kuhusu dowans mkwere kasema haya......
Dowans
Ndugu Wana-CCM na Ndugu Wananchi;
Jambo ninalotaka kulizungumzia sasa sikutaka kulizungumza kwa sababu Waziri Mkuu alishalifafanua baada ya semina ya Wabunge wa CCM na hata Mheshimiwa John Chiligati, Katibu wa Siasa na Uenezi Taifa alishalizungumzia. Sikuona umuhimu wa kufanya hivyo kwa sababu viongozi wenzangu hao wameelezea kwa ufasaha uamuzi wa Kamati Kuu na ule wa kikao cha pamoja cha Wabunge wa CCM.
Lakini, yapo maneno mengi ati mbona Rais yupo kimya sana, hatujamsikia kusema chochote? Niseme nini zaidi na hao wote wameshasema kwa niaba yangu. Wapo wanaosema nipo kimya kwa sababu nahusika na Downs na ati ndiyo mwenyewe hasa. Wapo wanaosema niko kimya au nashindwa kuchukua hatua, kwa sababu marafiki zangu wamehusika. Nawalinda. Kwa sababu hiyo, nikaona nami nisema angalau watu wanisikie lakini sina la ziada ni yale yale yaliyokwishasemwa.
Kwanza niseme wazi kwamba ule msemo wa wahenga wa akutukanae hakuchagulii tusi hapa umetimia. Napenda kuwahakikishia wana-CCM na wananchi wenzangu kuwa sina uhusiano wowote wa kimaslahi kwa namna yoyote ile na kampuni ya Dowans. Sina hisa zozote wala manufaa yoyote yale. Pia sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua kwa sababu ya rafiki yangu au hata kama angekuwa ndugu yangu kahusika. Maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu na Kamati ya Chama ya Wabunge wa CCM yalifanywa chini ya uogozi wangu. Ni uthibitisho tosha wa ukweli huo. Waliokuwepo kwenye vikao hivyo wanajua ukweli wa haya ninayosema. Ningekuwa na maslahi au hofu tusingefanya uamuzi ule.
kwa mtazamo wangu huyu jamaa kaongea siasa mtupu hAPA HAKUNA KITU CHA MAANA AMBACHO UNAWEZA KUMNUKUUU KAMA MSIMAMO WA RAISI WA NCHI
MY TAKE:
1. Rais kaonyesha udhaifu mkubwa sana kiutendaji.. ni kama hajali kabisa mambo mazito yanayoendelea ndani ya nchi ambayo hayakuwai kuonekana nchini hivyo bunge chini ya wabunge wa upinzani wa kweli ipige kura ya kutokuwa na IMANI na rais.
2. Waziri mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa serikali nae pia ameonesha uwezo mdogo sana katika kukabiliana na changamoto dhidi ya serikali yake ikiwemo baraza la mawaziri...ikiwemo kukosa sauti kwenye masuala mazito na kushindwa kushughulikia kero za wananchi hivyo nae pia a resign kitu kitachopelekea kuvunjwa kwa baraza, ndio baraza livunjwe kwani nchi inakwenda kama hukuna serikali vile
MAONI YAKO TAFADHARI