Kikwete ajisafisha Dowans

Kikwete ajisafisha Dowans

Tunabanana hapa hapa Yeye ndiyo atatoka atuachie nchi yetu.Hanan hadhi ya kuwa Rais aliwahadaa watanzania

wewe ndo utaondoka make no mistake about it .Rais is here till 2015 dont like it go and live in vatican.
 
Mwenzetu uko hapa kwa interest ya nani?? If I may ask Bro'........................???

Ndugu yangu nipo kwa interest ya kili ninachoamini ni haki na ukweli kwa upeo wa ufahamu wangu. Hata hivyo sisemi kwamba kila mimi ninachokiona kuwa ni kweli na haki ni lazima kwa kila mmoja wetu kitakuwa kweli na haki. Ndio maana naomba mchango wenu kimawazo kunikosoa, kunielimisha au kuniunga mkono kama mtaona inafaa.
 
:msela:Watanzania wezangu, kuna kitu kimeniumiza sana ile siku ya miaka 34 ya CCM! Eti rais wetu hawajui DOWANS? Hivi kwa mtu makini anawezaje kukaa IKULU na huku kuna kampuni tata ambayo inatajwa tajwa kila leo kwenye vyombo vya habari na rais hataki hata kuwajua? Anashindwaje kuitisha faili la DOWANS kutoka BREILA ili kuwajua wamiliki? Kuna haja ya kuwa na rais ambaye hataki kujua kampuni hewa ambayo inakula pesa za walipakodi? Naomba kutoa hoja wajameniiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:msela:
 

JK haijui Dowans, Ngeleja anaijua, haa haaa haaaa! Hiyo ndiyo Tanzania!
 
JK ameona watanzania ni wajinga na ni mbumbumbu ndio mana akasema vile. In fact, maneno kama yale ni dharau ya hali ya juu na katika nchi nyingine angeadibishwa.
 
Amekiri kuwa Richmond ni kampuni hewa na ndiyo maana alimtahadharisha Msabaha kuhusu kuwalipa Richmond down payment, ameonekana kuutambua mkataba wa Dowans kwa kusema tumetumia umeme wa Dowans miezi tisa na kuutambua ushindi wa Dowans dhidi ya Tanesco ila baada ya malalamiko mengi ameemua serikali isiipe fedha Tanesco ili kuona jinsi ya kuweza kuepa au kupunguza malipo hayo!
Ukiangalia sana aliyoyasema hayaendani na yale aliyoyaeleza Chiligati baada ya kikao, Chiligati alisema wazi kuwa CC imeona kuwa ... ICC imeshamua na Uungwana ni kulipa ....ila kwa kuwa kuna baadhi ya watanzania wenzetu wamefungua kesi mahakamani kupinga malipo haya serikali itasubiri kulipa mpaka pale kesi hiyo itakapotolewa uamuzi...." . Version ya JK ni kuwa ... ila baada ya malalamiko mengi ameemua serikali isiipe fedha Tanesco ili kuona jinsi ya kuweza kuepa au kupunguza malipo hayo! ....., hizi statement Hazina maana sawa kabisa zaidi ya kuwalisha KASA wananchi.
 
Anajua anchokifanya! Alisubiri ili kucheza na hisia za watu. Laiti Mungu angekuwa na tabia ya kuadhibu pale pele, leo hii binadamu tungekuwa na adabu kweli! Tunaendeshwa na matukio!
 
IMG_2909.JPG


Duh! Siwajui wamiliki wa Dowans wala si marafiki zangu chagueni huyu!
mramba1.jpg

Jembe la zamani halizeeki chagueni pia ile kesi ni ndogo sana!

_49601633_kikwete-lowassa.jpg

Huyu alisingiziwa tu chagueni ni mtu safi pia!

chenge-kulia+na+mwezke-baiadi+wakinadiwa.JPG

Na mama alikuwepo kuwanadi watu swafiii kabisa!

normal_IMG_4710.jpg

Na hapa wanateta nini tena katikati akiwepo swahiba!
JKNAMKAPANEW.gif

Akiteta na Mzee wa Kiwira!

IMG_0383.jpg

Like a Fadher! Like a Son!
 
Ukiangalia sana aliyoyasema hayaendani na yale aliyoyaeleza Chiligati baada ya kikao, Chiligati alisema wazi kuwa CC imeona kuwa ... ICC imeshamua na Uungwana ni kulipa ....ila kwa kuwa kuna baadhi ya watanzania wenzetu wamefungua kesi mahakamani kupinga malipo haya serikali itasubiri kulipa mpaka pale kesi hiyo itakapotolewa uamuzi...." . Version ya JK ni kuwa ... ila baada ya malalamiko mengi ameemua serikali isiipe fedha Tanesco ili kuona jinsi ya kuweza kuepa au kupunguza malipo hayo! ....., hizi statement Hazina maana sawa kabisa zaidi ya kuwalisha KASA wananchi.

