Kifo cha Norah; aliyejifanya mwanaume ili ajue maisha ya wanaume yakoje

mcshonde

Member
Jul 15, 2022
66
152
nor.jpg

Kifo cha Norah Vicent kiliibua hisia kwa jamii kutokana na namna utafiti alioufanya ulivyommaliza yeye mwenyewe. Norah alitaka kujua maisha ya mwanaume yakoje..ni changamoto zipi anapitia? Mwaka 2003, bila kubadili jinsia yake, akaamua ajifanye kuwa mwanaume; akaajiri mtu wa make up,mtaalamu wa sauti, pamoja na mwalimu wa mazoezi ya viungo.

Kwa miezi 18 akawa na jina jipya, Ned. Akajiunga timu ya mpira wa wanaume, akaanzisha mahusiano na wanawake, na kufanya kazi kwenye ofisi ya wanaume pekee. Lakini Norah, sasa Ned, hakuona raha yoyote na bila kujijua akaanza kupata msongo wa mawazo...depression. Kwenye kitabu chake "Self-Made Man" akakiri kuwa wanawake, pamoja na wanaharakati, huwa wanaamini wanawake ndio wanapitia magumu mengi katika jamii lakini ukweli ni kwamba wanaume wana machungu mengi katika maisha yao.
Wanaume wanateseka, Wana matatizo tofauti na ya wanawake, lakini bora sisi, wao wanahitaji zaidi upendo, kuonewa huruma" alisema Norah.

Zamani ukizaliwa mwanaume ilionekana ni bahati na nafasi ya upendeleo; lakini kaitka kizazi hiki kuwa mwanaume ni shida. Utafiti uliofanyika mwaka 2020, ulionyesha kuwa 70% ya watu wasio na makazi (homeless) ni wanaume. Pia hatari ya mwanaume kujiua ni mara 4 zaidi ya mwanamke. 90% ya ajali za sehemu ya kazi ni za wanaume

kwa aliyokutana nayo Norah, alipata matatizo ya akili yaliyotesa kwa zaidi ya miaka 17, na mwishowe julai 6, 2022 akaamua kujiua huko Switzeland. Kuwa mwanaume ni kazi.

nora.jpg
 
View attachment 2500007

View attachment 2500010
Hata huo utafiti wake ulionesha dhahiri ana matatizo ya akili. Hayakuanza mwaka jana.
 
bora huyu ametoa facts kwa kuingia field mwenyewe kujionea. hapo yeye kajiua na alikuwa na option ya kurudi kwenye uhalisia wake, sasa jiulize ni wanaume wangapi wanapia wakati aliopitia yeye? na mbaya zaidi hawana sehemu sahh pakujielezea hisia/matatizo yao zaidi ya kuvunga tu
 
Hii kitu niliwahi kumwambia wife kwamba wanaume tunapitia nyakati ngumu na mateso makali ispokua tu hatusemi, hatulii na dunia haituhurumii
Na katika hii safari ya kuwa mwanaume Kuna wengi hasa kizazi Cha Sasa wameshindwa na kuishia kuwa binadamu jinsia ya tatu(mashoga) na wengine wakakwepa majukumu na kuishia kujiua.

Kuwa mwanaume Ni zaidi ya ukomando.
 
Na wengi wanawake wanaobadili jinsia na kuwa wanaume, wengi wao hujutia na kurudi kuwa wanawake tena.
Mara chache wanaume waliojibadili jinsia kuwa wanawake, kutaka tena kuwa wanaume.

Ila huwa nasema, kama huo moto wa jehanamu basi utakuwa wa mafungu. Hawa ma Dr wabadili jinsia, wana moto wao wa pekee.
Haya mambo ya mtoto akizaliwa, achague jinsia yake yananivuruga kichwa sana.
 
Back
Top Bottom