Chozizwa2020
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 912
- 852
Mkuu kweli kabisa KATIBA MPYA ni muhimu sana kwa sasa. Ebu fikria mtu anaamka tu na kuanza kubomoa nyumba za watu bila hata sababu za MSINGI na bila hata FIDIA, ukimuuliza anakwambia kuwa ardhi ni mali ya Serikali na ni ya rais, na ameamua kujenga barabara 8. Mwisho wa siku baada ya kubomoa nyumba za watu anabaki na li-ardhi takribani kati ya mita 80 hadi 100 kila upande hana kazi nazo na hivyo anaanza eti anakodisha!!!! Kweli!! I we serous na maisha ya watu wetu?Nchi hii pekee ndiyo tuliyopewa bila malipo na Mungu,tuipiganie itoke kuwa la hovyo Mkuu.
Tudai Katiba itakayoweka upya misingi ya Tanzania tuitakyo sisi Wananchi.
Tumechoka kuishi Tanzania ya kina magufuli,CCM,V-wonder au ya wanyonge.
Uhuru wetu hauwezi kupimwa kwa kipande cha mkate.