Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
MASHEIKH WENGINE WATANO WAMEHUKUMIWA MIAKA 30, JELA LEO
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo tarehe 15.12.2023, imewahukumu Masheikh watano kifungo cha miaka thelathini jela.
Masheikh hao walikamatwa na watu wa Usalama mwaka 2014, na kuwahusisha na mlipuko uliotokea katika Hoteli ya VAMA iliyopo jirani ya Mahakama Kuu mjini Arusha.
Masheikh hao ambao wamepewa kesi nyingi zikiwamo za ulipuaji wa mabomu maeneo mbalimbali wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 9, kwa sababu ya upande wa serikali kudai wanatafuta ushahidi.
Katika muktadha huo wa kupewa kesi nyingi ndio leo wawili katika waliokwisha hukumiwa kunyongwa (jumanne ya tarehe 12.12.2023), na wao wamehukumiwa kwenda jela miaka 30.
Akitoa hukumu hiyo Jaji S.M. Magwaiga alisema ameridhishwa na ushahidi wa upande wa serikali na mlinzi wa Hoteli kwamba Masheikh hao walifanya jinai ya kutupa bomu katika mgahawa huo.
Masheikh walio hukumiwa ni:
1. Iddi Salum Abdallah.
2. Rajabu Yakubu Abdallah.
3. Amani Mussa Pakasi.
4. Yusufu Ali Huta (aliyekwisha hukumiwa kunyongwa) na-
5. Abashar Hassan Omari (aliyekwisha hukumiwa kunyongwa).
Akisoma hukumu hiyo Jaji Magaigwa alisema anawapunguzia adhabu Iddi Salum Abdallah, kutoka miaka 18, aliyo mhukumu atatumika miaka 9, jela na waliosalia (wakiwemo wale waliokwisha hukumiwa kunyongwa) wataishi jela miaka 21, baada ya kuwapunguzia miaka 9, na wao.
Jaji Magwaiga alimaliza kwa kuwaambia:
“mnaweza kukata Rufaa mwende kwa wazee watatu maana mimi ni binadamu naweza kuwa nimekosea”.
Adhabu mpya kwa Masheikh hao wanaanza kutumikia leo.
Pia, soma:
Arusha: Masheikh 6 wahukumiwa kunyongwa hadi kifo