Mimi naona tunatofautiana kuitafsiri hotuba ya mh. Raisi japo ilikuwa katika lugha ya wazi. Mh. Raisi kabla hajaanza kuzungumzia suala la Dowans alirejea majibu ya mh. Waziri Mkuu na Mh. Chiligati na akasema wazi kwamba hana kipya zaidi ya walichosema na ndio maana aliamua kukaa kimya. Akaongezea kwamba kwakuwa watu nanapaza sauti kumtaka aongee na wengine kumhusisha binafsi na Dowans ameamua kusema. Alizungumzia chimbuko la kesi ya Dowans na msimamo wa serikali ambao anakubaliana nao na akasisitiza kwamba kwakuwa katika kikao chao kuna wataalamu wa sheria walionesha kwamba kuna namna ya kuepuka kuwalipa Dowans fidia sio busara kukimbilia kulipa haraka kabla ya kutumia mbinu za kisheria kuepuka.

Hapo sioni tofauti ya kauli zao. Hamna yoyote kati ya Waziri Mkuu na Mh. Chiligati aliyefurahia serikali kulipa deni. Wote walisema kwamba kama hamna namna yoyote ya kisheria ya kuepuka kulipa tutalazimika kuheshimu amri ya Mahakama. Ndio hici hicho mh. Raisi.

Najua kwamba wanaweza kuwepo baadhi yetu ambao kwa maslahi ya kisiasa wangependa viongozi wa serikali watofautiane ali wapate nafasi ya kusema kwamba nchi imewashinda. Lakini kwa hili hamna chochote kinachoonesha tofauti. "Mnyonge mnyongeni lakini haki yenu mpeni" wanasema waswahili.
 
Pendekezo langu katika katiba mpya itakayo andikwa kuwe na kifungu ambacho kitamuwajibisha kiongozi yoyote atakaye wadanganya wananchi wake hadharani.
 
Pendekezo langu katika katiba mpya itakayo andikwa kuwe na kifungu ambacho kitamuwajibisha kiongozi yoyote atakaye wadanganya wananchi wake hadharani.

Nakubali na kuongezea kwamba viwepo vifungu vingine vinavyowawajibisha wanasiasa au watu wengine wanaopotosha kwa makusudi matamko ya viongozi wa dola, Bunge na Mahakama. Na pia uwepo utaratibu rasmi wa kisheria wa kubaini kama kiongozi wa dola ameudanganya umma kuliko kumpa kila mtu uwezo wa kumhukumu kiongozi wa dola kwa hilo. Hiyo itazuia uwezekano wa sheria kutumika vibaya kwa ushabiki na maslahi ya kisiasa kama ilivyo sasa
 





headline_bullet.jpg
Asema hawajui wamiliki wake wala hajawahi kukutana nao
headline_bullet.jpg
Asema bado anasubiri wanasheria waeleze namna ya kuepuka deni hilo



CCCM(1).jpg

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wakati wa kilele cha sherehe za miaka 34 ya kuzaliwa CCM zilizofanyika mjini Dodoma jana.(Picha Freddy Maro)



Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa hana uhusiano wa namna yoyote wa kimaslahi na wamiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme wa Dharura (Dowans) na kwamba hawajui wala hajawahi kukutana nao.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 34 ya CCM mjini Dodoma jana, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho taifa, aliendelea kukanusha kuwa hana hisa, wala ajizi wala kigugumizi na suala la kuwachukulia hatua wahusika katika suala hilo.
"Sina uhusiano wowote wa kimaslahi na kampuni hii, siwajui, sijawahi kukutana nao kwa sababu hawana haja ya kukutana na mimi, sina hisa wala sina manufaa yoyote kwa hili," alisema na kuongeza kuwa:
"Sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua pale panapokuwa na kosa hata kama atakuwa ni rafiki au ndugu yangu,"alisema.
Kikwete alisema endapo angekuwa na maslahi binafsi, maamuzi yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya chama hicho ambapo yeye ni mwenyekiti yasingefikia hapo yalipo.
"Baadhi ya watu wamekuwa wakisikika wakisema kuwa mimi ni mmiliki wa Dowans, Watanzania jambo hili halina ukweli wowote na watu hawa wanalengo la kunipaka matope," alisema.
Akielezea sakata hilo lilivyoanza, Kikwete alisema kuwa mmoja wa waziri wake wakati huo alimfuata na kumtaka amsaidie ili Hazina waweze kutoa fedha dola za Kimarekani milioni 10 kama malipo ya awali kwa kampuni ya Richmond.
Alisema alimjibu waziri huyo kuwa maneno yanayosemwa kuhusiana na kampuni hiyo ambayo iliiuzia mkataba kampuni ya Dowans yanamtia mashaka na kwamba inawezekana yakawa ya kweli.
"Nilimwambia naungana na Hazina wasitoe fedha hadi hapo kampuni hiyo itakapoleta mitambo yake nchini, baada ya hapo kampuni hii iliamua kuuza mkataba wao kwa Dowans na wakaleta mashine hizo za kufua umeme," alisema.
Rais alisema kuwa suala hilo liliibuka bungeni na kuundiwa kamati ambayo ilibaini kuwa kampuni hiyo ni ya mifukoni (hewa).
Alisema hatua zilichukuliwa ikiwa ni pamoja na kuunda serikali mpya baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, na mawaziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha kujiuzulu.
Alisema "hawakuthibitisha ni ya fulani ama mwanaye na ningekuwa ni mimi nina hisa ama mmliki wake nisingetoa maamuzi hayo,".
Alisema kuwa kamati Kuu ya CCM iliyokutana hivi karibuni iliamua kuwa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), lisiharakishe kuwalipa Dowans bali itafute jinsi ya kuepukana na deni hilo.
Alisema kuwa serikali imewakusanya wanasheria waliokuwa wakitoa matamko mbalimbali ya jinsi serikali inavyoweza kuliepuka deni ili waweze kutoa maarifa hayo.
Katika sakata hilo, Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara ilitoa hukumu mwishoni mwa mwaka jana ikitaka Dowans ilipwe na Tanesco Sh. bilioni 94 kama gharama ya kuvunja mkataba.



