Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bill, Oct 6, 2009.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete amekubali kustaafu kwa lazima kwa Mwansheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, ifikapo Novemba 6, mwaka huu.
  Bw. Mwanyika anastaafu kwa lazima katika kipindi ambacho Mkutano wa 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakuwa ukiendelea, ukitarajia kuhitimisha sakata la mkataba tata wa Richmond, ambao ulisainiwa wakati akiwa Mshauri Mkuu wa Serikali wa mambo yote ya kisheria.

  Habari za kustaafu kwa lazima Bw. Mwanyika ambaye amekanusha mara kadhaa kuhusika kwake na Richmond, zimethibitishwa Dar es Salaam jana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

  Majibu ya maandishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa gazeti hili, iliyosainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano (OR-MUU) Bi. Zamarad Kawawa, ilieleza; "Bw. Mwanyika amekubaliwa kustaafu atakapofikisha umri wa kustaafu kwa lazima wa miaka 60 ifikapo tarehe 6 Novemba, 2009."

  Hatua ya Bw. Mwanyika kukubaliwa kutaafu kwa lazima inaibua maswali mengi, hasa kwa kuzingatia kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 59, haina kipengele kinachoeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atastaafu baada ya kufikisha umri wa miaka 60.

  Kifungu kidogo cha (5) kinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atashika madaraka yake mpaka (a) uteuzi wake utakapofutwa na Rais au (b) mara tu kabla ya Rais mteule kushika madaraka ya Rais.

  Kwa maana hiyo ya katiba Bw. Mwanyika angeweka kuacha kushika wadhifa huo ama kwa kuachishwa na Rais au kusubiri mwakani baada ya Uchaguzi Mkuu, kabla ya Rais mteule kushika wadhifa wa rais.

  Kutokana na wadhifa wake huo, baada ya mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC kusainiwa, na baadaye bunge kuuda Kamati Teule ya kuchunguza utata uliogubika mkataba huo chini ya Dkt. Harrison Mwakyembe (Kyela), ilibainika kuwa utiaji saini mkataba huo ulisheheni makosa mengi.

  Wakati akiwasilisha taarifa ya kamati iliyochungusa utiaji saini mkataba huo bungeni, Dkt. Mwakyembe alisema;

  "Mkataba umesheheni makosa mengi ya kisheria yanayoashiria udhaifu mkubwa wa kitaalamu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au ukosefu wa umakini katika kuiwakilisha serikali."

  Dkt. Mwakyemba alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili wa Serikali, Bw. Donald Chidowu ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yoyote, hivyo, "Wawajibishwe na mamlaka ya juu ya nchi kwa kuchangia kuiingiza nchi katika mkataba wa aibu," alisema Dkt. Mwakyembe wakati akiwasilisha mapendekezo ya Kamati yake kwa bunge kuhusu hatua alizopaswa kuchukuliwa Mwanyika.

  Baada ya Kamati hiyo kutoa mapendekezo hayo, Serikali kupitia Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ilitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya kamati, akisema kikatiba, Mamlaka ya Nidhamu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  "Kwa hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa watendaji wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali, suala lake la kuhusishwa kwake katika mchakato mzima wa mkataba huo linashughulikiwa na Ofisi ya Rais, IKULU," alisema Bw. Pinda.

  Hata hivyo, katika Mkutano wa 16 wa Bunge uliomalizika mjini Dodoma, Serikali kupitia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Adam Malima, ilitangaza utekelezaji wa awamu ya pili mapendekezo ya Kamati ya Dkt. Mwakyembe, ambapo alisema Bw. Mwanyika hakuwa na kosa analoonekana kutenda kutokana na wadhifa wake huo.

  Bw. Malima alisema iwapo mtumishi yeyote wa umma atatajwa na watuhumiwa walioko mahakamani kuwa alihusika katika makosa ya jinai, Serikali haitasita kumfikisha mahakamani

  Hata hivyo utekelezaji wa mapendekezo hayo pamoja na yaliyohusu maofisa wengine ulikataliwa na Bunge na kuiagiza Serikali kuwasilisha upya utekelezaji mwingine wa maazimio yake katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanzia Oktoba 27, mwaka huu siku tisa kabla ya Bw. Mwanyika kustaafu.

