Kikwete ajisafisha Dowans

Kikwete ajisafisha Dowans

Ndo maana hata miye nasema hawa viongozi wetu mabwege issue simple wanazunguka mbuyu .ila hiyo hela ikilipwa mi nalia na WALOVUNJA MKATABA..Halafu mazee siko kwenye system nko bush .struggling like other village WALIPE WASILIPE HAINIPI HEADACHE huwa nachoka tu kila sku dowans dowans i get fedup

Mazee bush internet inapatikana vipi?? Acha kutusi wananchi sana sana unajitafutia laana tu....
 
"sasa mafuta yamepanda bei mimi nifanyeje sasa" hizi kauli cjui anatafuta huruma ya watz au inakuaje! Jk umewekwa pale na tume ili uchakarike na kuta2a matatizo ye2 na co kuwa muombolezaji mkuu.
 
"sasa mafuta yamepanda bei mimi nifanyeje sasa" hizi kauli cjui anatafuta huruma ya watz au inakuaje! Jk umewekwa pale na tume ili uchakarike na kuta2a matatizo ye2 na co kuwa muombolezaji mkuu.

ama kwa hakika hatuna rais nchi hii,kama majibu ya matatizo yanayolikabili taifa hili ndo ya aina hiyo.Lakini huo ni muendelezo wa majibu yake kwa swali la "kwa nini tz bado ni masikini"alilowahi kuulizwa na mabwana zake huko ng'ambo!
 
Jamani tumechoswa na hizi kauli za JK,CCM na serikali zisizo na kichwa wala miguu.Ebu tujaribu kuijadili hotuba ya JK aliyo itoa Dodoma khusu swala la Dowans,Kama hayo aliyoyasema ni kweli sasa tujiulize Ngeleja alipokua akitoa kauli ya serikali imeamua kuilipa Dowans alikua anawasilisha mawazo ya nani?Ukizingatia kwamba yeye ni muhusika katika wizara hiyo na ni kiongozi katika serikali.Chiligati alipotoa kauli ya kua CCM imekubali kuilipa Dowans alikua anawakilisha mawazo ya nani?Je viongozi wa CCM na serikali waliookua wakiwakemea na kuwabeza Mh.Sitta,Mwakwembe,viongozi wa upinzani,wanaharakati n.k.Baada ya kauli ya kinara wao sasa watatuambia nini?!!Nakubariana kwa kauli ya Sir George Kahama akihojiwa na gazeti la mwananchi aliposema ya kua kauli nyingi za viongozi wa CCM na serikali hazioani na lengo au matakwa ya chama na wananchi bali masilahi ya viongozi.Na chama na serikali hakifanyi utafiti kabla ya kutoa kauli zao bali ukurupuka kila mtu kivyakevyake kauli ya kinara tumeisikia basi linalofuata tunategemea Ngeleja ,Chiligati na wote waliokua wakiwakemea viongozi wa upinzani,wanaharakatin.k kuomba msamaha na kufuta kauli zao na Ngeleja na Chilingati kuachia ngazi zao mara moja.Vinginevyo hotuba ya JK tutaichukulia kama ni shinikizo kutoka kwa wapinzani na jamii ni sio kauli yake na yote hayo ni mazingaombwe.TUMECHOSHWA NA MAZINGAOMBWE MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Source:MWANANCHI
JK aunga mkono Dowans isilipwe
Sunday, 06 February 2011 07:51


Hebel Chidawali, Dodoma na Fidelis Butahe
RAIS Jakaya Kikwete jana alitumia maadhimisho ya miaka 34 ya CCM kuvunja ukimya na kuzungumzia sakata la malipo kwa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans kiasi cha Sh94 bilioni akisema amaunga mkoTanesco isilipe deni la Dowans.

"..Nataka kuwahakikishia kuwa na mie ni miongoni mwa wale wasiotaka Tanesco ilipe..," alisema Rais Kikwete akizungumzia sakata hilo.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete kuhusu Dowans ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na Watanzania, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitoa maoni mbalimbali,huku baadhi yao wakienda mahakamani kupinga kampuni hiyo isilipwe.
Akihutubia wananchi katika kilele cha Sikukuu ya kuzaliwa kwa CCM, ambazo kitaifa zilifanyika mkoani Dodoma jana Kikwete alisema ameamua kusema wazi baada ya kupata shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali waliosema kuwa amekuwa kimya juu ya Dowans.

