Kijana tafuta pesa upate mapenzi ya kweli

Mirr

Member
Jul 14, 2021
16
30
Wasalamu ndugu wana Jamii Forum,

Namshukuru Mungu kwa kutupatia uzima wa kuendelea kupeana mafunzo kupitia majukwaa mbalimbali ya kijamii mtandaoni hakika hatuna budi kusema asante Mungu.

Nianze kwa kusema mahusiano bila pesa yanawezekana kwa siku za mwanzo tu lakini ukata wa pesa ukizidi kwa muda mrefu kati ya mke na mume mapenzi huanza kufifia.

Mapenzi na pesa yanaenda pamoja, kijana tafuta pesa ndio uanze kuwaza kuwa na mwenza wa maisha. Ukiingia kwenye mahusiano bila kuwa na channel nzuri ya pesa utaona kila mwanamke ni mpenda pesa na utaishia kuugua magonjwa ya msongo wa mawazo na kushindwa kuishi katika lengo.

Kijana tafuta pesa upunguze wivu wa mapenzi kwa mwenza wako. Mtu asiye na pesa muda wote anakuwa na wasiwasi kwamba anaibiwa mwenza wake hivyo mwarobaini wa kukata huu wasiwasi na kutokujiamini ni kutafta pesa ndio uingie kwenye mahusiano.

Pesa inarahisisha upendo na ni waridi ya kuimarisha mahusiano hivyo kwa duniani ya sasa hakika yapaswa kuwa na msingi mzuri wa pesa unapojiandaa kuingia katika mahusiano kwasababu tupo kwenye dunia inayokumbwa na changamoto za magonjwa mbalimbali.

Leo hii mabinti wengi wanajifungua kwa operations tofauti na wakizazi kilichopita hivyo mwanaume tafuta pesa ndo uingie kwenye mahusiano , siku moja mke wako akishindwa kujifungua utumie pesa kuokoa maisha yake kwa kumpeleka hospitali haraka.

Kijana tafuta pesa upunguze kujieleza kwenye mahusiano na kuonekana muongo. Ukiwa huna pesa hata kama ukimwambia mkeo au mwenza wako mipango ya maisha na harakati unazopitia hata kama ni zakweli atakuona ni muongo. Hivyo tafuta pesa ili uaminike na kuheshimiwa.

Kijana kama umeachwa kwenye mahusiano kisa pesa,nakushauri usiingie kwenye mahusiano mapya, tafuta kwanza pesa ndio uanze tena mahusiano na hii itakufanya uepuke kulaani kila unapomuona kiumbe mwenye jinsia yakike huenda pia ukawa unakufuru kwa muumba wake.

Usitoe pesa kununua mapenzi bali tumia pesa kuimairisha mapenzi. Ukitumia pesa kununua upendo utakuja kujikuta unalaani hili andiko pasipo kujua unatakiwa utumie pesa kuimarisha mapenzi na mahusiano.

Kijana kama utaendelea kuamini kwa hiki kizazi cha hii karne kuwa mapenzi bila pesa yanawezekana basi jiandae kupendwa na wazazi wako tu. Tupo kwenye kipindi ambapo pesa ina umhimu zaidi ya upendo. Hadi matajiri wana achana japo wana pesa lakini hii nikutokana na pesa kuwa na thamani zaidi ambapo hii pesa inatumiwa kumaliza shida zote za dunia ya sasa.

Mwisho, Kijana jiimarishe na kujijenhea misingi imara ya pesa ili ukiingia kwenye mahusiano ujiandae kuzaa watoto watakaokuta umejiandaa kuwalea, kuwapatia elimu bora wasiwe omba omba na kuiga tabia zisizofaa na uwe chanzo.cha laana kwa watoto na kizazi chote.

Asanteni kwa kusoma andiko hili, unaweza kuongezea ama kutoa maoni yoyote,karibu sana.
 
Nina manzi mmoja anapenda hela kinoma, nilichokuja kugundua cko pekee angu licha hata ya hela nazo mpa.

Nilioona solution ni kusaidia wa nyumbani kwangu wallahi....nilimwambia manzi tuachane akasema fresh,tukaachana kweli mwezi hata hujaisha kaanza kunisumbua hatari eti anataka nimnunulie simu arooooooh.....ninunue simu ili atongozwe vizur hyo hamna asee, nyie wenye hela endeleeni kuimarisha mahusiano yenu.

Sisi mtuache na Puchu zetu asee.....

Home kwanza Mengine badaae
 
Nina manzi mmoja anapenda hela kinoma,nilichokuja kugundua cko pekee angu licha hata ya hela nazo mpa.

Hahahahhahahha, mbaya zaidi pesa zenyewe unapata kwa shida alafu bado anakunyonya na anampenda MTU mwinge
 
Wasalamu ndugu wana jamii forum,

Namshukuru Mungu kwa kutupatia uzima wa kuendelea kupeana mafunzo kupitia majukwaa mbalimbali ya kijamii mtandaoni hakika hatuna budi kusema asante Mungu.
Pamoja na hii ngonjera yote ulioandika hapa nasikitika kukwambia kuwa hamna mapenzi ya kweli yanayochipua palipo na pesa bali kuna maigizo ya mapenzi at large.

Najua hutambui kuwa mpenzi wako ana mpenzi wake huko alipo! Ana mpenzi wake ofisini ambaye wanaongozana pamoja muda wa lunch na kubembeana kwenye mabega, ana mpenzi wake kule chuoni ambaye hampi hata sh.100 ila anatumia zile laki mbili mbili zako unazomtumia kila week kumnunulia pamba kali na perfumes!

Endelea kutafta pesa ila ujue pesa sio suluhu ya mapenzi kama unavyojiongopea 😂😂😂! Siku huo mrija wa pesa ukikatika ghafla utajua hujui 😅
 
Pamoja na hii ngonjera yote ulioandika hapa nasikitika kukwambia kuwa hamna mapenzi ya kweli yanayochipua palipo na pesa bali kuna maigizo ya mapenzi.

Najua hutambui kuwa mpenzi wako ana mpenzi wake huko alipo! Ana mpenzi wake ofisini ambaye wanaongozana pamoja muda wa lunch na kubembeana kwenye mabega, ana mpenzi wake kule chuoni ambaye hampi hata sh.100 ila anatumia zile laki mbili mbili zako unazomtumia kila week kumnunulia pamba kali na perfumes!

Endelea kutafta pesa ila ujue pesa sio suluhu ya mapenzi kama unavyojiongopea 😂😂😂!
Ngoja watu waendelee kulisha wanaume wenzao
 
Nina manzi mmoja anapenda hela kinoma,nilichokuja kugundua cko pekee angu licha hata ya hela nazo mpa.

Nilioona solution ni kusaidia wa nyumbani kwangu wallahi....nilimwambia manzi tuachane akasema fresh,tukaachana kweli mwezi hata hujaisha kaanza kunisumbua hatari eti anataka nimnunulie simu arooooooh.....ninunue simu ili atongozwe vizur hyo hamna asee, nyie wenye hela endeleeni kuimarisha mahusiano yenu.

Sisi mtuache na Puchu zetu asee.....

Home kwanza Mengine badaae
Vipi yule wa Arusha bado uko nae?
 
Back
Top Bottom