GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Tutake tusitake, jamaa ni Rais wetu mpaka 2015..subiri Oct, 2010 uone atakapogaragaza hao wasiojiamini hata kuomba kuchaguliwa na chama chao kuomba kuteuliwa kugombea Urais
Hapo kwenye RED! Hata akama atawagalagaza hao wasomi, Je Afya inaruhusu kufika huko? Tusije ingia gharama ya uchaguzi mwingine in between mkuu??
 
Hapo kwenye RED! Hata akama atawagalagaza hao wasomi, Je Afya inaruhusu kufika huko? Tusije ingia gharama ya uchaguzi mwingine in between mkuu??

SI UNAONA ALIVYOBEBWA HAPO KWENYE PICHA....anaweza kufanya maamuzi? Kumbuka haku delegate power
 
Masa hivi kifafa ni kejeli enh! Maana naona the way unavyoiweka hii ishu hapa unakuwa unawanyanyapaa wenye matatizo hayo. Unaonaje km tukiheshim utu wa watu? Na pia maisha ni safari ndefu saana.
Kuna wengine hata kuambiwa yeye ni mnene ni kumnyanyapaa, inategemea na uelewa wa mtu, kama wewe unafikiri mtu kuambiwa ana kifafa ni kejeli hilo ni tatizo la perception yako.
 
Nasikia kwenye mfungo inabidi wale vitu vyenye sukari nyingi
Sasa kama ni kweli ana kisurkari huwa wanapima sugar content ya futari ya Mheshimiwa.? Au wanapima food poison tu?

Wasije wakawa wanahangaika kumvalisha rais wetu Bullet proof huku wanampiga silencer za misosi.

Nimepata Wazo
Sasa CAG inabidi akakague ikulu inavyoshughulika na afya ya Rais na Misosi
 
Naona sirikali inabidi itufahamishe wadanganyika kulikoni mh. rahisi adondoke mara kwa mara jukwaani au kuna makubwa zaidi ambayo walalahoi wa nchi hatutakiwi kufahamu khs rahisi?Watatudanganya leo lakini ipo siku wadanganyika wataamka...
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
 
Akizungumza na wana habari katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana jioni kuelezea kuhusu tukio hilo la Kikwete kuanguka, mkuu wa kitengo cha habari cha kampeni za CCM, Kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana, alisema kilichosababisha hali hiyo ni upungufu wa sukari, kulikosababisha kushuka kwa shinikizo la damu.
“Kwa mujibu wa madaktari wake, sababu kubwa iliyosababisha tukio la leo ni upungufu wa sukari mwilini na kushuka kwa pressure, kwa sababu alikuwa amefunga,” alisema Kinana wakati akitoa maelezo yanayoshabihiana na yale ya mwaka 2005, ambayo pia yalihusisha tukio la Kikwete kuanguka kwa sababu ya mfungo.
Kinana alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wanachama, wapenzi na mashabiki wa CCM kwamba hali ya afya ya Kikwete ilikuwa njema na ataendelea na ziara yake ya kampeni leo hii mkoani Mwanza na kwingineko nchini.
Mbali ya hilo, Kinana alisema uamuzi wa Kikwete kufunga ulikuwa ni kinyume cha ushauri aliopewa na madaktari wake ambao walishauri asifunge.
Alisema tayari chama hicho na madaktari wake wameshachukua hatua zote za tahadhari ili kuhakikisha kuwa mgombea huyo wa urais anaendelea na kampeni zake za urais pasipo kukwama.
Katika hatua nyingine, mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, jana alimtumia Rais Kikwete salamu za pole kutokana na tukio la kuanguka kwake.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Dk. Slaa, alisema aliamua kumtumia salamu za pole Rais Kikwete kwa kuwa Watanzania wote ni ndugu na siasa si uadui.
Alisema kuwa anakumbuka kuwa Rais Kikwete alimtumia yeye (Slaa) salamu za pole aliposikia kuwa amevunjika mkono baada ya kuanguka bafuni mkoani Mwanza. “Mheshimiwa Rais nimepokea kwa masikitiko taarifa ya hali ya afya iliyokupata Jangwani leo, nakuombea sana upate nguvu haraka hasa katika kipindi hiki kigumu, nakupa pole sana sana.” Alisema Dk. Slaa katika ujumbe mfupi aliomtumia Kikwete.
 

Yaani kama wewe ni mtaalamu wa Afya ya "Binadamu" kweli kama ulivyosema....Tanzania tuna shida kubwa sana kuliko nilivyofikiria.
 
Tutake tusitake, jamaa ni Rais wetu mpaka 2015..subiri Oct, 2010 uone atakapogaragaza hao wasiojiamini hata kuomba kuchaguliwa na chama chao kuomba kuteuliwa kugombea Urais
Hivi huyu anayejiamini kapeleka wapi nchi? Miaka 10 ya kusaka urais hamna hata vision, hata sense of direction, ni tabasamu tu. Si afadhali hao wasiojiamini angalau wanajua limits zao. Huyu alidhani urais ni Holywood. Hamna hata aibu?
 
VIDEO ya MWELEKA iko wapi???

Mtu66,
Juu kabisa ya ukurasa huu kuna bangola Jamii Forum, chini yake kuna sentensi inasomeka: "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY" baada ya tukio la kuondolewa kwa Vidio inayoonyesha kuanguka kwa Mh. Rais naamini slogan hiyo imepoteza maana yake, itakuwa vizuri MOD aiondoe na kutafuta slogan itakyofanana na wapiga soga tunaopast time kwenye hii forum. Kuna mtu amefanya kazi yake vizuri kwani hiyo video imepotea toka mitandao yote. Hayo mambo ya akina KGB bado yamekumbatiwa tu?
 
Tatizo lake halijafichwa liliwekwa wazi baada ya kufanyiwa chunguzi Ufaransa wakati mnaendelea kupiga kelele CCM ndiyo wanafanya mtaji huo.Kuhusu hili hebu tuangali statistics za haraka haraka alianguka ktk kampeni za 2005 watu wakanena hamalizi term amemaliza na ktk hiyo miaka mitano ameanguka mara nne tunazoozielewa majukwaani na amesimama majukwani nje na ndani ya nchi zaidi ya mara 100.
 
Huu ndiyo utu na uugwana na hawa wawili wote wameuonyesha!Nawatakieni nyote kampeni njema na kila la kheri ktk hilo!
l
 

...duuh, safari ni ndefu!
 
Kuna mtu amefanya kazi yake vizuri kwani hiyo video imepotea toka mitandao yote. Hayo mambo ya akina KGB
hakuna cha u-KGB wala nini, video ilikuwa mtandao mmoja tu, YOU TUBE, wengine wana link tu, aliyeiweka kashaona dili kaiondoa, simple as that
 
...kampeni ni sawa na mbio za marathon.
Wasaidizi wa Mheshimiwa hawajamtayarisha rais wetu kwa hilo.
Hii ni siku ya kwanza ya kampeni jamani, dunia inatuangalia!
 
Halafu nna swali la kizushi, hivi ukiwa UWT bongo shurti uvae Kaunda suti??????????????????????
 
Halafu nna swali la kizushi, hivi ukiwa UWT bongo shurti uvae Kaunda suti??????????????????????

That could very well be their dress code...now I don't know how you would call it...is it business casual, business professional, or casual? For sure it is not casual....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…