“Wapo wanaosema niko kimya au nashindwa kuchukua hatua, kwa sababu marafiki zangu wamehusika. Nawalinda. Kwa sababu hiyo, nikaona nami nisema angalau watu wanisikie, lakini sina la ziada ni yale yale yaliyokwishasemwa.
“Msemo wa wahenga wa akutukanae hakuchagulii tusi hapa umetimia. Napenda kuwahakikishia wana-CCM na wananchi wenzangu kuwa, sina uhusiano wowote wa kimaslahi, kwa namna yoyote ile na kampuni ya Dowans,” alisema Kikwete.
Rais Kikwete alisema hakutaka kuzungumza kuhusu Dowans kwa kuwa tayari lilikuwa limeshatolewa ufafanuzi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati .
“Sikuona umuhimu wa kufanya hivyo kwa sababu viongozi wenzangu wameelezea kwa ufasaha uamuzi wa Kamati Kuu na ule wa kikao cha pamoja cha Wabunge wa CCM,” alisema Rais Kikwete.
Alisema kuwa taarifa ya kutaka Tanesco iilipe Dowans Sh94 bilioni imeshtua wengi na kwamba yeye baada ya kupata taarifa hiyo aliuliza na kupewa ushauri mbalimbali.
“ Wapo waliosema lazima tulipe, wapo waliosema tusilipe, wapo waliosema tusiharakishe kulipa kwani kuna uwezekano wa kutokulipa kwa kutumia sheria,” alisema na kuongeza
“ Uamuzi wangu ukawa tusiharakishe kulipa, tutafute njia za kuepuka katika kulipa. Ndiyo maana ya taarifa ya Chiligati na ile ya Waziri Mkuu,” alisema Kikwete.
Alisema kuwa ni mzigo mkubwa kwa Tanesco kuilipa Dowans, hivyo ifanyike kila njia ili kuepuka kulipa deni hilo.
“ Tumewataka wanasheria wetu wasaidiane na wale wa Tanesco kuhakikisha hilo halitokei. Nataka kuwahakikishia kuwa na mie ni miongoni mwa wale wasiotaka Tanesco ilipe," alisema na kusisitiza:
"Kauli za mimi kuhusika na Dowans inanishangaza, maana nisingeamua hivyo katika Kamati Kuu(CC) na Kamati ya Wabunge wa CCM. Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi”alisema Kikwete."
Alisema kutokana na ukimya wake maneno mengi yalisemwa ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na kampuni hiyo Dowans na kufafanua kwamba jambo jingine lililomfanya kuzungumza kuhusu Dowans ni kauli kwamba hawezi kuzungumza kwa kuwa kampuni hiyo inahusishwa na marafiki zake.
“ Sina hisa zozote wala manufaa yoyote yale, Pia sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua kwa sababu ya rafiki yangu au hata kama angekuwa ndugu yangu kahusika. Maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu na Kamati ya Chama ya Wabunge wa CCM yalifanywa chini ya uogozi wangu,”alisema Kikwete.
Kuhusu suala la Katiba, Rais Kikwete alisema siyo sera ya wapinzani bali ni mali ya CCM ambayo tangu mtangulizi wake Benjamini Mkapa alishaianzisha, hivyo akasema na yeye ni muumini mzuri wa kutaka mabadiliko.
Alisema kuwa atawaambia wasaidizi wake waharakishe kupeleka muswada bungeni ili uweze kujadiliwa na wabunge ambao wataona ni namna gani mchakato huo utakavyotekelezwa ili kupata katiba mpya.
Kuhusu matatizo ndani ya CCM, alisema bila ya chama hicho kufanya mageuzi makubwa katika kubadili muundo na uongozi, kitakufa kifo cha mende.
Kikwete pia aliwaeleza mamia ya watu waliohudhuria kilele cha sherehe hizo za miaka 34 ya CCM, kuwa chama hicho kimeishiwa fedha na kwamba yako maeneo yanayosababishwa na viongozi wasiokuwa wabunifu.
Mwoshoni mwa mwaka jana gazeti hili liliwahi kuchapisha kichwa cha habari kuwa CCM hoi kifedha baada ya kupata habari kutoka ndani yua chama hicho.
Alisema katika mabadiliko makubwa yanayotarajia kuja ndani ya chama hicho kikongwe nchini, yataanza mara moja mwishoni mwa mwezi ujao wakati Kamati Kuu itakapokutana kupokea tathmini ya uchaguzi.
Akitumia maneno ya ukali Kikwete alisema: “Mabadiliko hayo yanatakiwa kuanza mara moja bila kuchelewa kwani ukongwe wa chama chetu pamoja na baadhi ya viongozi wanaweza kuwa ni mzigo unaokisumbua chama”.
Mwenyekiti huyo alisema mabadiliko hayo yanatakiwa kuendana sambambana matakwa ya watu wakiwemo kundi kubwa la vijana, ili wasije kiona chama hicho kuwa ni mzigo usiobebeka.
“Lazima chama kianze mchakato wa mageuzi kwani kuwepo kwa muda mrefu ndio hatari ya chama chetu, lakini pia tabia za baadhi ya viongozi zinaweza kuwa ni sehemu nyingine ya hatari hiyo hivyo. Nasema lazima chama kiwe kama nyoka anayeweza kujivua magamba yake na kuwa mpya wakati wote hilo litajadiliwa katika vikao vya kamati na utekelezaji wake utaanza mara moja ili kuongeza mvuto ndani ya chama chetu”.
Alisema chama kinatakiwa kukimbia kutokana na hali halisi ya namna walivyoiona katika mchakato wa uchaguzi ulipita hivyo wale ambao wanakwenda mwendo wa kinyonga lazima watabwagwa kuanzia Machi mwaka, huku akisisitiza kuwa mvuto huo uwapendezeshe vijana.
Kuhusu suala la mapato, alisema kwa sehemu kubwa CCM imeacha kusimamia vyanzo vyake na badala yake imekuwa ikitegemea zaidi fedha za ruzuku ambazo mara baada ya kupungua kwa viti bungeni, sasa ruzuku hiyo inaishia kulipa mishahara ya wafanya kazi tu.


Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alisema hata kwa miujiza hawezi kutimiza matakwa ya Watanzania wote katika kipindi cha uongozi wake wa miaka 10.


Alitolea mfano kuwa hata hayati Mwalimu julius Nyerere alishindwa kumaliza mambo yote ingawa alikaa kwa muda mrefu Ikulu kuliko marais wengine, hali kadharika pamoja na watangulizi wake akiwemo Benjamini Mkapa pamoja na Ali Hassan Mwinyi.

“Watanzania wasitegemee kuwa nitafanya mageuzi makubwa hata Mungu mwenyewe hakumaliza kuiumba dunia kwa siku moja, lakini pia hata Mwalimu aliyekaa muda mrefu hakumaliza matatizo ya Watanzania kwa kipindi chake”.


Kwa upande wa wananchi wa Dodoma ambao walimpa Kikwete zaidi ya asilimia 81 ya kura za urais , alisema mji huo utaboreshwa pamoja na kufikiria kuipanua Ikulu ya Chamwino iliyo nje kidogo ya mji, ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba ya rais.
 
Rais anapaswa kuelewa kuvaa uso wa huruma na kutafuta huruma ya wanachi hakusaidii lolote. kabili mahitaji yao ya msingi
 
Rais kasema baada ya kusikiliza ushauri mbalimbali wengine wakitaka tulipe,wengine tusilipe,wengine tusiharakishe... "uamuzi wangu ukawa tusiharakishe kulipa( Please note hajasema tusilipe ...amesema tusiharakishe..).

Maswali yangu kwa Kikwete:

1.Chiligati alisema mmekubaliana kulipa Dowans kwa kuwa ndio uungwana kuheshimu sheria na hicho kikao wewe ndio ulikuwa mwenyekiti na hatujasikia kuwa ulikana ile statement ya chiligati. Je sasa ile statement ya Chiligati ni kweli au la?Manake kama ulivyosema mwenyewe wewe ndio ulikuwa mwenyekiti wa hicho kikao na mlisema mtalipa ..

