Kijana ukihitaji kuoa chagua mke kutoka kwenye familia ya kipato cha kati

Kijana wa sasa ambae hujaoa ila pia unategemea kuoa unapokuwa unatafuta mwenza jitahidi uchague mwanamke anaetoka kwenye familia ya kipato cha kati, vinginevyo itakuwa unaendeleza umasikini au utafanywa mgodi.
Sio kweli. Tajiri, mtu kati na maskini wote wanahitaji pesa. Tena wenye pesa wanahitaji pesa kubwa zaidi. Michango mikubwa mikubwa.
Maskini wanahitaji buku 10, buku 30, buku 50. Ukifikisha laki, unaabudiwa.
Familia zenye pesa au kipato cha kati sasa! Dah!
Watu wenye pesa sio wa mchezo mchezo!
Inaonekana kwa akili yako umejiandaa kuwa tegemezi au kuwa maskini.
 
Utajiri una mzigo wake kama ilivyo umaskini. Tena mzigo wa utajiri ni mgumu zaidi. Watu wenye pesa hawajiachii kwa lolote kama walivyo maskini. Hawana muda mwingi kama maskini. Utajiri ni mgumu kuutunza kama ilivyo kuupata. Na watu wa kipato cha kati iko hivyo hivyo.
 
Kijana wa sasa ambae hujaoa ila pia unategemea kuoa unapokuwa unatafuta mwenza jitahidi uchague mwanamke anaetoka kwenye familia ya kipato cha kati, vinginevyo itakuwa unaendeleza umasikini au utafanywa mgodi.
Hata Mtume Mungu ameeleza hivi kwenye Uislam. Mungu habahatishi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom