Kijue Kijiji cha Ikola na watu wake

Kijue Kijiji cha Ikola na watu wake

Mbona unaandika kifupi sana mkuu. Jaribu kurefusha stori yako.
Wanabodi heshima kwenu....heri ya mwaka mpya..,mwaka iliopita katika harakati za kusaka ndururu...nikapata mchongo wa kwenda mkoa wa katavi wilaya ya Tanganyika,tarafa ya Karema Kijiji Cha IKOLA..mwanaume nikajikoki huyoo mpaka katavi mjini mpanda...kufika ikola nikadandia kihaisi ...masaa matano njiani tunakata pori...mida ya saa moja jioni naingia ndani ya ikola..nampijia simu mwenyeji wangu anakuja kunipokea haoo mpaka nyumbani...kwa kuwa ulikuwa Giza tayari mwanaume nikaoga huyoo nikalaza ubavu maana Kila kiungo kulikuwa kinauma kutokana uchovu....saa Tisa usiku naanza kusikia makelele ya watu nafungua dirisha kidogo kucheki nje naona wajuba wanapita na mandoo,tochi,masufuria,,majiko,,wanakielekea sipajui...,huku na huku kukakucha ebwanaeee kumbe nyumba ya jamaa yangu iko mita 35 kutoka ziwa Tanganyika....mwenyeji wangu anaamka ananiambia karibu ikola Kijiji Cha maajabu..kimoyomoyo nikasema safari hii nimeuvagaa..,,ITAENDELEA.
Inaonyesha na wewe utakuwa kachawi tuu. Kilichokupeleka huko ni kwenda kusaka dawa za kongo Ili mambo yaende vizuri.
 
TUENDELEE

Kwanza niwatake radhi ndugu zangu, naandika kwenye notipad halafu ndo nahamishia hapa, sasa simu ilijizima kabla sijasevu, ninatumia kitecno kinasumbua kweli.

BALAA LA PILI

Baada ya jamaa kukata moto, ndugu walikaa kikao wakatoka na azimio moja, kwamba kwa yeyote atakayekuwa amehusika na hicho kifo basi hatabaki salama, yeye na ndugu zake hadi mifungo yote wanayomiliki na panya walioko kwenye nyumba zao.
Wakamzika ndugu yao maisha yakawa yanaendelea.

Sasa yule jamaa aliyesema ameenda kwa waganga 20 alikuwa na mke na mtoto mmoja, siku moja wakatoka ili waende kuzunguka mjini, akapita kule kwenye boti yake ili aangalie kama wametia nanga kiusahihi. Mara mtoto akamwambia baba yake kwamba anataka kupanda boti, baba akamwita na mke wake wakaingia ili wazunguke kidogo ziwani. Sasa wakati wamefika mbele akaibuka yule mwamba aliyefariki, akazima injini, yule baba akashtuka, mara mtumbwi ukapigwa ukageuka. Hao wakawa wa kwanza kwenye ile listi.

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom