Kikwete Akataa Balali Asiletwe!

BALALI SIO KWAMBA TU NI MTUHUMIWA!BALI NI MTUHUMIWA WA KWANZA!SASA KAMA HAOJIWI SI INA MAANA YEYE NDO ANAOGOPWA?ETI KAACHISHWA KAZI ILI KUPISHA UCHUNGUZI!?UCHUNGUZI WA KUMCHUNGUZA NANI ZAIDI YAKE YEYE MTUHUMIWA WA KWANZA AMBAYE NDO KWANZA KAACHISHWA KAZI?NA PIA UTAMCHUNGUZA VIPI MTUHUMIWA BILA KUMHOJI?YEYE NDIYE ANAYEJUA KILA KITU!NA MH RAIS NAYE ANAJUA KILA KITU..LAKINI TUNAMUOMBA ACHUKUE MAAMUZI YA KISHUJAA!KWANI KIZAZI HIKI NA PIA VIZAZI VIJAVYO VITAMKUMBUKA KWA MAAMUZI YAKE MAGUMU ATAKAYO CHUKUA!MAAMUZI YA KIZALENDO..KWAMBA ALIKUWA UPANDE WA WANANCHI KATIKA VITA DHIDI YA UFISADI!NA KWAMBA YEYE AKIWA KAMA KIONGOZI NA JEMEDARI WA NCHI HII,KWA KUSAIDIANA NA WANANCHI WAKE WALIVISHINDA VITA HIVYO DHIDI YA UFISADI!NI JUU YAKE KUAMUA KUMLETA BALALI AMA LA!KAMA VILE ILIVOKUWA JUU YAKE KUMFUKUZA KAZI!PAMOJA NA KWAMBA AMECHUKUA HATUA YA KUUNDA HIYO KAMATI YA UCHUNGUZI..BADO AMEKWEPA KUCHUKUA MAAMUZI AMBAYO SISI WANANCHI TUNADIRIKI KUFIKIRI KWAMBA HAYUKO UPANDE WETU KWENYE VITA HIVI VYA UFISADI!NI WAZI KAMA ANGEKUWA UPANDE WETU SISI WANANCHI ANGEMLETA BALALI,ANGEMWACHISHA KAZI MEGHJI.AMA KUMUOMBA AJIUZULU!ANGEMUOMBA PIA ATOE USHIRIKIANO KWENYE HIYO KAMATI YA UCHUNGUZI!KWA NINI INAONEKANA KWAMBA NI BUSINESS AS USUAL WAKATI KUNA UHUJUMU UMETOKEA KWENYE TAIFA LETU?HII NI ISSUE TOSHA YA KUIWEKA NCHI KWENYE HALI YA TAHADHARI!THIS IS SOMETHING BIG!ETI HAYO MAKAMPUNI YA UFISADI YAHAKIKISHWE YANALIPA KODI!MIMI NAFIKIRI KIKWETE KAMA ANASHINDWA KUDILI NA HII ISSUE KWA KUEGEMEA UPANDE WA WANANCHI..THEN AJIUZULU!WATU WA KUCHUNGUZWA NI WALE WOTE WALIOIDHINISHA MALIPO KIMNYUME NA MAADILI NA UTARATIBU..WALIOKUWA WAKIJUA WAZI KUWA PESA HAZIENDI KULIPA MADENI YA NJE BALI MATUMBO YA MAFISADI!WALIKIUKA MAADILI YAO..HATUA YA KWANZA NU KUJIUZULU AMA KUFUTWA KAZI!HUKU WAKIHOJIWA KUWA NI NANI ALIWAAMBIA WAIDHINISHE HUO UOZO NA UJAMBAZI!HIYO NDIYO COMMON SENSE!SASA WANANCHI WAHOJIWE ILI IWEJE? VIPI KUHUSU BALALI MWENYEWE!Balali alipozitoa huko benki kuu..kuna watu aliwapa..na kuna watu waliandika barua za kuidhinisha kwa sababu ni wazi kuwa pesa zilikuwa zinaibiwa!sasa hao waheshmiwa wako wapi?hao si ndio wana information za kutosha?longo longo za nini?
Waungwana nimeonelea nigusie hili..ni wazi baraza la mawaziri sasa ni jipya!Hii thread ni mojawapo ya threads zilizokuwa zikimshinikiza mh rais achukue hatua!Kwa mara nyingine tena napenda tukumbushane kuwa vita dhidi ya ufisadi bado inaendela na tunamsisitizia mh rais amlete Balali ili naye ahojiwe na kamati yake hiyo.
 
Kwa wale wote waliokuwa wakiipinga thread hii na kuwalazimisha mamods waipeleke kwenye udaku ndio hao hao wanaodhani kuwa mh rais hataki kumleta Balali!Ama nimekosea?Watu walikuwa wanaendekeza ushabiki wa kisiasa!Mh rais tafadhali tujulishe kama umegoma kumleta Balali..la sivyo tutamfungulia mashtaka wenyewe!
 
Tutamlaumu sana Kikwete, ila tutambue kuwa Rais wetu amezidiwa na hawa jamaa, ila Mungu anampenda sana ndiyo maana amemuomba mola ili wapukutike wenyewe,waache wafu wazikane wenyewe
 
Mods Naomba Muirudishe Hii Kwenye Jukwaa La Kisiasa Tafadhali!
Thanks!
 
Wale wote waliokuwa wakimtetea Kikwete...Lunyungu,Mtanzania,Fdr na wengine wengi waliokuwa wakisema ni spin!VIPI SASA?JK ALIMTAKA BALLALI?
 
