Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Huo Ni Wehu Mtupu Kuwa Mallya Ni Jasusi,na Nimesikitika Kusikia Hivyo Kutoka Kwa Mmoja Wa Wanasiasa Aarufu Nchini,
Lakini Hii Inatuonyesha Ni Watu Gani Tulio Nao Ktk Siasa Za Nchi Hii Mie Nafikiri Prof Lipumba Ameona Uvivu Kufikiria Akaamua Kutoka Na Conclusion Yake Hiyo
 
Tangu jana ulipokiri kuwa wewe ni mtu wa CCM sitashangaa unapotetea hapa na kuandika kuwa ni sahihi kwa CCM kuwa na waraka huo na kuusambaza siku moja kabla ya kifo chake, tena unasambazwa kwa makatibu wa CCM nchi nzima.

Pili,hao CCM wanapaswa kujitoa humo walimo kwani kama leo wanamuona Wangwe kama hero wao ,basi kuna mambo mengi huwa wanafanya kuliko haya machache ambayo yanaanza kuonekana ,wanafiki mwisho wao ni kupata aibu na kuumbuka , ona sasa MACCM YANAVYOUMBUKA ,KUMBE NDIVYO YALIVYOOOOOOO....

MK,

Hivi kweli nyie mungelikuwa na waraka wa Kolimba unaosema CCM imekosa dira, mungeshindwa kuusambaza kwa wafuasi wenu?

Mambo mengine mimi naona ni obvious mno. Vyama vya siasa vipo kutafuta weaknesses kwenye wapinzani wao na kuzitumia.

Kama CCM wangeshindwa kuitumia nafasi hiyo ningewaona kweli watu wao wa propaganda wamelala.

Usitegemee hata siku moja Makamba akiri kuusambaza huo waraka.

Haya mambo ndiyo ambayo tuliongea wengine wakati ule tunajadili mgogoro wa CHADEMA na Wangwe. Kwamba hivi vita vya panzi furaha ya Kunguru. Tena mlianza kuendesha mambo kwenye magazeti, kumchafua Wangwe kwenye magazeti na forums, mlitegemea yeye akae kimya? Hapa CHADEMA mnavuna mlichopanda na kama mnajua siasa ilitakiwa mlitegemee hili, kama hamkulitegemea nitakuwa na wasiwasi mkubwa na uwezo wenu wa kupambana na CCM.
 
MK,

Hivi kweli nyie mungelikuwa na waraka wa Kolimba unaosema CCM imekosa dira, mungeshindwa kuusambaza kwa wafuasi wenu?

Mambo mengine mimi naona ni obvious mno. Vyama vya siasa vipo kutafuta weaknesses kwenye wapinzani wao na kuzitumia.

Kama CCM wangeshindwa kuitumia nafasi hiyo ningewaona kweli watu wao wa propaganda wamelala.

Usitegemee hata siku moja Makamba akiri kuusambaza huo waraka.

Haya mambo ndiyo ambayo tuliongea wengine wakati ule tunajadili mgogoro wa CHADEMA na Wangwe. Kwamba hivi vita vya panzi furaha ya Kunguru. Tena mlianza kuendesha mambo kwenye magazeti, kumchafua Wangwe kwenye magazeti na forums, mlitegemea yeye akae kimya? Hapa CHADEMA mnavuna mlichopanda na kama mnajua siasa ilitakiwa mlitegemee hili, kama hamkulitegemea nitakuwa na wasiwasi mkubwa na uwezo wenu wa kupambana na CCM.

Tunachohoji hapa ni waraka kusambazwa masaa 24 kabla ya kifo cha Marehemu, ni kwanini walitumia fax za ofisi tena yya Katibu mkuu wa CHAMA ?

Mengine nimekuelewa .
 
Mkuu Kitila,

Maneno mazito sana, ninaomba kuongeza kidogo kwamba ufike wakati Chadema, waamke na kuona kwa macho mawili kwamba as long as huu mjadala wa Wangwe unaendelea kati yao na CCM, ni advantage kubwa sana kwa CCM, kwa sababu kwa mara ya kwanza Chadema nayo inaanza kuwekewa mashaka na wananchi, kitu ambacho ni kawaida kwa CCM,

