Mwanaume ongea tu

Ntaganda boy

Member
Jan 16, 2016
90
59
Kauli ya Mwanaume Ongea Tu Si Sahihi

Kulingana na matukio mengi ya wanaume kujiondoa uhai na kufanya ukatili kwa wenza wao, watoto, familia na marafiki zao, watu wengi wamekua na muamko wa fikra za kuwahimiza wanaume kuongea na hasa wakitumia familia kama njia kuu ya kupokea hayo maongezi.

Familia na marafiki ndio njia ya kwanza kabisa ya kufanya nao mawasiliano na kauli ya wanaume ongeeni mnapokua na matatizo ni nzuri ila sio suruhisho sahihi la mtu kutatua au kuondoa tatizo hasa likiwa la Afya ya Akili.

Wanaume wengi si watu wa kuongea wala kutafuta msaada wa mawazo mbadala na zaidi inakua mbaya anapokua mwanaume mkimya (Introvert) au mwenye tabia za ubinafsi zaidi.

Kwa nini kauli ya wanaume ongeeni si sahihi, ongeeni haitoshi ila wanapaswa kuhimizwa kujenga tabia ya kutafuta huduma stahiki za kuwasaidia tofauti na kuongea na ndugu tu na kusema utakua sawa.

Ndugu/Marafiki katika kuongea nao wanakua na uhukumu ndani yake (Judgemental mindset or biasness) na hii inampelekea hata yeye kutokua na utayali wa kukusikiliza kwa umakini lakini pia ndugu na marafiki wanakusikia ili wakupatie jibu la kitu unachoongea na sio kukusikiliza. Hapa ni vyema kujua tofauti ya kusikia na kusikiliza.

Ndugu na marafiki kwa dunia ya sasa wako busy kutafutia familia zao na kulingana na hali ya maisha kuwa ngumu inakua changamoto wao kukupatia sikio na ndio maana tuna mawazo ya ndugu wako busy nitaongea nao lini na simu hawapokei au wanakata.

Dunia ya sasa imekua na watu wenye taaluma tofauti tofauti kwaajili ya binadamu, ni wakati sasa kwa wanaume kuwatumia wana taaluma hao. Hapa ninazumgumzia wataalamu wa Afya ya Akili, Wanasaikolojia na Wanasihi. Hawa wanaondoa ile kauli ya ndugu wako busy na hawasililizi.

Wanaume na jamii nzima inapaswa itengeneze utamaduni wa kutafuta huduma kutoka kwa wataalamu na hii itaondoa ile kadumba kuwa ndugu wanageuza matatizo yetu kama sehemu ya kupiga stori na watu wengine. Usalama wa taarifa na matatizo yako upo kwa wataaluma na sio kila sehemu.

Kauli ya Wanaume Ongeeni, igeuke na kuwa Wanaume Tafuteni Huduma za Kinasihi na Kusaikolojia.

Bosco Bosco
Mwanasaikolojia Nasihi (Counselling Psychologist).
 
Hakika...
unnamed-1.jpg
unnamed.jpg


Cc: Mahondaw
 
Una hoja;

1. Mwanaume ukiongelea hisia zako utabezwa tu, hamna mtu atakuvumilia

2. Tukisema tuhimize wanaume wawe wanaongea, waoneshe udhaifu, walie... utofauti kati ya me na ke utapungua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom