jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,259
Balozi wa Marekani nchini, Bw. Mark Green amesema kuwa serikali ya nchi yake haijaombwa na Serikali ya Tanzania kumrudisha nchini aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Balali.
Alisema kwa kiasi kikubwa, hatua kama hizo zitategemea maamuzi yatakayochukuliwa na Serikali ya Tanzania kuhusiana na jambo hilo.
Hata hivyo, alisema wao wako tayari kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kushughulikia ombi litakalofanikisha utekelezaji wa azma hiyo kama ipo.
Bw. Green alikuwa akijibu maswali ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ambapo aliwaita kuzungumzia ujio wa Rais George Bush nchini mwezi ujao.
Alipoulizwa mahali alipo hivi sasa Dk. Balali huko Marekani, Balozi huyo alijibu kwamba hajui na kuongeza kwamba sheria za Marekani hazimruhusu kutangaza nyendo na mahali walipo watu wanaoishi Marekani.
Kuhusu uwezekano wa kurudishwa nchini fedha zinazodaiwa kuchotwa BoT endapo sehemu yake imehifadhiwa kwenye mabenki ya Marekani, alisema kwa kuzingatia sheria za nchini mwake, fedha kama hizo zitafuatiliwa na hata kama zilipitia katika mkondo wa benki za Marekani.
Alisema suala la kurudishwa kwa fedha (kama zipo), kama ilivyo katika kumrejesha Balali, kwa kiasi kikubwa pia litategemea maamuzi ya Serikali ya Tanzania.
Aidha, kuhusu habari zilizozagaa kuwa Dk. Balali alipatiwa uraia wa Marekani kwa njia ya Green Card, alisema kuwa mtu yeyote anayeomba viza maana yake siyo raia wa Marekani na kwamba Balali aliomba viza miaka miwili iliyopita kwa wadhifa aliokuwa nao kama Gavana wa BoT.
Alisema, juhudi za Rais Kikwete kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa ni miongoni mwa mambo ambayo Rais Bush atayazungumzia akiwa nchini.
Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za Afrika ambazo zitatembelewa na Rais George Bush wa Marekani mwezi ujao. Nchi zingine ni Rwanda, Benin, Ghana na Liberia.

- SOURCE: Nipashe