Kifahamu kijiji cha maajabu kinachoongoza kwa utalii Afrika, kinaelea kwenye ziwa

Happycuit

JF-Expert Member
Aug 18, 2013
638
530
ganvie-benin-106.jpeg
Ganvie ni kijiji kilichopo kwenye ziwa huko nchini Benin ambacho kiko katika Ziwa Nokoué, karibu na Cotonou. Kikiwa na idadi ya watu karibu 20,000, kikielezwa kuwa huenda kikawa ndio kijiji kikubwa zaidi kilichopo kwenye ziwa barani Afrika na ni maarufu sana kwa watalii.

Kijiji kiliundwa mnamo karne ya kumi na sita kuelekea karne ya kumi na saba na watu wa Tofinu ambao walikwenda ziwani kuepuka wapiganaji wa Fon ambao walikuwa wakikamata watumwa kwa kuuza kwa wafanyabiashara wa Ulaya hivyo walikimbilia sehemu ambayo walikuwa hawawezi kufikiwa kwa urahisi kipindi hicho.

Unaambiwa kuwa licha ya kukimbilia huko watu hawa kutoka kabila la Tofinu walijitahidi kukifanya kina cha ziwa hilo kuwa kirefu na visiwa vya Ziwa Nokoue na wakategeneza bandari yao maalumu. wanakijiji wa Ganvie mara nyingi huitwa “watu wa maji” na eneo lenyewe mara nyingi huitwa “Venice ya Afrika.”

Hapo awali walitegemea kilimo, ingawa kwa sasa kazi kubwa inayowapatia kipato kikuu za kijiji hicho ni utalii, uvuvi na ufugaji wa samaki. Njia pekee ya kusafirisha kwenda na kurudi kijijini ni kupitia boti za mbao.

Unaambiwa watu wanapenda kwenda kutalii katika kijiji hicho sio tu kwamba ni kizuri bali kuwaona watu wanaoishi katika eneo hilo pia jinsi maji yalivyokuzunguka na njia zao/vyombo vya usafi ambavyo ni boto za mabo.

Kinaitwa kijiji cha maji au kijiji cha maajabu

images (96).jpeg
EuqISfNWYAA_Pu6.jpg
 
Sipati picha mifumo ya kutolea uchafu kwenye hicho kijiji....au maji ndo yanamaliza kila kitu,,,,,samaki wa huko watakua wanakula sana eksikreta
 
Nasi Kule Kigoma, Ziwa Victoria, Nyasa, Natron, Waige Mfano Huo
 
UKIFUMANIWA UNARUKIA KWENYE MAJI UNAIBUKIA NYUMBANI KWAKO :cool::cool::cool:,
NASIKIA WATOTO WAKULEWANAAANZA KUJUA KUOGELEA KABLA YA KUANZA KUTAMBAA
 
Kina baba wameenda wapi naona kina mama tu na watoto kwenye picha apo ndio sokoni noma sana acha nikaishi huko.
 
Back
Top Bottom