Kijue kitabu kilichotafsiriwa kwa lugha nyingi zaidi duniani

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Kitabu cha kwanza kutafsiriwa kwenda kwenye lugha nyingi ni Biblia, Ambayo ilitafsiriwa kwenda kwenye lugha takribani 3589.

Kitabu cha pili kutafsiriwa kwa lugha nyingi ni Don Quixote, riwaya iliyoandikwa na Miguel de Cervantes (Pichani), Riwaya hii huhesabiwa kuwa ni riwaya bora ulaya nzima, Na ilitafsiriwa kwa lugha zaidi ya 140.

Mwandishi wa Riwaya hii bwana Miguel alikua mtoto wa Daktari huko Uhispania, Alijiunga na jeshi akiwa na miaka 23 tu.

Alipokua akipigania nchi ya yake dhidi ya Milki ya Osman, Alijeruhiwa vibaya na kupoteza mkono wake wa Kulia.

Aliwahi kukamatwa na maharamia wa Algeria mwaka 1575 na kufungwa, Kisha akanunuliwa na Wamonaki Wakatoliki kama mtumwa kisha kuachiwa huru kwenda Nyumbani.

Aliwahi fanya kazi ya kukusanya Kodi miaka ya 1584 alipoteza sana Hesabu, kitendo kilichomfanya awekwe jela, ndipo kuanza Uandishi.

Mpaka anakufa alikua maskini, sifa za Uandishi wake zimekuja kupatikana baadae sana.

FB_IMG_1696271240064.jpg
 
Spoiler: Don Quixote alikuwa anapenda sana vitabu. Hasa vya mashujaa. Baadaye vikamfanya awe kama chizi. Akawa anajiona naye shujaa wa vita. Akatafuta farasi, mavazi ya vita na kijana msaidizi kisha akaanza harakati za kusaidia wanaoonewa. Ni kitabu cha comedy.

Ila inasemwa kitabu cha pili kwa kutafsiriwa kwenye lugha nyingi ni The Little Prince
 
Back
Top Bottom