Kikwete ajisafisha Dowans

Kikwete ajisafisha Dowans

Katika maadhimisho ya miaka 34 ya ccm jk alitoa hotuba inayogusa mambo mbalimbali,
1.Dowans,anasema eti hata yeye anashangazwa na hilo swala la dowans,kwa amiri jeshi mkuu,mwenye mamlaka kamili anatoa kauli ya ajabu,badala ya kueleza mikakati ya kuzuia uhaini na ubakaji uchumi,ni dhahiri amekosa uhalali wa kuwa rais
2.Mauaji ya arusha,et yalisababishwa na chama flani kwa malengo ya kisiasa,ikiwa hana uelewa wa kujua chanzo cha vurugu arusha,kuwa ni uchakachuaji wa meya,na ni vita kati ya haki na udhalimu,jambo ambalo kila mtu analijua,Jk kushindwa kuujua ukweli huu umekosa uhalali wa kuwa rais
Jk simamia haki na ukweli
saa ya ukombozi ni sasa

Kama ni kweli kaongea hivyo basi nchi hii haina kiongozi. Tuvumilie tu tupate kiongozi muafaka ifikapo 2015.
 
Yeye Jk ndio anamteua mkuu wa usalama wa taifa,ambayo moja ya kazi za idara hii ni kulinda nchi na maslahi ya nchi,dowans ambao ni wabakaji uchumi,na matapeli wanitapeli serikali mchana kweeupee na bado rais anataka tuwe na imani nae?haiwezekani ameshindwa kazi tuliyomtuma kwa mujibu wa katiba,he must go,,,,,
saa ya ukombozi ni sasa,,,,,,,
 
What did you expect him to say?? You know, siku hizi hakuna element of surprise inapofikia hotuba za JK na mawazo alionayo yeye. He is in his own planet.
 
Kikwete hana uwezo wa kuliongoza hili Taifa. Hatuna maji wala umeme aibu kubwa sana kwa viongozi wa hili Taifa
 
Kama ni kweli kaongea hivyo basi nchi hii haina kiongozi. Tuvumilie tu tupate kiongozi muafaka ifikapo 2015.

hatupaswi kuvumilia!Kwa kauli alizozitoa jana ametuthibitishia wazi kuwa hana uwezo wa kuongoza taifa hili,kumuacha aendelee na wadhifa huu nikuliangamiza zaidi taifa letu!
 
Nafedheheka kuwa mtanzania, kuwa sehemu ya kizazi hiki ambacho kinajisifia kwa kuwa inactive ktk fikra na vitendo; ambacho suluhisho lamatatizo yako ni kukubali yaishe, na kinamwachia mwenye nguvu aamue lini atatoa haki... Na aspoitoa basi, tukae tu...tutafanyaje. Huu ni unini jamani?! Hauna hata adjective yake, aaaaaagghhhhh!
 
KUKIRI KUWA CCM KUNA KITU INAMISS (mvuto) NDIO MAANA IKO ILIVYO "kuna kitu tunakosa ndio maana tuko hivi"
CCm jnamjss rais wa kuwashughulikia Kagoda, Deepgreen, Meremteta na ufisadi wote mwingine.
wakimpata huyo tu, basi chama kitarudi kwenye status yake ya zamani.
 
hoja nzito majibu rahisi. tumuombee atabadilika kwasababu keshakua RAHISI WETU.
 
Mwanampambanaji, ulichosema ni kweli na ndicho ambacho naamini wengi wanakifikiria.

Mheshimiwa Jakaya Kikwete ni kiongozi ambaye huwezi kuelewa anasimamia nini. Kuna wakati unaweza kuamini kwamba yeye anaonewa, hausiki! Kuna wakati unaweza kuamini kwa dhati anahusika! Hapa sizungumzii Dowans peke yake! Nazungumzia masuala yote muhimu yanayotugusa!

Inakuwa vigumu sana kuelewa msimamo wake hasa pale anaposema 'wenzangu wameshalisemea' bila kujali hao waliosema wamesemaje au wamesema nini!!

Hapo ndipo mtu anahoji uhalali wake kuwa Raisi au kuendelea kuwa Raisi!
 
This is very strange!

A president, head of State, Chief in Command wenye kila resource mkononi mwake hajui nani anataka kuibia wananchi wake.
Kwenye kikao anachojisifu kukisimamia mwanachama wake (mwakyembe) kamtaja mmiliki kwa nini asimwite chemba kupata taarifa zaidi?

Kama ni kuua soo bora angesema "Nimesikia kuna watanzania wenzetu wanamasilahi kwenye Dowans, tunafuatilia ili kubaini ukweli ila wanapaswa kujua hii ninchi yetu sote, madhara ya kuihujumu wao hawawezi kusalimika"

Mie hata sijui kina nani wanamshauri cha kuongea

Unamshangaa JK? Huyu ni mtupu mukichwa. Washauri wake ni machekibobu wa hapa tauni, na wanaokwenda mlingotini.

Huyu tunaye mpaka 2015.
 
Sijawahi kusikia RAIS anasema "sasa tunatafuta manouver ya kisheria ili tujue la kufanya"!!! Tanzania haikuwahi kuongozwa namna hii, kama duka la viatu. Mungu wetu, Mungu wetu, MBONA UMETUACHA??
 
Ndo maana hata miye nasema hawa viongozi wetu mabwege issue simple wanazunguka mbuyu .ila hiyo hela ikilipwa mi nalia na WALOVUNJA MKATABA..Halafu mazee siko kwenye system nko bush .struggling like other village WALIPE WASILIPE HAINIPI HEADACHE huwa nachoka tu kila sku dowans dowans i get fedup
Hivi mtu akiiba gari akakuzia, wewe ukashikwa na hiyo Gari, utaachiwa kuwa nalo au utanyanganywa? na hela hurudishiwi na serikali/na mwenye gari aliyeibiwa.
Kuto kujali kwako kulipwa au kuto kulipwa kwa Dowans kuonyesha jinsi gani una akili nyingi saana una shindwa kuelewa ikiwa hiyo hela ikilipwa Dowans, badala ya kuwekezwa kwenye vitu vingine wewe una pungukiwa na huduma ambayo ulitakiwa kuipata mfano barabara ya kwenda kijijini kwenu haitotengenezwa au kufanyiwa ukarabati, au shule kujengwa au kuwekewa umeme hata wa jua, mwalimu kulipwa mshahara wake au kuboreshewa malipo yake wewe kukatwa kodi zaidi ili kufidia pengo la mapato na matumizi ya sirikali inapidi umeone jirani yako akupige msasa kidogo.
 
Hivyo tu ndiyo kujisafisha, hivi tulitegemea asema anahusika???

Je ni kweli hawajui wamiliki wa DOWANS?!
 
>2najua dowans haitalipwa, kibiriti cha wenye nchi kimejaa.

>watawala wote duniani wanafanana, angalia misri jinsi mbaraka anavo2pa karata zake.

>mizengwe ni sehemu ya uongozi.

>hesabu za serikali ziwekwe hadharani, quaterly
 
Nafedheheka kuwa mtanzania, kuwa sehemu ya kizazi hiki ambacho kinajisifia kwa kuwa inactive ktk fikra na vitendo; ambacho suluhisho lamatatizo yako ni kukubali yaishe, na kinamwachia mwenye nguvu aamue lini atatoa haki... Na aspoitoa basi, tukae tu...tutafanyaje. Huu ni unini jamani?! Hauna hata adjective yake, aaaaaagghhhhh!

Naamini bado tuna nafasi mkuu ya kukabiliana hali hii.hatupaswi kunyong'nyea na kukubali matokeo.Sisi vijana tunapaswa kusimama pamoja kuufuta udhalimu wa jk na serikali yake.Tukikaa kimya nakusema "waache tu Mungu anawaona",watoto wetu watatuadhibu!
 
sijui katika kuwafanyia shorlist wagombea uraisi nk tuanze na kuwafanyia mtihani, wa general knowledge au kuelewa uwelidi wao wa mambo ya msingi ? kwa kuwapa scenerio tofauti tofauti ili tuweze kujua huyu atatufaa au hato tufaa. badala ya kufikiria sera za chama au chama kinaweza kusaidia wakati tuli mpa madaraka , mambo yake hayako ..........kichama chama. na tatizo lingine nililo liona ni kumwachia mwenyekiti aweke watu wake kwenye cc, na hata katibu mkuu anaye oana yeye atamfaa badala ya katibu mkuu atakaye wafaa wanachama wake.
 
Tangu lini mwizi akakubali kuibwa kirahisi hata kama amekamatwa na mali ya wizi? Lazima atajitetea tu.
 
Rais wa nchi anapongea kama vile ana mamlaka ni kitu cha kushangaza na kusikitisha sana kwa kweli. Huyu ni mtu mwenye mamlaka na uwezo wa kupata taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya dola kama vile usalama wa taifa, polisi na takukuru. Anajua kinachoendelea. Ina maana hajui kuwa rostam anahusuka kwenye hii dili na yeye ni mtu wa karibu sana na rostam.
 
Back
Top Bottom