2.Pinda alisema kuwa Dowans italipwa kwa kuwa tumeshindwa kesi .Nini maoni yako >? Manake umetuambia kuwa ulikuwa kimya kwa kuwa Waziri mkuu kashaongea.

3.Watu pekee ambao wamesema kuwa Dowans isilipwe ni Sita na Mwakyembe .. WEWE umesema tusiharakishe kulipa hujasema TUSILIPE ILA TUSIHARAKISHE wenzako wamesema wazi tusilipe.

4. Vipi kuhusu Ngeleja .. alisema tulipe ...vipi utamfukuza kazi?

5. Vipi kuhusu Mwanasheria mkuu amesema tulipe wewe unasema tusiharakishe( Nasisitiza hujasema tusilipe)..nae vipi utamfukuza kazi?

6. Aisee....



halsu waandidhi wa habari hasa Television hivi hamuwezi kuandaa taarifa hivi kuonyesha mtililiko wote wa hii issue kwa ubunifu?Kwa mfano mnaanza pale ngeleja aliposema tunalipa,kisha mnamuweka chiligati aliposema tunalipa,kisha pinda ..kisha mnamuweka pinda tena baada ya kikao cha wabunge...halfu mnamweka JK..kaclip kama cha dakika tano hivi kwenye taarifa ya habari ..kwani zile recordings si bado zipo?Au mnaogopa ...


Aisee....
 
yaani yeye kama Raisi kwa nini awe analalamika tu, kwani kuna shida gani ya kupangua safu zote za uongozi maramoja? Hapo ndio utajua kuwa hapa hatuna Leader(Kiongozi) bali tuna ruler(mtawala) na follower.
 
ni mheshimiwa ni msanii tu, anataka kuomba huruma ya watanzania.!!!!
 
hahahahahah,ina maana kuwa zile ahadi zake asipozitekeleza msimuulize,dah!anajua kucheza na maneno,maana ahadi zake zilikua nzito sana na kuztekeleza ni kazi,any way ndo wanasiasa wetu
 
Kampeni ni kampeni tu. Au umesahau chenge alivyosafishwa? Mramba na wengineo?
 
Anasema hawajui Dowans wala hajawahi kukutana nao,je? anataka kutuaminisha kwamba hajui uhusika wa Rostam kwenye hilo,Rostam si rafiki yake?hakutani na Rostam? uongo na ujinga mtupu!
 
hii bongo yetu karibia mtu atatolewa utumbo mbele ya wasaidizi wake tumechoka na movies za kisiasa zinazoibuka kila siku na waigizaji ni wale wale sema wanakuja kwa sura nyingine
 
This is very strange!

A president, head of State, Chief in Command wenye kila resource mkononi mwake hajui nani anataka kuibia wananchi wake.
Kwenye kikao anachojisifu kukisimamia mwanachama wake (mwakyembe) kamtaja mmiliki kwa nini asimwite chemba kupata taarifa zaidi?

Kama ni kuua soo bora angesema "Nimesikia kuna watanzania wenzetu wanamasilahi kwenye Dowans, tunafuatilia ili kubaini ukweli ila wanapaswa kujua hii ninchi yetu sote, madhara ya kuihujumu wao hawawezi kusalimika"

Mie hata sijui kina nani wanamshauri cha kuongea
 
Katika maadhimisho ya miaka 34 ya ccm jk alitoa hotuba inayogusa mambo mbalimbali,
1.Dowans,anasema eti hata yeye anashangazwa na hilo swala la dowans,kwa amiri jeshi mkuu,mwenye mamlaka kamili anatoa kauli ya ajabu,badala ya kueleza mikakati ya kuzuia uhaini na ubakaji uchumi,ni dhahiri amekosa uhalali wa kuwa rais
2.Mauaji ya arusha,et yalisababishwa na chama flani kwa malengo ya kisiasa,ikiwa hana uelewa wa kujua chanzo cha vurugu arusha,kuwa ni uchakachuaji wa meya,na ni vita kati ya haki na udhalimu,jambo ambalo kila mtu analijua,Jk kushindwa kuujua ukweli huu umekosa uhalali wa kuwa rais
Jk simamia haki na ukweli
saa ya ukombozi ni sasa
 
Back
Top Bottom