la heri J. Mwanyika!!! Ukweli ninao ufahamu jamaa hakuwa na raha kabisa na huo wadhifa (from reliable sources). Cheo kile kinakulazimisha kufanya uproffessional decissions!!!! Hakupenda!!! Believe it or not. Ni kwa muda mrefu alitaka ajiuzulu!!! Ingeleta mtikisiko!!!

Mkuu u can say that again.
Ninavyomfahamu huyu mtu ni safi... kama ni makosa siyo kwa vile yeye ni fisadi...ni basi tu unajikuta uko na watu wenye mambo yao.
 
Mkuu u can say that again.
Ninavyomfahamu huyu mtu ni safi... kama ni makosa siyo kwa vile yeye ni fisadi...ni basi tu unajikuta uko na watu wenye mambo yao.

Kwani ilikuwa lazima afanye kazi hiyo? Hata hivyo ashukuru Mungu tu kwamba JK mwenyewe ndiye mzee wa Richmond. Vinginevyo baada ya lile azimio la Bunge watu wote walitajwa wangekimbia na mitondoo huko keko na segerea. VX zao zingebadilika na kuwa zile Green Coaches!!
 
Hata mimi ningekuwa sifahamu sana hii maneno ningesema hivyohivyo kama ulivyosema wewe mkuu.
Kwa wanaomfahamu huyu bwana,wataniunga mkono kuwa kapanda vyeo hadi AG on merit na hata ingekuwa mie huenda labda ningejikuta kwenye kasheshe kama hilo.Unatumikia serikali yako na katika kufanya kazi yako siyo kila mtu atafanana na wewe.Kuna mambo unaweza yafanya kwa uamuzi wako na kuna maamuzi mengi unayafanya ndani ya system yenye systemic problems.Ikiwa ni kukataa kufanya kazi basi nadhani wengi wangejikata lakini what is the alternative system?Umekulia ndani ya serikali hii hii... utakimbilia wapi na umri umeeshaenda? Mnakumbuka kilio cha huyu bwana kwenye lile sakata ni kulilia uadilifu wake.
Mh Johnson kapumzike kwa amani katika ustaafu wako na heshima yako pamoja na kukaribia kuharibika, wenye kukufahamu watakutetea daima.
 
Inawezekana unayosema ni kweli. Lakini kunaweza kuwa na ukweli kuwa jamaa alibadilika ghafla na kuwa fisadi. Kwani kubadilika kunahitaji karne ngapi? Ulishasikia neno mutation? How long does it take for mutation to take place?
 
Asante Mkuu... nimekusoma
I rest my case.
 
Asante Mkuu... nimekusoma
I rest my case.

Sure,

Kwa mtu aliyejenga reputation yake kwa muda mrefu siyo rahisi kuruhusu heshima yake iharibike bila kishawishi cha nguvu (strong inducement). Kama Mwanyika alikubali kula na mafisi basi naye alibadilika na kuwa fisi siku hiyo. Ni vigumu kusema kuwa alioga baada ya kulowa damu aliyomwagiwa na mafisi akatakata. You can only be with them or against them but never halfway.:rolleyes:
 
Wewe Congo,
Mimi natamani wote wanaohusika na Richmond waondoke kabisa serikalini. Hata kama Kikwete naye ni mhusika aondoke.

Nina hakika nchi inaweza kuenda mbele vizuri bila wababaishaji hawa wezi wakubwa.

Hakuna lolote litakaloharibika hata kama serikali yote iliyo madarakani ikiondoka. Ilimradi tubaki na serikali safi yenye hofu ya Mungu kwa kuwajibika kwao.

Lakini kwa sababu ya ujinga wao na wa baadhi ya watu wanadhani wakiondoka wao basi nchi haitabaki. Ni uongo na udanganyifu wao tu.
Tumechoka na wezi wa mali za nchi yetu hii tuliyopewa wote na mwenye enzi Mungu wetu.
Ulipokuwa halmashauri ya Bukoba ulifanya ufisadi nani kakuchukulia hatua?chama ulichokihama una tuhuma nzito za wizi wa pesa unasemaje?
 
Back
Top Bottom