Katiba ikiheshimiwa na kulindwa basi Taifa litabaki salama na umoja muda wote. Tujifunze kupitia maandamano ya 24/01/2024

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Niwapongeze CHADEMA kwa kuandaa maandamano haya muhimu. Mimi huwa nadeclare interest mara zote kwamba ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Sijawahi kuwa nje ya chama hiki asilani. Lakini kuna wakati mnauguza mgonjwa na haponi hivyo mnaomba Mungu amtwae kumpunguzia mzigo. Mgonjwa hakimbiwi

Kuhusu maandamano naamini kupitia CHADEMA ninajifunza jambo moja kubwa nalo ni UTHUBUTU, UMAKINI na UJASIRI.

Tunaweza kujitia upofu kwa kuanza kumpongeza Samia kwa kuruhusu maandamano. La hasha! Tunapaswa kuienzi Katiba ambayo imetoa haki ambazo watawala wamekuwa wakizitoa kama hisani. Rais anawajibika kwa Watanzania na siyo chama chake pekee.

Kwa minajili ya nchi kusonga mbele ni lazima sana tukubali kuwa tofauti zetu ni kwa minajoli ya kujenga na siyo kubomoana na kutafutana kama magaidi.

TUnashuhudia chawa wakitamba huku wakifanya uhalifu wa charracters assassinations kwa wenye maoni na mtazamo tofauti na watawala. Tumeona namna ambavyo watawala wakitumia hazina ya nchi kujenga taswira zao badala ya kutimiza ahadi na malengo mtambuka ya nchi.

Leo, Samia anaongoza Taifa ambalo limejaa hofu na uoga mkuu. Watu wanaogopa kukosoa pale mambo yanapokwrnda vibaya kwa hofu ya kushughulikiwa. Taasisi kama vile TRA, Polisi, TISS, DPP na mhimili wa Mahakama vimekuwa ni vyombo vinavyotumika kukandamiza hoja na fikra kinzani. Tanzania ya Samia na kabla ya Samia imekuwa na utamaduni wa kuwapa jina baya wale wambao hawaendani na fikra za watawala.

Karibia asilimia 99% ya watumiaji wa JamiiForums tumekuwa salama muda wote kwa kutumia majina bandia ili tuweze kutimiza haki yetu ya kikatiba ya kutoa maoni na kujumuika na wengine kutumia haki hiyo. Tumeona namna ambavyo mwanzilishi wa JamiiForums ndugu Maxence Melo alivyosulubiwa mahakamani kwa sababu ya kulinda uhuru wa maoni kwa kutotoa taarifa za mtumiaji wa JF ambaye alitoa taarifa iliyoisaidia serikali kung'amua wizi wa mafuta ghafi bandarini. Badala yake serikali ikaamua kutumia nguvu zake zote kutaka kumshughuulikia mtoa taarifa badala ya kuzifanyiakazi taarifa hizo.

Hivyo tunavyojisahau leo kwa kumpongeza Samia kuwa amekuwa mwanademokrasia kwa kuruhusu maandamano ni sawa na kujiingiza kwenye mtego wa kifo cha demokrasia.

Tutakuwa na neno la kumshukuru na kumpongeza Rais Sania pale atakapo ataridhia mchakato wa akatiba Mpya ya Wananchi na kuheshimu kanuni ya wananchi ndiyo wenye nchi.

Kuhusu jeshi letu la Polisi, hatuna cha kuwapongeza kwa sababu wao wanafuata amri. Wale wale waliokuwa wanawapiga risasi za moto waandamanaji ndiyo hao hao walioongoza kulinda maandamano ya tarehe 24 January 2024. Hivyo polisi wanafuata amri huku wakiweka kando utashi wao wa utii kwa Katiba na Sheria.

Ninatoa kongole kwa Jeshi letu la Wananchi kwa kutoshiriki mazonge ya kisiasa kama ambavyo Mkuu wa Mkoa alivyowataka washiriki.

Ninakubali kwamba, safari bado inaendelea kuutafuta uhuru wa kweli wa Tanzania (Tanganyika). Hatua elfu moja huanzia na moja.
 
Maneno Mazito sana haya....Mkuu
Mkuu wangu.
Kuna wakati tunajutafuta kama nchi inayosubiri kuvumbuliwa.

Tuna watawala ambao wanaamini mtu anapokuwa kiongozi basi hapo hapo anakuwa superhuman na superbrain kuliko wale wote anaowaongoza

Tunayaona hayo kupitia tambo zao, amri zao hata visions zao zisizokuwa msaada kwa Taifa.

