Kijana, kujenga nyumba ni uoga wa maisha

Kijana umemaliza zako chuo ukapata ajira (mshahara hauzid 1m) basi ukafanikiwa kupata ki-mkopo kisichozidi 14m kisha unajitesa eti unaenda kununua kiwanja ili ujenge nyumba. Hivi niulize, utajenga chumba ama nyumba na 14m?

Acheni mawazo ya kimaskini, hiyo hela iingize kwenye biashara uzichange kwanza.
Usitake kila mtu afanye kitu unachofanya au anachofanya mtu fulani na usitake ktu anachofanya fulani kikufurhishe nafsi yako....... Nafanya kitu kinachonifurhisha nafsi yangu kama mimi naona kujenga nyumba ndo jambo la msing saana na litaifurhisha nafsi yangu najenga nyumba kama naona kusoma saana mpaka ma PhD ndo furaha yangu nitafanya hivyoo kama naona kuwa ma miradi mingi ndo furaha yangu na nafsi itafurahi nitafanya hivyoo........
KILA MTU ANAFANYA KILE ROHO INAPENDA
 
Nani kasema Wahindi hawajengi? Haya maflt ya huku Upanga na Masaki yanamilikiwa na nani? Quality Plaza na Quality Centre ni za Mmakonde yupi?
Wengi wao wamepanga kwenye maghorofa machafu mijini
 
Hata kujenga nyumba nayo ni biashara unaweza kujenga nyumba baadae ukaiuza kwa faida kubwa zaidi au ukaipangisha ukaendelea kuishi kwenye nyumba ya shirika.
Mifano tuliipata ss wa zamani kidogo kipindi hicho tuliwaona wanajeshi,polisi na wale wazee waliokuwa wanaishi nyumba za mashirika baada ya kustaafu aibu iliyokuwa wanaipata asikuambie mtu.
WOTE HATUWEZI KUWA WAFANYA BIASHARA WALA WOTE KUWA WAAJIRIWA
Usichojua mtoa mada kila mtu anafundishwa na kusomea kazi mbalimbali lkn hakuna elimu ya nn ufanyie mshahara wako unapoupata hiyo unaachiwa mwenyewe uamue sasa usitake wote tufuate mawazo yako mgando biashara ni zaidi ya uijuavyo hasa Tanzania ukifungua kabiashara tu halmashauri zinaona ndo sehemu zao za kupiga hela hawa ni baadhi ya wanyonyaji wa biashara zetu TRA,AFISA BIASHARA,FIRE,MABANGO,BIBI AFYA,TFDA,LEVY,KODI ZA FREM,USAFI TAKATAKA,UMEME USIO WA UHAKIKA NA MENGINEYO.
 
Haya mambo ya kukariri biashara ndiyo itakuwa msaada kwako huwa naona uvivu wa kufikiria, hivi mnafikiria watu wote tunavipaji vya biashara, hata kuuza vocha tu ukinipa mtaji lazima uishe, najiona siwezi biashara ya nn kuhangaika bora niijengee nyumba hata isipoisha nitamalizia baadae. Biashara kipaji jaman
 
Mwanaume nyumba ndiyo mama tunaitwa "Baba mwenye nyumba". Kila mtu ana priorty zake. Tatizo mnataka kujenga ndani ya mwaka umengia katika gorofa!! Miaka yetu kujenga nyumba took not less than 10 years ranging 4<x<10!!!.

Hii kali sasa miaka 10 unasubiria nyumba hiyo hiyo si itageuka gofu sasa na hizi mvua za Elnino au unakuja kuingia style ya nyumba ishakuwa ya kizamani, mlikuwa wavumilivu kweli kweli.
 
Hii kali sasa miaka 10 unasubiria nyumba hiyo hiyo si itageuka gofu sasa na hizi mvua za Elnino au unakuja kuingia style ya nyumba ishakuwa ya kizamani, mlikuwa wavumilivu kweli kweli.
Sure mkuu. Mimi nilitumia 8 years kukamilisha Nyumba tena kwa kuwa nilipata na ka trip ka Nje. Wenzangu miaka mpaka 15. Ilikuwa Nyumba ni jasho haswa. Leo hii KIJANA anaingia kampuni ya Simu anaanza kuchanga vihela vyetu ya airtime na Mpesa walioajiriwa bank wanaanza kuliza Hela ya suspense account na kuchomoa 2000 kila account ya mteja. Kesho eti wanatimua vumbi na Hummer na gjorofa. Thubutu.
 
Wakati nachukua mkopo mwaka 2007 wa 16M na kumalizia nyumba yangu pale Dom watu walinicheka sana, wenzangu wakanunua hiace na used coaster, ila usimamizi ukawashinda na wakaziuza zoote

Kwa ss nachukua 400,000 kiulaiiini! Maisha nikujipanga tu, na siku zote usimuige mtu kuishi
 
Kijana umemaliza zako chuo ukapata ajira (mshahara hauzid 1m) basi ukafanikiwa kupata ki-mkopo kisichozidi 14m kisha unajitesa eti unaenda kununua kiwanja ili ujenge nyumba. Hivi niulize, utajenga chumba ama nyumba na 14m?

Acheni mawazo ya kimaskini, hiyo hela iingize kwenye biashara uzichange kwanza.
Kweli mkuu ni wazo nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani umeangalia upande mmoja jambo hili kwa mwingine ni Bora ajenge awe na kwake na aepukane na shida za kupanga.

Na kwa mwenye mentality ya biashara ni Bora afanye biashara.

Maamuzi ya wote ni sawa kulingana na mtazamo wao wa maisha. Huwezi kulazimisha watu Wafanane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom