Kijana afanya utani wa kutaka kumuua Rais Magufuli, aambuliwa kifungo cha miaka 2 jela

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,704
2,000

Rais John Magufuli.

MAHAKAMA ya Mwanzo ya Ipembe mjini Singida, imemhukumu mkazi wa mtaa wa Minga, Bahati Martin (39), kifungo cha miaka miwili jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kutamka maneno ya kwamba atamuua Rais John Magufuli.

Mshtakiwa anadaiwa kuropoka maneno hayo Novemba 26, mwaka huu, huku siku ya pili yake (Novemba 27) Rais Magufuli na msafara wake ukipita mkoani Singida kwa njia ya barabara kwenda Chato.

Hakimu wa Mahakama hiyo, Yohana Zakaria, alitoa adhabu hiyo juzi baada ya kusema mahakama imetibitisha pasi na chembe ya shaka kwamba mtuhumiwa alitishia kwa maneno hayo, kosa ambalo ni kinyume cha kifungu cha 89 (2) (9) sura ya 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Zakaria alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo katika eneo la kituo kikuu cha mabasi cha zamani mjini Singida, kwenye meza maarufu ya kuuzia magazeti, inayosimamiwa na kijana aliyetajwa kwa jina la John.

Alisema baada ya mshtakiwa kuropoka maneno hayo, mara moja raia wema waliripoti katika kituo kikuu cha polisi askari wa jeshi hilo walifika na kumtia mbaroni.

Kijana huyo aliyefungwa awali alikuwa akijihushisha na kazi ya kuonyesha picha, hususan mipira kupitia kibanda stendi hapo.

Hakimu Zakaria alisema baada ya kukamatwa na polisi, alikiri kutamka maneno hayo na hata alipopandishwa kizibani pia alikiri kosa lake.

Pamoja na kukiri huko, lakini alijitetea kwamba alifanya hivyo akiwa na lengo la kutania tu wala hakuwa na lengo la kuua.

Kabla ya kutolewa adhabu hiyo, Hakimu Zakaria alisema Rais wa nchi ni nembo ya taifa, hivyo mtu anapotishia uhai wake ni sawa na kutishia amani na usalama wa nchi kwa ujumla, hivyo mahakama inamtia hatiani kwa kosa alilofanya.

"Mshtakiwa pamoja na kuwa hujaisumbua mahakama hii inakupa adhabu ya kutumikia jela miezi 24 ili iwe fundisho kwako na wengine wanaokusudia kufanya kosa kama hili. Adhabu hii iwaogopeshe wengine wanaotarajia kufanya makosa ya aina hii," alisema hakimu.

Baada ya hukumu hiyo, mshtakiwa alipelekwa jela kuanza maisha mapya ya kutumikia kifungo chake cha miaka miwili.
 
For the English Audience
A Singida court sentences one Bahati Martin (39) to two years in prison for publicly saying that he would kill President John Magufuli.

Judge Zacharia said the defendant committed the crime at a popular newsstand around Singida bus terminal and was reported to the authorities by good Samaritans.

During the sentencing, the Judge insisted that this should be a lesson to other people. After his arrest, he confessed to saying the words, with the defense that it was a joke and he had no intention of actually causing the President any harm.

Many have engaged on this news, with some saying threatening the President is an offense that shouldn’t be taken lightly while others have said that his sentencing was easy as he confessed to committing the crime.

delako

JF-Expert Member
Oct 6, 2012
2,594
2,000
Katenda kosa tarehe 26/nov Leo tarehe 4/12 na hukumu tayari imeshatoka!!! Pongezi kubwa kwa Mahakama kwa kuendesha kesi ushaidi kukamilika na kutoa hukumu ndani ya wiki moja toka mshtakiwa kutenda kosa.Mahakama nyingine nchini kote ziige mfano huu maana kuna ndg, rafiki, jamaa zetu wengi sana wapo mahabusu bila kujua hatma ya mashtaka yao.
 

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
559
1,000
Ni kosa kisheria jamani, hata wewe ukitishwa kuuawa nenda kashtaki.Mimi nimewahi kumshtaki mtu kwa kunitamkia kwamba ataniua ila badae nikamuonea huruma sikwenda mahakamani mpaka kesi ikafutwa. Pamoja na hayo Rais ni nembo ya Taifa unatishia vipi kumuua hata kama unatania.

Tuache ushabiki wa kijinga.
 

Nyambiza jr

JF-Expert Member
Oct 5, 2018
805
1,000
Katenda kosa tarehe 26/nov Leo tarehe 4/12 na hukumu tayari imeshatoka!!! Pongezi kubwa kwa Mahakama kwa kuendesha kesi ushaidi kukamilika na kutoa hukumu ndani ya wiki moja toka mshtakiwa kutenda kosa.Mahakama nyingine nchini kote ziige mfano huu maana kuna ndg, rafiki, jamaa zetu wengi sana wapo mahabusu bila kujua hatma ya mashtaka yao.
Kesi ilikua rahisi kwa sababu alikiri
 
Top Bottom