Hebu tufikirie issue ya Umeme, Sukari, Maji hata kipindupindu na kadhalika ni mambo ambayo kwa wenye akili wanaona namna tunavyofanywa wapuuzi.

Tujitambue na tusikubali kuwa wajinga tena.

Mama Samia bado anao muda wa kufanya yaliyowashinda waasisi na watangulizi wake. Lakini akiendelea kuishi kwa muono wa wanaoangalia usalama wake asidhani wanamjali sana bali wanazingatia usalama wao waendelee kuneemeka na familia zao.

Tuanze mabadiliko leo ili wajukuu zetu waje kukamilisha hii safari ya mabadiliko
 
Tume huru tuitakayo ni Ile ambayo;

1. Rais hatoteua wakurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, wachaguliwe na Tume huru.

2. Matokeo ya Urais yatahojiwa mahakamani na kukatiwa Rufaa.

3. Mgombea HURU aruhusiwe kugombea bila kuwa chama Cha siasa. Uwepo mchujo wa wagombea huru Ili apatikane mmoja pekee wa kushindana na wenye vyama.

4. Pasiwepo mgombea apitaye bila kupingwa.

5.Kinga ya Rais,Spika kutoshtakiwa iondolewe. Rais aweze kushtakiwa mahakamani kama Raia wengine endapo atavunja Katiba.
 
Mie nikajua kila FISIEM ni chizi kumbe mpo wenye akili zenu timamu, mie nilikuwa nikimuona mtu tu mwanachama wa chama chocgote cha siasa namuona tayari FUSE imekufa 😂🤣

Mnisamehe kwa mawazo mgando, japo yana ukweli 90% 😂🤣
 
Kanuni ya MwanaTanu ya Nitasema Kweli Daima..... imesalia ktk historia.
Ukijaribu kuitendea haki ndani ya chama itapelekea historia yako kushabihiana na ya Kolimba aliyesema ukweli kwamba CCM imepoteza dira na mwelekeo.
 
Siku hizi siasa imeingiliwa na uchawa, watu wanasifu na kuabudu mradi mikono yao iende kinywani
 
Bandari imegawiwa na hawa CHADEMA kwa wivu wao na umalaya wa Kisiasa wakawasaliti 'Sauti ya Watanganyika' Walishindwa kufanya chochote.
Niwapongeze CHADEMA kwa kuandaa maandamano haya muhimu.
Ndio tumeona walivyojipoteleza.
 
Niwapongeze CHADEMA kwa kuandaa maandamano haya muhimu. Mimi huwa nadeclare interest mara zote kwamba ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Sijawahi kuwa nje ya chama hiki asilani. Lakini kuna wakati mnauguza mgonjwa na haponi hivyo mnaomba Mungu amtwae kumpunguzia mzigo. Mgonjwa hakimbiwi

Kuhusu maandamano naamini kupitia CHADEMA ninajifunza jambo moja kubwa nalo ni UTHUBUTU, UMAKINI na UJASIRI.

Tunaweza kujitia upofu kwa kuanza kumpongeza Samia kwa kuruhusu maandamano. La hasha! Tunapaswa kuienzi Katiba ambayo imetoa haki ambazo watawala wamekuwa wakizitoa kama hisani. Rais anawajibika kwa Watanzania na siyo chama chake pekee.

Kwa minajili ya nchi kusonga mbele ni lazima sana tukubali kuwa tofauti zetu ni kwa minajoli ya kujenga na siyo kubomoana na kutafutana kama magaidi.

TUnashuhudia chawa wakitamba huku wakifanya uhalifu wa charracters assassinations kwa wenye maoni na mtazamo tofauti na watawala. Tumeona namna ambavyo watawala wakitumia hazina ya nchi kujenga taswira zao badala ya kutimiza ahadi na malengo mtambuka ya nchi.

Leo, Samia anaongoza Taifa ambalo limejaa hofu na uoga mkuu. Watu wanaogopa kukosoa pale mambo yanapokwrnda vibaya kwa hofu ya kushughulikiwa. Taasisi kama vile TRA, Polisi, TISS, DPP na mhimili wa Mahakama vimekuwa ni vyombo vinavyotumika kukandamiza hoja na fikra kinzani. Tanzania ya Samia na kabla ya Samia imekuwa na utamaduni wa kuwapa jina baya wale wambao hawaendani na fikra za watawala.

