Kikao cha Kamati zote za Bunge kilichokuwa kiongozwe na Spika Job Ndugai leo chaahirishwa

Ndugai atapaswa kujiuzulu si kwa kutofautiana kimawazo na Serikali bali ni kwa ujinga wake wa kuomba radhi kwa jambo ambalo si kosa na kuhalalisha mwenyewe kuwa amekosa sana
 
Magufuli alikuwa akikaa chato,wageni wote wa kitaifa na kimataifa alikuwa anawapokelea chato, au kwakuwa msukuma mwenzenu ndiomaana mlikuwa mnasifia tu kila kitu?! Mara ya mwisho nakumbuka Rais wa Kenya alienda chato akapewa na zawadi ya ndege wale Tausi
ulikuwa na bwana msukuma akakuacha ndiyo maana kila post unayoona unamkumbuka bwana wako wa zamani
 
Hizo taarifa za kujiuzulu nafasi zote ni uongo!. Kama ni kujiuzulu ni kujiuzulu uspika tuu, ubunge na ujumbe wa CC unaendelwa hadi kuitishwe kikao cha chama kumjadili. CCM hawafanyi mambo kienyeji kama wale wenzetu.
P

Mkuu lakini hizo nafasi za chama kama zinatokana na cheo cha uspika si itakuwa ni automatically pia?
 
Ndugai bado ni Spika bora zaidi kuliko.
pamoja na yote yaliyo tokea bado watanzania wengi wangependa kumuona anaendelea kukalia kiti hicho, isipokuwa wafuasi wa Mbowe/chadema.
Mhe. Spika Bado anahitajika sana ktk kipindi hiki.
Shida anaongoza kikundi cha kumuondoa Rais Madarakani hiyo ndio shida
 
Ndugai hawezi jiuzulu. Bunge ni mhimili unaojitegemea 🙄.Hivi Bunge na Mahakama vipo huru kweli ?Dictator Nyerere kweli alituachia majanga. Na kupata solutions ni ngumu. Mpaka wote waliozaliwa kabla ya uhuru wafe dunia.
Haki za kubak ofsn anayo
Ila haki ya kufanya kazi natakuwa nayo
Yaani ni sawa na boss kivuli
 
Leo kilikuwa kifanyike kikao maalum cha wawakilishi wa kamati zote za bunge chini ya uongozi wa Spika Job Ndugai. Kikao hicho ambacho kilikuwa kifanyike huko Unguja kimeahirishwa.

Sababu za kuahirishwa kwake hazijawekwa wazi ingawa zipo taarifa za ndani kuwa tayari Job Ndugai ameshajiuzulu nafasi zake zote ndani ya CCM na bungeni.
Ni kweli kajiuzulu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
kwaiyo kusema Nchi itapigwa mnada, kusema wananchi 2025 wataangalia wachague serikali inayokopakopa au waisaliti, we huoni Kama hizo kauli ni viashiria vya uhaini?

Jobo anaigombanisha serikali na wananchi,so ajiuzulu akawe mpinzani apinge vizuri sasa
Hii kauli ni kubwa sana
Sio ya kupuuzwa hata kidogo
 
Kiukweli mimi ni Tomaso, siamini!, mpaka nione, nisikie toka vyanzo rasmi.
P
Kwa mhemuko ulioonesha leo kwenye uzi huu hakika leo nami nimeamini kuwa wewe Pascal umo katika kundi la akina Ndugai.

Maana ulivyo ambiwa kuwa mwenzenu kabwaga manyanga umeshtuka Sana hata ukashindwa kuamini kuwa kuwa kujiuzulu inawezekana bila vikao.

Sasa umeonesha rangi yako halisi. Ila pole Sana maana utashi wa matamanio yenu umevuka hata hekima ya kawaida Ndiyo maana hata mmepanga mambo yenu bila tahadhari, ubavu wa kushindana na Rais kwa Katiba zetu za chama ccm haiwezekani.

Karibu sasa tuungane kudai katiba mpya maana matamanio yako basi tena.
 
Huyu ni mtu wa hovyo professionally kuwahi kupewa nafasi kubwa kama hiyo, it was a big risk kama nchi kumpa muhimili huu!

Ilikua ni issue ya muda tu! Bila kinyongo, fitna majungu wala mrengo wa kisiasa, naweza kuthubutu kusema hata siku moja huyu mtu hakuweza kua na level ya professionalism ukiacha tabia za wanasiasa vigeugeu aka fit kua mkuu wa mhimili huu!… msaidizi wake ni acdemically qualified (paper) ila reasoning na siasa zake ni wa hovyo as well!
 
Kwa mhemuko ulioonesha leo kwenye uzi huu hakika leo nami nimeamini kuwa wewe Pascal umo katika kundi la akina Ndugai.

Maana ulivyo ambiwa kuwa mwenzenu kabwaga manyanga umeshtuka Sana hata ukashindwa kuamini kuwa kuwa kujiuzulu inawezekana bila vikao.

Sasa umeonesha rangi yako halisi. Ila pole Sana maana utashi wa matamanio yenu umevuka hata hekima ya kawaida Ndiyo maana hata mmepanga mambo yenu bila tahadhari, ubavu wa kushindana na Rais kwa Katiba zetu za chama ccm haiwezekani.

Karibu sasa tuungane kudai katiba mpya maana matamanio yako basi tena.
Pasco yupo kundi Moja kina Ndugai
 
Back
Top Bottom