Kijue Kijiji cha Ikola na watu wake

Pununkila

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
689
1,692
Wanabodi heshima kwenu, heri ya mwaka mpya.

Mwaka uliopita katika harakati za kusaka ndururu nikapata mchongo wa kwenda mkoa wa Katavi wilaya ya Tanganyika,tarafa ya Karema Kijiji cha Ikola. Mwanaume nikajikoki huyoo mpaka Katavi Mjini Mpanda. Kufika Ikola nikadandia ki-hiace masaa matano njiani tunakata pori...mida ya saa moja jioni naingia ndani ya Ikola.

Nampigia simu mwenyeji wangu anakuja kunipokea haoo mpaka nyumbani. Kwa kuwa ulikuwa giza tayari mwanaume nikaoga huyo nikalaza ubavu maana kila kiungo kilikuwa kinauma kutokana uchovu. Saa Tisa usiku naanza kusikia makelele ya watu nafungua dirisha kidogo kucheki nje naona wajuba wanapita na mandoo,tochi,masufuria,majiko, wanakielekea sipajui...,huku na huku kukakucha ebwanaeee kumbe nyumba ya jamaa yangu iko mita 35 kutoka ziwa Tanganyika.

Mwenyeji wangu anaamka ananiambia karibu Ikola Kijiji cha maajabu..kimoyomoyo nikasema safari hii nimeuvagaa.

ITAENDELEA.
===
MUENDELEZO
TUENDELEE,

BALAA LA KWANZA

katika mwambao wa Hilo ziwa hapa kijijini ikola Kuna bandari ndogo ambayo inapokea maboti yalioundwa kwa mbao kwaiyo yakifika hapa ikola yanapakia mizigo ya mazao yanapeleka Congo...Sasa kumbe Hawa watu wanaomiliki haya maboti wanarogana hakuna mfano..boti lako likionekana linafanya kazi Sana linazamishwa kichawi ziwani na upepo maarufu uitwao lukuga.

Sasa Kuna mwamba alipewa laki mbili akachote maji kwenye boti la mfanyabiashara mmoja ili hayo maji yapelekwe kwa mganga...mwamba akachukua dili Hilo huyooo mpaka kwenye boti akachota maji na kuyapeleka kwa aliemuagiza.

Basi baada ya siku mbili yule mwamba alietumwa kuchota maji kwenye boti akaanza kuota kidonda mkononi...baada ya wiki Hali ikawa mbaya...Kijiji hakina huduma ya afya zaidi ya maduka ya dawa tu...ikabidi apelekwe kwa mnganga kufika huko ikaonekana jamaa amerogwa kwa kuchota maji botini...ametibiwa na mnganga ikashindikana Hali yake ikazidi kuwa mbaya..ikabidi ndugu wamtafute mmiliki wa boti wamueze Hali halisi.

Mwenye boti akawaambia kuwa boti lake amelizindika kwa waganga zaidi ya ishirini kutoka kongo...kwaiyo hajui ni dawa za mnganga yupi zimempata ndugu yao..baada ya siku tatu mbele mgonjwa akakata Moto... ITAENDELEA
 
Nimewahi fika hapo Mwezi January, 2020. nakumbuka ilikuwa jioni sana tulisogea pembezoni mwa ziwa Tanganyika wakati jua linazama nilichoambiwa na wenyeji wangu ni kwamba "usiende kwenye maji peke yako hakikisha kuna mwenyeji karibu yako kwenye maji" .
 
Back
Top Bottom