Karibia asilimia 99% ya watumiaji wa JamiiForums tumekuwa salama muda wote kwa kutumia majina bandia ili tuweze kutimiza haki yetu ya kikatiba ya kutoa maoni na kujumuika na wengine kutumia haki hiyo. Tumeona namna ambavyo mwanzilishi wa JamiiForums ndugu Maxence Melo alivyosulubiwa mahakamani kwa sababu ya kulinda uhuru wa maoni kwa kutotoa taarifa za mtumiaji wa JF ambaye alitoa taarifa iliyoisaidia serikali kung'amua wizi wa mafuta ghafi bandarini. Badala yake serikali ikaamua kutumia nguvu zake zote kutaka kumshughuulikia mtoa taarifa badala ya kuzifanyiakazi taarifa hizo.

Hivyo tunavyojisahau leo kwa kumpongeza Samia kuwa amekuwa mwanademokrasia kwa kuruhusu maandamano ni sawa na kujiingiza kwenye mtego wa kifo cha demokrasia.

Tutakuwa na neno la kumshukuru na kumpongeza Rais Sania pale atakapo ataridhia mchakato wa akatiba Mpya ya Wananchi na kuheshimu kanuni ya wananchi ndiyo wenye nchi.

Kuhusu jeshi letu la Polisi, hatuna cha kuwapongeza kwa sababu wao wanafuata amri. Wale wale waliokuwa wanawapiga risasi za moto waandamanaji ndiyo hao hao walioongoza kulinda maandamano ya tarehe 24 January 2024. Hivyo polisi wanafuata amri huku wakiweka kando utashi wao wa utii kwa Katiba na Sheria.

Ninatoa kongole kwa Jeshi letu la Wananchi kwa kutoshiriki mazonge ya kisiasa kama ambavyo Mkuu wa Mkoa alivyowataka washiriki.

Ninakubali kwamba, safari bado inaendelea kuutafuta uhuru wa kweli wa Tanzania (Tanganyika). Hatua elfu moja huanzia na moja.
Ninatoa kongole kwa Jeshi letu la Wananchi kwa kutoshiriki mazonge ya kisiasa kama ambavyo Mkuu wa Mkoa alivyowataka washiriki.

Ninakubali kwamba, safari bado inaendelea kuutafuta uhuru wa kweli wa Tanzania (Tanganyika). Hatua elfu moja huanzia na moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bandari imegawiwa na hawa CHADEMA kwa wivu wao na umalaya wa Kisiasa wakawasaliti 'Sauti ya Watanganyika' Walishindwa kufanya chochote.

Ndio tumeona walivyojipoteleza.
Kuna wakati wa kuyaachilia mengine yaende ili kuepuka kutoka relini
 
Kumpongeza Rais Samia HAKUEPUKIKI. Mbona yule DHALIMU hakutaka kusikia kitu kunaitwa maandamano? Na kumbuka Februari 16, 2018 tulimpoteza mwanafunzi mbichi kabisa Akwilina Akwelini kwa UNUNDA wa Magufuli!!

Halafu wajinga humu bado eti WANAMKUMBUKA Magufuli. Nyambaaaaf
 
Attachments

  • Screenshot_20240125_090244_Google.jpg
    Screenshot_20240125_090244_Google.jpg
    83.5 KB · Views: 1
Kumpongeza Rais Samia HAKUEPUKIKI. Mbona yule DHALIMU hakutaka kusikia kitu kunaitwa maandamano? Na kumbuka Februari 16, 2018 tulimpoteza mwanafunzi mbichi kabisa Akwilina Akwelini kwa UNUNDA wa Magufuli!!

Halafu wajinga humu bado eti WANAMKUMBUKA Magufuli. Nyambaaaaf
Je muungwana wa Msoga aliruhusu maandamano?

Dhalimu ni CCM kwa kutuwekea katiba inayotumiwa na hao mnaowslaani kutukandamiza. Endapo Katibabingekuwa bora tena jumuishi, unadhani ungesema YULE DHALIMU leo?

Usihangikie na ulipoanguka, deal na kisiki kilichokukwaa
 
Tume huru tuitakayo ni Ile ambayo;

1. Rais hatoteua wakurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, wachaguliwe na Tume huru.

2. Matokeo ya Urais yatahojiwa mahakamani na kukatiwa Rufaa.

3. Mgombea HURU aruhusiwe kugombea bila kuwa chama Cha siasa. Uwepo mchujo wa wagombea huru Ili apatikane mmoja pekee wa kushindana na wenye vyama.

4. Pasiwepo mgombea apitaye bila kupingwa.

5.Kinga ya Rais,Spika kutoshtakiwa iondolewe. Rais aweze kushtakiwa mahakamani kama Raia wengine endapo atavunja Katiba.
Huu ndio uahalisia tunaoutaka kwenye katiba yetu.
 
Back
Top Bottom