  Source: Majira 06 October 2009
  Mwandishi: Reuben Kagaruki

   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Muda wake umefika labda naye anatayarishiwa mashitaka ya kupelekwa mahakamani.. maana sasa hana ofisi.. itakuwa vizuri labda wakafuata ushauri wa kamati ya Mwakyembe wa kuwajibisha wote kwenye scandal ya Richmond. Naomba kujua wakuu amestafu yeye mwenyewe au ndio umiri wake umefika au amembiwa kufanya hivyo??
   
 3. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mambo haya ndio yanasababisha serikali kuonekana inalichezea Bunge. Kama amekubaliwa kustaafu, manake hajachukuliwa hatua zozote za kinidhanimu kama ilivyoshauriwa na Bunge. Kwa kweli kama Mwanyika amekubaliwa kustaafu bila ya kulazimishwa kisheria (Kuwajibishwa) basi kwa mara nyingine serikali yetu imetuthibitishia kuwa in wenyewe, na wenyewe ni wale waliomtuma Mwanyika kukubaliana na RICHMOND kama ilivyo na wao watamlinda, na kweli wamemlinda mpaka amestaafu.
  Tatizo naona mkataba kati ya Mwanyika na walimtuma ni kumlinda akiwa kazini, nafikiri akitoka hapo itabidi atafute pa kujificha kwani uchaguzi unakaribia na JK anatafuta kura za imani, asije akawa mhanga wa sifa za serikali.
   
 4. O

  Omumura JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu ile dana dana iliyokuwepo ya kumshtaki sasa imejionesha wazi ilikuwa inafanywa makusudi ili jamaa astaafu n apate mafao yake, walah haki ya mafisadi, hafungwi mtu hapo!!
   
 5. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni mwendelezo wa Tanzania zaidi ya uijuavyo! Hakuna hata mmoja aliyewajibishwa tangu varangati la Richmond lianze licha ya kuwepo kwa ushahidi wa wazi. Itakuwa si haki kumwajibisha Mwanyika peke yake ilhali vigogo wenzake wameachiwa kuendelea na pensheni zao. Serikali yetu inajali "watu wake" na imeapa kuwalinda kwa kila hali.

  Watafanya watakalo maana wanajua hamuwezi kuwafanya lolote. Hata uraisi bado wataendelea nao mwakani.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  nchi haina rais makini unategemea nini.those kind of games utazisikia sana na hilo bunge lijalo hakuna cha maana kitakachoaamuliwa juu ya RICHMOND,wataanza kubishana tu kwa nini kuna mgao wa umeme and that is it
   
 7. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Sioni ubaya wowote kustaafu. Kwanza keshatimiza miaka 60 ambao ni umri wa lazima wa mtumishi wa serikali kustaafu. Ingawa inaweza kuonekana ni kulea maovu lakini watumishi wa serikali wafanyapo makosa (ingawa makosa mengine hayatangazwi) na kuwajibika kuadhibiwa, na hasa suala la kufukuzwa kazi, mara nyingi umri wao huangaliwa kabla ya adhabu kutolewa. Hii haiko kisheria lakini ni suala la ubinadamu tu. Hata mahakamani inatokea adhabu kupunguzwa kwa sababu ya umri.
  Wakati mwingine lazima Serikali ionekane imara kuwa haishurutishwi na chombo chochote. Bunge litakapokaa mwezi November itatolewa taarifa kuwa Mwanasheria Mkuu kastaafu kwa lazima. Azimio la bunge litakuwa limetekelezwa.
  Wakianza kufukuzana kwa kila kosa linalotokea habaki mtu serikalini. Kastaafu mwacheni aende. Mengine baadae.
  Halafu kama ni suala la kuwajibishana kuhusu Richmond wa kuondoka ni wengi.
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  aaah siasa za bongo
   
 9. Zwangedaba

  Zwangedaba Member

  #9
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 1, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Labda kuna kitu kinaweza kufuat baada ya huyu jamaa kusitaafu, na ukichukulia kustaafu kweneyewe kumekuwa kwa lazima.
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wewe Congo,
  Mimi natamani wote wanaohusika na Richmond waondoke kabisa serikalini. Hata kama Kikwete naye ni mhusika aondoke.

