Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,024
- 1,616
Akihitimisha Kikao cha Mafunzo yaliyotolewa na TAKUKURU ya kujiepusha na vitendo vya Rushwa vinavyoweza kusababisha kuchukuliwa hatua za kisheria kwa Askari wa Usalama Barabarani (Trafiki), Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoani humo ACP. Justine Masejo amesema baada ya Mafunzo hayo yeyote atakayebainika kujihusisha na Rushwa hatakuwa salama
Mafunzo hayo ni baada ya Mwananchi kulalamikia kukithiri kwa vitendo vya Rushwa miongoni mwa Askari wa Usalama Barabarani katika Jiji la Arusha na kutoa wito kwa RPC kufuatilia na kushughulikia changamoto hiyo
Mwananchi huyo alidai kuwa baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani husimamisha Magari bila sababu za msingi kisha kuomba ‘kitu kidogo’ huku akiyataja maeneo ya Barabara ya Moshi Arusha, Barabara ya Monduli maeneo ya Shamsi, Barabara ya Njiro Maeneo ya Fire na Barabara ya Ngaramtoni kukithiri kwa changamoto hiyo
Madai ya Mdau haya hapa >>>> DOKEZO - RPC Arusha, tatua hii kero ya kuomba hela inayoshamiri kwa Trafiki