Kijana tafuta pesa upate mapenzi ya kweli

Kijana tafuta pesa upate mapenzi ya kweli

Mapenzi yanayoshikiliwa na pesa yanayeyuka kama ice cream
Hahahah halafu yana levels! Ukiwa una uwezo wa Tsh.10,000 akijitokeza wa Tsh.100,000 utashangaa sms hazijibiwi tu 😅😅😅 mapenzi ya mafungu hayo! Wanawake wa aina hii wananufaika na wanaume vilaza na wanaotapanya hela hovyo!
 
Umemaliza kila kitu mleta mada

Pesa inanogesha mapenzi

Kuwa na mpenzi asiyekuwa na vijisent ni kutafutiana lawama tu.

Utamvumilia weee kadri siku zinavyozidi kusonga, kama ataendelea kulia lia njaa na wewe mapenzi kwake yanapungua automatic

Wanawake nature yetu ni nyie kutulisha sisi

Wanaume msipingane na nature mnatakiwa kula kwa jasho!!!!

Au nasema uongo ndugu zangu.
 
Umemaliza kila kitu mleta mada

Pesa inanogesha mapenzi

Kuwa na mpenzi asiyekuwa na vijisent ni kutafutiana lawama tu.

Utamvumilia weee kadri siku zinavyozidi kusonga, kama ataendelea kulia lia njaa na wewe mapenzi kwake yanapungua automatic

Wanawake nature yetu ni nyie kutulisha sisi

Wanaume msipingane na nature mnatakiwa kula kwa jasho!!!!

Au nasema uongo ndugu zangu.
We sema tu humpendi mtu ila unapenda pesa zake
 
Wasalamu ndugu wana Jamii Forum,

Namshukuru Mungu kwa kutupatia uzima wa kuendelea kupeana mafunzo kupitia majukwaa mbalimbali ya kijamii mtandaoni hakika hatuna budi kusema asante Mungu.

Nianze kwa kusema mahusiano bila pesa yanawezekana kwa siku za mwanzo tu lakini ukata wa pesa ukizidi kwa muda mrefu kati ya mke na mume mapenzi huanza kufifia.

Mapenzi na pesa yanaenda pamoja, kijana tafuta pesa ndio uanze kuwaza kuwa na mwenza wa maisha. Ukiingia kwenye mahusiano bila kuwa na channel nzuri ya pesa utaona kila mwanamke ni mpenda pesa na utaishia kuugua magonjwa ya msongo wa mawazo na kushindwa kuishi katika lengo.

Kijana tafuta pesa upunguze wivu wa mapenzi kwa mwenza wako. Mtu asiye na pesa muda wote anakuwa na wasiwasi kwamba anaibiwa mwenza wake hivyo mwarobaini wa kukata huu wasiwasi na kutokujiamini ni kutafta pesa ndio uingie kwenye mahusiano.

Pesa inarahisisha upendo na ni waridi ya kuimarisha mahusiano hivyo kwa duniani ya sasa hakika yapaswa kuwa na msingi mzuri wa pesa unapojiandaa kuingia katika mahusiano kwasababu tupo kwenye dunia inayokumbwa na changamoto za magonjwa mbalimbali.

Leo hii mabinti wengi wanajifungua kwa operations tofauti na wakizazi kilichopita hivyo mwanaume tafuta pesa ndo uingie kwenye mahusiano , siku moja mke wako akishindwa kujifungua utumie pesa kuokoa maisha yake kwa kumpeleka hospitali haraka.

Kijana tafuta pesa upunguze kujieleza kwenye mahusiano na kuonekana muongo. Ukiwa huna pesa hata kama ukimwambia mkeo au mwenza wako mipango ya maisha na harakati unazopitia hata kama ni zakweli atakuona ni muongo. Hivyo tafuta pesa ili uaminike na kuheshimiwa.

Kijana kama umeachwa kwenye mahusiano kisa pesa,nakushauri usiingie kwenye mahusiano mapya, tafuta kwanza pesa ndio uanze tena mahusiano na hii itakufanya uepuke kulaani kila unapomuona kiumbe mwenye jinsia yakike huenda pia ukawa unakufuru kwa muumba wake.

Usitoe pesa kununua mapenzi bali tumia pesa kuimairisha mapenzi. Ukitumia pesa kununua upendo utakuja kujikuta unalaani hili andiko pasipo kujua unatakiwa utumie pesa kuimarisha mapenzi na mahusiano.

Kijana kama utaendelea kuamini kwa hiki kizazi cha hii karne kuwa mapenzi bila pesa yanawezekana basi jiandae kupendwa na wazazi wako tu. Tupo kwenye kipindi ambapo pesa ina umhimu zaidi ya upendo. Hadi matajiri wana achana japo wana pesa lakini hii nikutokana na pesa kuwa na thamani zaidi ambapo hii pesa inatumiwa kumaliza shida zote za dunia ya sasa.

Mwisho, Kijana jiimarishe na kujijenhea misingi imara ya pesa ili ukiingia kwenye mahusiano ujiandae kuzaa watoto watakaokuta umejiandaa kuwalea, kuwapatia elimu bora wasiwe omba omba na kuiga tabia zisizofaa na uwe chanzo.cha laana kwa watoto na kizazi chote.

Asanteni kwa kusoma andiko hili,unaweza kuongezea ama kutoa maoni yoyote,karibuni sana

mirajihathuman@gmail.com
 
Comments za wananchi zinaniacha hoi hadi sasa sijajua hela nazotafuta ni za kupata mapenzi au kuishi maisha Bora [emoji2363]
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Ila ladies [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yan shida sana
 
Wengine tulikuwa na pesa na bado hatukupata mapenz ya kweli

Ex wangu Ali ni cheat et afu akawa na yeye ana honga [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahahahhahahha,mbaya zaidi pesa zenyewe unapata kwa shida alafu bado anakunyonya na anampenda MTU mwinge
Nampa kumbe ana enda kumpa mwingine.

Mapenz ni upumbuva saiz Bora uwe na demu WA kuchapa na kusepa yaani Una mpa pesa Una chap asepe
 
Hata wenye pesa wanapigiwa wake zao. Yule mfalme kule UAE pamoja na mapesa yake chungu nzima mkewe pia wahuni walimpigia na kakimbilia UK.
 
Tajiri Bill Gate na Jeff wa Amazon wana pesa lakini wameishia kupeana talaka na waliokua wenza wao
Ebu acheni kufananisha matajiri na wanaume mafukara waliojazana huku bongo acheni kabisa hizo Stor sijui bilget kaachwa pesa inanguvu kubwa kwenye mapenzi mwanaume unakuwa uhakika wa kupata mwanamke mpya muda wowote
 
Back
Top Bottom