Tunaendelea,,BALAA LA TANO,,Hapa kileji pamoja kuwa ni sehemu ndogo lakini Kuna sehemu ama kijiwe Cha starehe kinaitwa SHILAWADU aisee eneo Hilo sio powa .hapo vurugu zote kwanzia ulevi madawa ya kulevya ndo sehemu yake. ..Hilo eneo bangi Haina thamani,,sigara zenu za embasi,,sijui spoti na esiemu zinachukuliwa Kama takataka ..hapa ikola sigara maarufu na ya kijanja unaitwa SHIKATAA ,,aisee sio vijana sio wazee sio wakina mama sio wasichana wote wanakwambia sigara ni SHIKATAA,,sigara hiyo inatokea kongo huko mzigo huo ni zaidi ya mundende na vumbi la kongo unaambiwa ni BALAA..,,Hilo eneo la SHILAWADU ni noma usishangae kukutana na shangazi yako toka mkoani huko Arusha ,,songea,ama mwanza anajiuza ,,hapo warembo kutoka mikoa yote utawapata na gesti zote Kijiji kizima wamezikodi wao ..Kuna jamaa alikutana na mama yake mdogo kumbe anajiuza huku kwa wavuvi wakati nyumbani huko singida ameaga amekuja kufunga mzigo wa samaki,,hapo SHILAWADU ndani ya ikola pamoja na watu kupiga vinywaji vikali na vya gharama lakini pombe maarufu unaitwa TEVERE. ,,kunywa madude yako yooote Ila Kama hujanywa tevele watu wanakuona unaigiza ....ITAENDELEA.....