"Kafulila adai JK hawajui Dowans, Ngeleja anawajua
Kwa upande wa mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi, David Kafulila, alimshangaa Rais Kikwete kusema hawajui wamiliki wa Dowans wakati waziri wake Ngeleja alikwishawataja.
"Ngeleja alikwishawataja wamiliki wa Dowans, inakuwaje Rais anasema hawafahamu..., suala hili linazidi kuwachanganya wananchi, inabidi likajadiliwe bungeni,"alirejea msimamo wa hoja yake anayotarajia kuiwasilisha bungeni kama ikikubaliwa.
Kafulila alifafanua kwamba, suala hilo likijadiliwa bungeni ndipo linaweza kutoa majibu sahihi kwa wananchi.
"Kwa ujumla Rais Kikwete kusema hawajui wamiliki wa Dowans ni kielelezo kuwa wale tuliotangaziwa na Waziri Ngeleja sio wenyewe kwani wangekuwa wamiliki Rais angewajua," alisema Kafulila na kuongeza:
Je waziri wake na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliposema lazima tulipe Dowans hawakumwambia wanamlipa nani?
Source: Mwananchi
JK ameshindwa kazi....watanzania hawadanganyiki teena!
Hii akili ya uchambuzi ktk Gazeti la Mwananchi na Kafulila mwenyewe ni zaidi ya akili ya JK kuweza kutoa hata ufafanuzi kidogo kujisafisha mbele ya umma.
Kumbuka kuwa awali alipokuwa anaanza kuelezea ktk hotuba JK alisema....kuhusu suala la Dowans, naona niseme...." mimi siwajui Dowans, wala Wamiliki wake, na wala hawana haja ya kunifahamu au kunihusu ili niwafahamu...na wala sina uhusiano wowote nao, sina hisa nao na hawanihitaji niwafahamu...nk"
Jamani....hii ndiyo kauli ya 'Rais' ambaye Waziri aliyemteua yeye alisema kuwa ..."wamiliki wa kampuni ya Dowans SA, ni kama ifuatavyo....(akawataja Maruhani wake wote ambao hata JK alipelekewa copy, ila RA hakutajwa!) " ... njia ya mwongo siku zote ni fupi!
Kama JK hawajui, je Ngeleja anasubiri nini ofisini asijiuzulu kwa kubuni wamiliki, au hawajibiki kumpa taarifa JK??
Na ktk kuthibitisha kuwa JK anajikanyaga (kudhihirisha uongo, au usanii wake) kila anapoongea maneno mawili au matatu zaidi mbele ya umma, midomo ilikuwa inamkauka kila baada ya dakika, (ambayo ni tabia ya mtu anayesema au kutetea uongo), hivyo ilimbidi kunywa maji au kujilamba-lamba! Na ktk kudhihirisha kuwa alikuwa anachonga uongo, alifikia pahala akajisahau au kwa kutokujua kuwa 'anajifunua' ndipo akasema...."ngoja tukumbuke historia ya jambo hili.....(ndipo akaeleza kila kitu kuhusu kampuni feki ya mfukoni - Richmond, na jinsi ilivyokuja kuuza mkataba wake kwa Dowans', na haya aliyaeleza kwa mtiririko kuliko akina Pinda na Chiligati walivyojitahidi hapo awali)..., " Na hadi akaitetea Dowans kuwa "....baada ya kupokea mkataba toka Richmond, ndipo Dowans maana walikuwa na mtaji mkubwa, wakaingiza mitambo mikubwa-mikubwa, ambayo ndiyo iliyotusaidia kuondoa kiza na tatizo lililokuwepo...."
Hapo ndipo tukagundua kuwa...jamaa anayesema 'siijui Dowans hii' kama Petro alivyomkana Yesu, 'simjui mtu huyu' ili naye asisulubiwe!....ila hapa JK ni zaidi, anaikana DOWANS, kumbe sio tu asisulubiwe -ambayo ni haki kama kiongozi, bali pia anawaficha wananchi wasiujue ukweli maana yeye kama 'mkuu wa nchi' alitakiwa atoe dira na ufahamu na udhalimu unaofanywa kwa umma na kuwa hata kama ikitokea awepo 'tapeli' atafichuliwa na mkuu wa nchi, kumbe ni ZERO!. Tofauti yake ni kuwa, hata mkuu wa nchi ameshiriki kuuficha ukweli....Hatari sana!
SWALI: Je; Na hapo baadaye ikijulikana kuwa alikuwa anawafahamu ataruhusu afanyiwe nini?? kifungo au umma utaamuaje? (Au, Labda kasema hawajui maana anajua 'nyaraka nyeti zitakuwa zimesachomwa na hivyo hakuna wa kuzipatana kum-link na udhalimu huu!!!);
Ila nguvu ya umma itatawala ukweli tu...Mungu ndiye mtawala....! hata siku ya mwisho hata Mfalme Suleimani alianguka....sembuse JK! hatajiepusha na anguko kutokana na matendo yake mwenyewe, kama kuudanganya umma ndio mafanikio, basi anaelekea asipojua bado...uongo haudumu, utafichuliwa punde. Ndio maana tunasema, Kwa sasa mpira JK kautupa mwenyewe kati uwanjani....'umma wa wananchi' uamue mwelekee, kama ni upande upi...kama uelekee upande wa 'Timu ya Umma' kwa ushindi wa haki, ukweli na nguvu au kwa 'Timu ya JK' inayotetea udhalimu na uozo??
.................Watanzania hawadanganyiki tena ng'o!