Chupaya aliuawa na kijana wake wa pekee kisa ni mapenzi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Chupaya alisoma masomo ya biashara pasi kujua huko mbele kutakuwaje. Aliajiriwa serikalini kwa muda mrefu akiwa Afisa biashara wa Wilaya. Siku moja katika kutoa leseni za biashara alikutana na Mhindi aliyemuomba wawe washirika katika biashara ya kupeleka matunda na mboga Arabuni.

Mchakato wa kupata vibali ulikamilika na walianza biashara kwa tabu kwani hawakuwa na mtaji mkubwa. Baada ya biashara kuanza walipata mkopo bank na kujikuta wana empire kubwa ya biashara. Chupaya aliacha kazi serikalini na kuwa CEO wa kampuni yake. Yule Mhindi aliamua kuweka makazi yake Arabuni kwenye soko na Chupaya akawa upande wa Tanzania.

Ndoa ya Chupaya alimuoa mtoto wa mjomba wake, alikabidhiwa binti yule na bibi yake mzaa mama baada ya mjomba na mke wake kufikwa na mauti na mtoto wao kulelewa na bibi yake. Katika usia alioachiwa na bibi yake, Chupaya aliusiwa asisababishe machozi yamtoke mkewe yeye awe mfariji wa mjukuu wake yatima.

Chupaya na mke wake walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume. Akiwa mdogo yule mtoto J’mosi alishinda na baba yake ofisini. Alifundishwa majukumu madogo madogo mfano kulipia umeme wa ofisi, kununua sukari ya chai ya wafanyakazi na hivi vyote aliambiwa aweke risiti na mwisho wa mwezi amueleze CEO matumizi yake ya mwezi mzima katika ofisi kwa ushahidi.

Mtoto wa Chupaya alipomaliza six form alikaa nyumbani gap year mwaka mzima na alipewa majikumu zaidi ofisini. Baada ya hapo alikwenda Canada kwa masomo ya juu.

Huku nyuma Chupaya alikutana na Rose binti wa Chuo. Chupaya alimpenda sana Rose, alimpa hela za shopping Dubai, alimpangishia nyumba na kumuwekea house girl. Alimnunulia kila alichotaka. Rose alijua kuwa Chupaya ni mume wa mtu, hakuwahi kumpigia simu, alipokea tu simu za Chupaya na massage alimuandikia kwenye Facebook massanger akiwa na shida ya dharura.

Chupaya alipendezwa sana na tabia ya Rose, hakuwa kama magumegune ya mjini. Alitamani kupata watoto na Rose lakini kila alikumbuka usia wa bibi yake wazo hilo alilitoa kichwani. Mke wa Chupaya hakuwa na sababu ya kupata maumivu. Alimpenda mume wake aliyetoka nae mbali. Chakula chake na Chupaya alipika mwenyewe mama wa watu.

Chupaya alipata wazo la kumkutanisha Rose na kijana wake atakapo rudi kutoka masomoni. Alimpenda Rose na hakutaka kumpoteza kabisa.

Baada ya kijana kurudi nyumbani kabisa, Walikutanishwa na Rose, Rose alimpenda mtoto wa Chupaya na ilifanyika harusi kubwa. Baada ya harusi, kijana alikabidhiwa kampuni na Chupaya na mke wake walihamia katika nyumba yao ya kijijini. Katika retirement package yake kama CEO wa kampuni Chupaya alinunua Jaguar kama gari yake ya kutembelea.

Alikaa kijijini kwa miezi takeibani mitatu kabla baba hajazua ugonjwa akidai mguu unamuuma na anakwenda kutibiwa mjini. Alikwenda kwa mtoto wake na kuanza tiba. Chupaya alisema hospitali wamesema ana saratani hivyo wamepata nyama kidogo kwa uchunguzi. Mke wake kusikia habari hizi alisononeka sana.

Kijana wa Chupaya aliipanua abiashara na kuanza kulima na kusafirisha maua ikiwemo mauwa ridi. Nyumbani alirudi usiku na mara nyingi alimpeleka mke wake kula nje ikiwa sehemu ya kukoleza penzi.

Kumbe bwana Chupaya haumwi ila ameamua kukaa mjini ili akumbushie kwa Rose. Mchezo mzima aliusoma mlinzi ambae aliumia sana kwani mtoto wa Chupaya alikuwa mtu mwema sana. Mlizi alijivika mabomu na kumtumia boss ujumbe kwenye simu. Kijana hakuamini alichosikia, alimfuata mama yake kijijini na walipanga mpango wa kumfumania Mzee.

Chupaya alikutwa akiwa na Rose chumba cha wageni, Kijana wake alimpiga risasi mbili kichwani
Roae
 
Ila kijana angevunga tu kwanza mzee kampa maisha , kwani mapenzi kitu gani bana mpk umlambe mzee wako risasi
Na nyie kina Rose , msituchanganye
 
Ila kijana angevunga tu kwanza mzee kampa maisha , kwani mapenzi kitu gani bana mpk umlambe mzee wako risasi
Na nyie kina Rose , msituchanganye
Laana ya bibi ilisababisha kifo cha Chupaya. Aliposababisha mke wake kutokwa na machozi, kuanzia aliposema ana saratani wakati haikua kweli. Pili alikutwa live akicheat na aliyetakiwa kuwa mkwe wao
 
Kwa hiyo ndiyo imeishaa? Nini kilitokea kwa muuaji, mke wake, mama yake, biashara yao?
MmuajiMuuaji alifungwa kwa kuua bila kukusudia, mke wa Chupaya alikua na access na account za mumeww Kwan’s alikua joint holder kwahiyo hakupata shida wakati kijana akiwa jela na aliweza kuweka mawakili wazuri waliosimamia shoo.

Rose alipotea mwenyewe maana aibu kwake ilikua kubwa. Baada ya kifungo kijana wa Chupaya aliendelea na kampuni iliyoongozwa na wafanyakazi pamoja na ndugu was mini fun kipindi akiwa jela.
 
Back
Top Bottom