Nguvu kubwa ya mwanaume inayofifia kila kukicha

Richard mtao

JF-Expert Member
May 13, 2018
209
236
Habari za Muda huu waungwana,

(Uzi wa kufikirika sina maana ya kutukana ama kudharirisha jinsi yoyote ni kwajili ya kuchangamsha bongo zetu basi).

Hvi mnafahamu kwamba mwanaume alipewa nguvu kubwa sana juu ya utawala wa viumbe vyote hapa duniani?

Jibu ni ndio.
NB: Watalamu wa maswala ya kidini watanisaidie katika ilo.

Lakini kwa bahati mbaya sana kadri siku zinavyozidi kwenda nguvu hii inapungua kila siku na mbaya zaidi hata wanaume wenyewe tunajichukulia kawaida sana kiasi kwamba mpaka inafikia hatua mwanaume hajui afanye nini yaani anabaki kuwa mtu wa ndio mzee au kufanya matendo yatakayo mfedhehesha na kushusha thamani yake kama mwanaume.

Zifuatazo ni tabia zinazochangia mwanaume/wanaume wengi kupoteza nguvu zao za asili pasipo wao kujua:-

  • Kukubali kujibizana na mwanamke! Aibu
  • Mwanaume aliekamilika kiafya na kiakili Kufanya vitendo /matendo ya kike. Mfano kuvaaa nguo za kike, kusuka, kutoboa masikio, kupaka make up na kadharika
  • Kuwa mmbea mmbea, kutokuwa na misimamo, Unaishi kwa shemeji yako na kutwa nzima anashindia vijiweni bila sababu za msingi.
  • Mwanaume kufanya ushoga, ubakaji, kulawiti.
  • Kukubali kujinyenyekeza mbele za watu kwasababu ya shida.
  • Kuiacha familia au wapendwa wake kwasababu ya malaya, mchepuko. N.k

Hizi ni baadhi ya tabia ambazo zinachangia pakubwa kuiondoa nguvu yako ya asili/uwezo wa asili.

Mwanaume uliumbwa kuwa mtawala, uliumbwa ukiwa umepewa uwezo mkubwa wa kuwaza nje ya box pale unapopatwa na hali ngumu au tatizo fulani, uliumbwa ukiwa na nguvu kubwa ya kuwasiliana na Mungu, uliumbwa kama jeshi la akiba la Mungu dhidi ya muovu ibilisi shetani na ndo maana shetani mpaka leo anatuogopa dhambi zote anazofanya mwanaume shetani humtumia mwanamke, uliumbwa kama kielelezo cha uwepo na mwendelezo wa dunia, nakadharika.

Lakini kwasababu ya upumbavu mwingi tunaoufanya baraka tulizopewa na kufunuliwa uwezo mkubwa wa kufanya mambo zinapotea na hatuna kitu tunafanya kurudisha nguvu zetu za asili.

Shetani alivyoona tumelala yaani hatutumii nguvu zetu za asili ipasavyo akaja na mikakati yake ya kutufanya tulale kabisa ili iwe rahisi kwake.
1. Akashawishi baadhi ya watu wenye nguvu duniani kuanzisha propaganda ya haki sawa baina ya jinsi ya Me na Ke.
Na ndio maana mpaka leo mashirika na mataifa yenye nguvu yanaendelea kuipush ajenda hii ili kukamilisha mpango wa kutufanya wanaume tulale usingizi fofo.

2. Zikaundwa stori mbalimbali zenye utata juu ya mwanadamu wa kwanza kuumbwa na kuwekwa kwenye bustani ya edeni( wakadai binadamu wa kwanza alikuwa mwanamke alieitwa lilith, lengo la haya yote ni kuwapa wanawake ujasiri kwamba wana uwezo mkubwa kuliko mwanaume.

Ipo mikakati mingi sana ya ibilisi lakini kwa leo naomba niishie hapa ili kufupisha uzi huu wenye lengo la kuwasaidia wanaume kurudishaa nguvu zao za asili.


Itaendelea sehemu ya 2.
 
Back
Top Bottom