Rais wa JMT amejisafisha kuwa si mliki wala hawalindi marafiki zake katika sakata la DOWANS. Ameeleza kila kitu kuhusu mchakato wa Richmond hadi Dowans. Aisee naona sasa jamaa ameshutuka amefafanua mpaka basi, ameweka bayana Richmond ni kampuni ya mfukoni na kugusia maamuzi ya CC ya CCM.
Walioona taarifa hiyo jamani tuijadili kidogo.
Source TBC1 Time 02:19
Raisi wetu Bwana mbana ni mwepesi wa kusahau? Maamuzi ya cc ambayo yeye mwenyewe alikaa yalikuwa ni kwamba Dowans walipwe maana Tanesco wenywewe ndio walio katisha mkataba.
Uamuzi wa Wabunge wa CCM ndio uliotoa uamuzi tofauti baada ya watu nje ya ccm kupiga kelele kwa saana, na Sitta na Mwakyembe kusimamia msimamo wao.
Ok yeye anasema hana cha kusema maaana Pinda na Chiligati wamemsemea, Mbona hazungumzi Alivyo sema ngeleja? kwani yeye hajamsemea Raisi??? na Je Werema alivyo sema haja msemea Raisi? mbona hizi kauli anazikimbia?
Ok hawajui wala hawa fahamu, je uamuzi wa kuwaleta si ulikuwa wa baraza la mawaziri ambao yeye mwenyewe alikuwepo? mbona kikao hiki hakikubali?
Watu walilalamika kuhusu uteuzi huo je hakusikia na kubatili? leo suruali imekuwa ndogo yeye anaikata anasema wala hakuiona.
Ok imekuja Dowans vikao kasimamia yeye , mawaziri kawateu yeye, bado anasema hawajui watu hawa? kuna IPTL atasema hawajui watu hawa? na mtu akikuchagulia tusi atakutupia tu? Oh mimi si semi uongo lakini yeye anasema ukweli.
Kuna issue ya uteuzi wa Mkurugenzi wa ATC, atasema hamjui mtu huyu? akafanya madudu ATC , magazeti yakaandika, yeye atasema hausiki na maamuzi hayo, na wala hamjui aliye fanya hivyo, wakati huo huo ana waziri wa wizara husika na vikao vya baraza la mawaziri na TISS, lakini bado atatuambia kwamba hajui wala hamjui mwizi wetu. Huyu ndio Kanali JK Mrisho