Kikwete ajisafisha Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ajisafisha Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Rula, Feb 5, 2011.

 1. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amejisafisha kuwa si mmliki wala hawalindi marafiki zake katika sakata la DOWANS. Ameeleza kila kitu kuhusu mchakato wa Richmond hadi Dowans. Aisee naona sasa jamaa ameshutuka amefafanua mpaka basi, ameweka bayana Richmond ni kampuni ya mfukoni na kugusia maamuzi ya CC ya CCM.
  Walioona taarifa hiyo jamani tuijadili kidogo.

  Source TBC1 Time 02:19
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  "Ukweli siwajui wenye Dowans na wala kampuni hiyo siijui...wapo wanaosema sijasema kuhusu Dowans kwa sababu wanaohusika ni rafiki zangu....sijasema kwa sababu Chiligati na Pinda wamesema, waliyosema yamtokana na kikao changu cha kamati kuu...."


  Hii ni kauli ya Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa CCM. JK ameeleza kuwa Wakati waziri wa Nishati na Madini Salum Msabaha alipomfuata kudai kuwa wizara ya fedha imegoma kuwalipa Dowans, lakini yeye alimtahadharisha kuwa hii inaweza kuwa kampuni feki..... anaendelea kueleza


  --
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nasikitika sijaiona hiyo habari nipo barabarani kutafuta pesa ili niweze ku-maintain heshima yangu mbele ya familia yangu maana kamshahara kangu kamechakachuliwa na mfumuko wa bei hivyo njia mbadala hazikwepeki
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  rais kuongea maneno ya namna hii ni mpumbafu na ujinga wa hali ya juu...asifanye watu watoto hapa na majibu yake ya hovyohovyo...kwanza nani kamuuliza mpaka anaanza kufafanua ...stupid
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naona amemaliza kwa kusisitiza kuwa serikali haitaipa TANESCO walipe DOWANS ili waone jinsi wanasheria wanavyoweza kusaidia kupunguza mzigo huu mwananchi. Alizungumzia utata wa kampuni ya Richmond na ushindi wa kampuni ya Dowans dhidi ya Tanesco na kuonyesha sasa miujiza ya kutoilipa Dowans ipo kwenye jopo la wanasheria.
   
 6. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Pole lakini wana JF walio makini watakujuza kupitia thread hii maoni yao.
   
 7. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupeni habari mkuu
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Za mwizi arobain, yangu macho
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Sawa si kaongea yeye kama Kikwete, ningependa sasa kusikia msimamo wake kama Rais! kama raisi nae anaongea kama mpita njia sasa sisi wananchi wake tumueleweje? sijaona alichoongea zaidi ya kupoteza muda, sisi hatuhitaji ufafanuzi, tunahitaji decision, the way forward sio kutafuta public sympathy! aseme kama rais na sio mpayukaji!!!
   
 10. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama amekiri wazi kuwa Richmond/Dowans kampuni hewa, sasa basi Rostam Aziz, mbunge wake aliyehusika kuisimamia Kampuni hii feki kuchukua tenda, anamfanyaje???????????? Atueleze bayana hapo.
   
 11. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sakata hili ni kubwa hivyo rais kusema kauli yake ilikuwa ni muhimu maana kuna madai kuwa yeye naye ana hisa katika hili na hata kama si kweli basi anawalinda marafiki zake ambao inaaminika walimwaga mabillion ya fedha ambazo ndizo zilizomuweka madarakani mkuu. Ukimya wake ulikuwa ni kama mtu asiyeelweka.
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Jamani hajaongea lolote la maana na nina uhakika ndo kazidisha moto, alichofanya ni kupiga story na alikua wapi sikuzote hizo hadi aje kuongea leo? kwa nini asubiri hadi wengine wawe wakali na kukataa malipo hayo ndio leo ajitutumue azungumzie Dowans, tena kwenye sherehe za CCM ili mambo yakiwa magumu aseme kuwa alizungumza kama Mwenyekiti wa CCM na sio RAIS, na mtaamini maneno yangu
   
 13. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama Rais anatakiwa kututangazia uamuzoi wa nchi. Mfano, hatuliupi Dowans, tutaifishe mitambo yao, tuwafungulie mashtaka wahusika wote wa dowans n.k. Umeme bye, dowans hao...
   
 14. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimefarijika kusikia JK akikiri hili huko Dodoma leo. Lakini bado sijaelewa vizuri ..

  Kumbe JK anakubali matokeo ya tume ya Mwakyembe kuwa ilipatia kuwa Richmond in kampuni hewa.Kama hii ni kweli anatuambiaje kuhusu matokeo ya TAKUKURU waliosema kuwa Richmond haikuwa na shida? Je, kukubali matokeo ya tume ya Bunge siyo kukataa yale ya TAKUKURU? Iweje JK halizungumzii hili la kazi nzuri au mbaya ya TAKUKURU kuhusu Uchunguzi wao kuhusu Richmond?

  nauliza ili tutafakari kuhusu gharama zilizotumika na Takukuru kuchunguza Richmond na kuishia kuwadanaganya Watanzania.

  Hivi bunge lisingekomaa mpaka ikaundwa Tume ya Mwakyembe ikaundwa tungekwendaje kuhusu hili?

  Je ni mangapi yanafunikwa hivi?

  Hivi ukidanganya umma bosi wako anakupongeza na kuomba wananchi wakupe ushirikiano kama alivyofanya JK hotuba yake bungeni?

  Hivi wananchi wanakosea wakisema hawawamini TAKUKURU?

  Angalizo: "Ukiona wakuu wanakazania kupinga jambo kama walivyofanya kupinga kamati ya Mwakyembe jua kuna jambo linafukiwa"
   
 15. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Kwa hio kama hahusiki anataka tufanyeje?
   
 16. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Amekiri kuwa Richmond ni kampuni hewa na ndiyo maana alimtahadharisha Msabaha kuhusu kuwalipa Richmond down payment, ameonekana kuutambua mkataba wa Dowans kwa kusema tumetumia umeme wa Dowans miezi tisa na kuutambua ushindi wa Dowans dhidi ya Tanesco ila baada ya malalamiko mengi ameemua serikali isiipe fedha Tanesco ili kuona jinsi ya kuweza kuepa au kupunguza malipo hayo!
   
 17. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Kikwete anahusika!!! Kusimama jukwaani na kusema huhusiki haimaniishi kuwa ni kweli hahusiki, HAYO ni maneno tu
   
 18. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  nadhani leo ndio amevuruga kabisa wananchi...all those days anakuja kutuambia utumbo huuu....No way....Kawulethi umshine wange!!!!(bring my machine gun)...sijamuelwa na sitakaa nimuelewe...Nilishasema huko nyuma kuwa nchi haina Rasi serious sasa ndo mumeona...huwezi mambo ya msingi kama haya unaongea as if wewe ni waziri kivuli tena wa kambi ya upinzani isiyo rasmi bungeni....JK SIJAKUELEWA BANA
   
 19. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mumuone kuwa ni msafi na hausiki na uchafu wa Dowans.
   
 20. l

  limited JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  raisi ameongea vizuri lakini mimi bado najiuliza power of attorney ya roastam aziz? angeifafanua
  na pili intelejinsia ya machafuko arusha angefafanua who was behind it bcs amesema alipewa ripot before it happen!!!!!!!
   
Loading...