Kikwete, kwa nini Ballali?

ban_tahariri.jpg



KAMA kuna jambo lililotushangaza kwa Rais Jakaya Kikwete tangu alipoingia madarakani, ni kumpa kisogo aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Ballali, tangu alipoanza kuugua, alipolazwa hospitalini hadi alipofariki dunia Ijumaa wiki iliyopita.
Si kawaida ya rais wetu kufanya kitendo kama hiki. Tunavyomjua sisi wa Tanzania Daima Jumapili, ni mtu anayewajali Watanzania wake, hasa wanapokuwa katika matatizo, bila kujali kama walimkosea yeye au serikali yake.
Maswali wanayojiuliza Watanzania wengi kwa sasa baada ya kupatikana kwa taarifa za kifo cha Dk. Ballali, ndiyo tunayojiuliza hata sisi, ingawa hatupati majibu. Tunajua wapo wanaoweza kuyajibu lakini kwa makusudi wameamua kukaa kimya.
Ukimya wao huo, ndio uliotufanya tufikirie mbali zaidi hadi kumfikia Rais Kikwete, ambaye ingawa ameonyesha kutenda tofauti na kawaida yake katika hili la Dk. Ballali, lakini tunaamini anaweza kuwaambia Watanzania sababu iliyomfanya yeye na serikali yake kujiweka mbali katika kipindi chote kigumu cha kuugua hadi kufariki dunia kwa Dk. Ballali.
Tunaamini kuwa kifo cha Dk. Ballali, iwe kilitokea kwa mipango ya watu fulani au kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kinamuweka Rais Kikwete katika wakati mgumu, kwa sababu kadhaa, kubwa ikiwa kushindwa kwa serikali na timu aliyoiunda kuchunguza wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Aidha, picha waliyonayo sasa Watanzania dhidi ya Rais Kikwete, inazusha maswali mengi, likiwamo la kama huruma yake ni kwa Watanzania wote au wapo baadhi ambao hawaonei huruma hata wanapokuwa katika hatari ya kufa.
Picha hii inajitokeza kutokana na mlolongo wa matukio yasiyo kuwa ya kawaida aliyoyafanya dhidi ya Dk. Ballali.
Tangu aingie madarakani, Rais Kikwete amejiwekea rekodi ya kutokataa barua za kujiuzulu za wasaidizi wake.
Mifano ya hali hii ni kukubali kwake kujiuzulu kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, marehemu Ditopile Mzuzuri, aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, ambaye aliachia ngazi pamoja na mawaziri wawili, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, na hivi karibuni, Andrew Chenge.
Hawa wote waliandika barua za kujiuzulu baada ya kuandamwa na kashfa, kila mmoja kwa namna yake. Lakini kwa Dk. Ballali haikuwa hivyo, alikataa barua yake ya kujiuzulu baada ya kutolewa kwa taarifa ya uchunguzi wa kashfa ya EPA na siku chache baadaye alimtimua kazi.
Jambo jingine linaloleta utata ni kutopatikana kwa taarifa za kama Rais Kikwete alikwenda kumjulia hali Dk. Ballali wakati akiwa kitandani huko Marekani, akiugulia ugonjwa uliomuua. Rekodi zilizopo zinaonyesha kuwa Rais Kikwete ni mwepesi kwenda kuwajulia hali watu wanaomgusa wanapokuwa wagonjwa au kuhudhuria mazishi yao.
Alifanya hivyo kwa marehemu Amina Chifupa, alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Lugalo na alikwenda Muhimbili kuwajulia hali waandishi wa habari wa MwanaHalisi, Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage, walipojeruhiwa wakiwa kazini, bila kujali kama watu hao ni wakosoaji wakubwa wa serikali yake.
Kwa Dk. Ballali haya yote hakuyafanya. Kwa roho ya ubinadamu ya kawaida sisi tunadhani ipo sababu ya kutokea kwa yote haya ambayo sasa yamezua picha tofauti kabisa miongoni mwa jamii ya Watanzania. Tunaamini kuwa Rais Kikwete anatambua Dk. Ballali alikuwa ni mmoja wa washirika wake wa karibu kikazi hadi alipougua na kwenda Marekani kutibiwa, hivyo kwa roho ya kibinadamu, anaweza kuwaeleza Watanzania walau kwa ufupi sababu ya ukimya wake kwa Ballali. Tunaamini rais anaweza kufanya hivyo kwa kumbukumbu tuliyonayo kutoka kwa swahiba wake, Lowassa, ambaye baada ya kulazimika kujiuzulu, rais alitumia mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam kueleza jinsi alivyoumizwa na kujiuzulu huko kwa Lowassa, bila kuwajali watu wangemfikiliaje! Tunaomba afanye hivyo na kwa Dk. Ballali.
 
Mods kwanini hii isiunganishwe na ile ya Kikwete alikataa?
 
Tumeshawasoma Mafioso Na Kwa Uwezo Wa Mungu Muda Wao Umewadia!its Time To Go!
 
Mushi unaweza kusema kwa uhakika kabisa "Kikwete Akataa Balali asiletwe"? Tumia maneno yako vizuri basi arawa! Otherwise unaonekana kama kituko hivi.
Ndiyo mkuu,naweza kusema kwa uhakika kabisa alikataa asiletwe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naunga mkono kauli yako Mkuu.
Nashukuru kamanda.You can see how difficult is for people to see stuff.It even takes years for people to c.
Unaweza kuona watu waliamini vitendo vilivyofanyika ni justifiable.I dont know what kind of thinking this is.
 
Back
Top Bottom