SOURCE: NIPASHE JUMAPILI


3 Comments | View comments


 
"Sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua pale panapokuwa na kosa hata kama atakuwa ni rafiki au ndugu yangu,"alisema (JMK).

Sijajua kama angekuwa mtoto wake ama watoto wake angefanyaje ?
 
Nilivyosikiliza maazimio ya bunge jana....sakata hili halijaisha kama tunavyoweza kufikiria.

Ufunguo wa safe la mikataba umepatikana bungeni....watu wamepeana muda wa kuandaa majibu kama kawaida yao na kutegemea support ya kishabiki toka kwa wabunge wa ccm.

Maazimio ya jana ni kifo cha ccm na mzizi wa mafisadi sasa unaenda kufukunyuliwa. Tulio wasikia wakitajwa hadharani bungeni kuwa ni wahusika, hao ni viji dagaa vilivyotangulizwa viliwe na mamba ili akishiba aachane na mawindo ili papa wapone.

Lakini kwa maazimio yale ya jana, na wale wabunge wachache wakaendelea kuwa hai na misimamo isibadirike...tutashtushwa sana na yatakayokuja kuwekwa hadharani hapo mwakani.

Kuna uvundo mkubwa sana umefichwa na hapo ndio tutaelewa kiburi cha Maswi na Muhongo kilikua kinatokea wapi.

Mungu tujaalie hayo mambo yaendelee kuwekwa peupe na hatimae wote tuvune kwa jasho letu na sio hizi janjajanja na kupongezana kwa wizi.

Mastermind wao kesha pokwa nguvu za maamuzi bungeni na ndio walikua wanamtegemea kwa ubingwa wake wa mbinu za wizi akitumia elimu yake iliyogharamiwa na Taifa hili huko Havard lakini badala ya kuja kutusaidia ndio amekua kinara wa kutuangamiza. Damu mpya imefanikiwa kumnyofoa tena pasipo kuhitaji elimu ya Havard. Hakika nimefarijika sana na ninawaomba Wabunge wetu vijana waungane kulikomboa Taifa letu. Wazee wachache wenye uchungu na Nchi yetu, wasaidieni vijana hawa mbinu za kuwafichua wazee wenzenu wezi ambao mmekua mkiumia kwa miaka mingi kutokana na matendo yao ila busara ya kuoneana aibu na kusekana kwa nguvu za maamuzi mkashindwa kuwashitaki kwa wananchi. Mmepata njia sasa kupitia kwa vijana hawa na wala msiangalie mambo ya vyama kwa sasa bali ukombozi wa Taifa kwanza....tutarudi kwenye vyama baada ya vita vya ufisadi kuisha.
 
“Sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua pale panapokuwa na kosa hata kama atakuwa ni rafiki au ndugu yangu,”alisema (JMK).

Sijajua kama angekuwa mtoto wake ama watoto wake angefanyaje ?
Hapa ndipo nashindwa kumuelewa JK. Anatuambia kua hawajui wahusika au wamiliki halali wa Richmond/Dowans na angewajua angewachukulia Sheria. Sasa Mbona jana katuambia tena anawajua na hua wanazunguka na Lissu?

Tuseme hapo juu alikua anadanganya au ya jana ndio kadanganya?

Au inawezekana ikawa kauli zote mbili (ya hapo juu na ya jana) ni kauli sahihi? Kama ndio kivipi?

Na kama kauli mojawapo ya hizi sio kauli sahihi, anaweza kutusaidia kujua ni kauli gani zingine sio sahihi aliowahi kuzitoa?
 
jamii forums katika ubora wake wa kutunza kumbukumbu
 
Back
Top Bottom