  Nina hakika nchi inaweza kuenda mbele vizuri bila wababaishaji hawa wezi wakubwa.

  Hakuna lolote litakaloharibika hata kama serikali yote iliyo madarakani ikiondoka. Ilimradi tubaki na serikali safi yenye hofu ya Mungu kwa kuwajibika kwao.

  Lakini kwa sababu ya ujinga wao na wa baadhi ya watu wanadhani wakiondoka wao basi nchi haitabaki. Ni uongo na udanganyifu wao tu.
  Tumechoka na wezi wa mali za nchi yetu hii tuliyopewa wote na mwenye enzi Mungu wetu.
   
 11. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naaaam! Tena watanzania wanajali ubinadamu sana. Lazima unawashangaa sana watu wanojifanya kuwachungua wenzao na kuwaita mafisadi eti? Kufanya makosa kama hayo, wizi na ubadhilifu wa mali ya watanzania ni kosa la kibinadamu tu. Jamani waacheni watanue hadi umri wao wa kustaafu kwa lazima. Dah, ubinadamu!
   
 12. Robweme

  Robweme Senior Member

  #12
  Oct 6, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani tuvute subira kidogo kwani hata akisitaafu sio kwamba hawezi kuchukuliwa hatua za kisheria.
  Anaweza kusitaafu na akachukuliwa hatua za kisheria vilevile.
  Asante.
   
 13. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,666
  Likes Received: 21,892
  Trophy Points: 280
  Tusubiri tuone kama wabunge katika kikao chao cha Novemba kama hili watalipokeaje. Maana hapa wamepigwa changa la macho.
  .
   
 14. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nenda baba nenda iwe kwa kujiuzulu, kwa lazima au kwa umri who care! tunakusubiri mahakamani kama wenzako kina Mgonja na Yona na Mramba etc.
   
 15. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio Tanzania!
  Sio chini ya serikali ya Kikwete!
  Sio baada ya kuona kilichotokea kwa watangulizi wa hili saga!

  Hakuna mwenye nia wala haja ya kuwachukulia hatua yoyote yenye tija wote wale waliohusika na njama za kuiibia nchi hii kupitia Ricmond, achilia mbali wizi mwingine wowote. Serikali iko macho "kiulinzi" bwana!
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ni upuuzi mtupu. KWA nini hawakutii maelekezo ya bunge walipotakiwa kufanya hivyo? Hivi si ndivyo walivyofanya kwa Mgonja pia?
   
 17. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angekuwa ni kweli ana kosa lolote, angeshughulikiwa akiwa bado ofisini. Huu ni uzushi tu, Mwanyika ni mtu safi. Anastaafu baada ya kuifanyia "serikali" yake kazi ya kukumbukwa na anaondoka na pensheni yake. Hata wazusshi wakijifanya kumzonga mahakamani, mambo hayatakuwa tofauti na yaliyowatokea mafisadi wa EPA. Kelele kwa sana but business as ususal!
   
 18. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inaonyeesha wazi jinsi gani Bunge letu lipo tu. Hivi kuna haja gani ya kuwa nalo?
   
 19. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mahakama ndio ita-detrmine ana makosa au hana makosa kama mahakama itamkuta ni mtu safi then --- wananchi kama mimi nasema "ishi salama na watoto wako"
  Hivyo hivyo kwa wazee wa EPA kina Mramba, Yona na Mgonja mahakama ikisema ni watu safi too me is a fair play wakaishi salama na watoto wao! maana ulitaka serikali ifanyeje? justice as per our system iko mahakamani kama wewe una-alternative tuambie! tujue!
   
 20. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikuelewi! Mimi nimesema Mwanyika ni mtu safi maana hajashtakiwa wala hatashtakiwa mpaka aachie ofisi. Nimesema angekuwa na kosa lolote angeshtakiwa kabla hata ya kustaafu. Alternative gani nyingine unataka usikie toka kwangu?
   
Loading...