Kuondolewa kwa clip inayomuoyesha Rais JK akila ngwala ktk viwanja vya Jngwani kwa ugonjwa usiojulikana bado imenishtua sana mimi!
Kupasha au kupashwa habari ni haki ya kila MTZ na ipo hata ndani ya katiba;inakatazwa tu kuleta habari za uongo,za uchochezi au hata za kuleta mgawanyiko wa kidini,kikanda na kikabila;lkn kama habari husika ni ya kweli hata kama inazungumzia ukabila,udini au hata siasa inaruhisiwa watu waisome kwa mujibu wa sheria!
As far I know;Kuanguka Jangwani kwa Rais JK ni tukio la kweli lisilokuwa na uongo hata punje;kujaribu kuondoa clip inayoonyesha kuanguka kwake Rais JK sio tu kunawanyima nafasi wa-TZ kuona wenyewe kuhusu mustakabali wa Rais wao bali ni uvunjaji mkubwa wa sheria ulioambatana na uoga usio na maana yeyote kwa wana JF na watz kwa ujumla
Nalaani vikali kwa kitendo hiki cha kuondolewa kwa clip inayomuonyesha Rais JK akidondoka kiwanjani Jangwani kwa sababu imenikosesha mimi niliye mbali na Dar kusoma na kuona kw amacho yangu mwenyewe kilichotokea ;hii inaanza kunipa hisia kali kuwa baadhi ya wagombea haswa wa CCM hawagusiki wala hawafai kujadiliwa kwenye jukwa la JF;na hii itaipunguzia JF heshima yake iliyoanza kujijengea kama ni chombo huru cha majadiliano kisichofungamana na chama chochote kile cha siasa!
Clip inayomuonyesha Rais JK akila mwereka kwa sababu ambazo bado Ikulu haijasema ni nini irudishwe mara moja tena bila masharti yeyote ile hapa JF!Kumbuka kuwa si sheria za usalama wa Taifa wala ya uchaguzi mkuu ya mwaka 2009 inayokataza watz wasione matukio yanayowapata wagombea wake ikiwemo kwa Rais kuanguka akihutubia!
Bado motto ya JF ni"wanachama wake wapo huru kusema na kuwaambia watz vitu vinavyotokea ili watz wengine wajue"?