It is about time sasa, Chadema wakatafuta a new subject ya kuiondoa hii ya Wangwe, kwa sababu the more inasimama na wao kujiingiza kurushiana maneno ya propaganda na CCM, ni the more wana-sink kwenye Public Opinion na ni kwa sababu moja nzito sana ya kumsimamisha Makamu Wa Mwenyekiti wao, in only seven months toka achaguliwe, na hasa kitendo cha baadhi ya viongozi wao wa juu kujiingiza kwenye vita vya propaganda na marehemu, alipokuwa hai, wananchi hupenda the under dog hiyo ni sheria ya siasa na michezo dunia nzima, ingawa hufuraia sana the top dog akishinda, lakini hufurahi zaidi the underdog akishinda, hapa the under dog Wangwe ameshia kutangulia kwenye haki, sasa the top dog viongozi wa juu wa Chadema wamebaki, Wangwe hakuwa na ishus na CCM, bali Chadema, sasa wanashindaje the Public Opinion kwa kurushiana maneno na CCM, kwa ajili ya marehemu the under dog waliyekuwa wamemsimamisha uanachama?

Only kama Chadema wataweza kutoa ushaidi mzito kuwa hawahusiki na kifo cha Wangwe, na kutoa ushahidi mzito wa wanaohusika na hicho kifo kama wapo, otherwise ni kufukuza hewa kushindana na CCM on this ishu, na believe me kuwa kuna wajinga flani ndani ya CCM ambao are having a lot of fun na hii topic,

Chadema, please change the subject now kabla haijawa too late!

Ushauri wa bure na wa binafsi, kwa sababu can you imagine our national politics bila ya Chadema?

Mkuu FMES,
Nimekuwa kwa wakati wote ni msomaji wa majibizano katika thread hii ikiwa mengine mengi ni ambayo hayana msingi wowote zaidi ya propaganda ya vyama vya siasa na blah blah kama za vijiweni.

Lakini kubwa ninachangia pale ambapo ninaona kuna mwelekeo wa kupiga hatua rather than kuzunguka au kuganda hapohapo.

Siasa ni uwanja mpana sana na huenda hauna mipaka kila mtu hucheza kadri ya vile anavyoona inafaa. Mara ajali ilipotokea ndani ya CHADEMA nadhani ilizuka hofu ya kuhusishwa na kifo hiki na kitendo cha kutoa taarifa mara kwa mara kiliwafanya wachezaji katika uwanja wa siasa kuchukua udhaifu huo mara moja ambapo CHADEMA ikajitwisha mzigo ambao si wa lazima wa kuongelea kila jambo lililohusiana na ajali ile hali iliyosababisha kila mwenye lake alielekeze kwa CHADEMA. Kama utaangalia kwa makini hii hofu ya kuhusishwa na kifo cha Mh. Wangwe baadhi ya viongozi bado haijawatoka na ndiyo maana wanashindwa jinsi gani ya kubadilisha mwelekeo. Kwa mfano wanatumia muda mwingi ku-counter attack propaganda zinazorushwa hewani, hebu angalia haya yafuatayo...
- Mbowe ahusishwa na msiba Wangwe

(Jibu la CHADEMA lingekuwa ni fupi tu Mbowe hahusiki, period anayetaka kumuhusisha zaidi atoe ushahidi usio na shaka)
- Mbowe atimuliwa kwenye msiba Tarime
(Jibu la CHADEMA lingekuwa hakutimuliwa isipokuwa vurugu zilikuwepo na si kusema kuwa alishangiliwa)
- Kwanini TBC ilionesha mazishi live
( Jibu la CHADEMA lingekuwa, hiyo ni kazi ya vyombo vya habari kama CHADEMA haiwezi kuingilia mambo ya ndani ya TBC)
- Waraka wa Wangwe wasambazwa na CCM[/COLOR]( Sioni haja ya kuendelea kuingia kwenye mitego, waacheni CCM wasambaze kadri wanavyotaka kwani huo ni waraka wao na ndiyo kazi ya siasa)

Nimeorodhesha machache, kwa wale wenye jazba watadhani labda ninataka kuwafundisha CHADEMA nini cha kusema au kujibu, la hasha haya ni mawazo yangu binafsi kwani kila siku zinavyozidi kwenda CHADEMA watajikuta wanahangaikia issue mpya moja baada ya nyingine, guess what? watakuwa wanasambaratishwa bila ya wao kujijua wakidhani wako sawa lakini sivyo.[/SIZE]
 
Tunachohoji hapa ni waraka kusambazwa masaa 24 kabla ya kifo cha Marehemu, ni kwanini walitumia fax za ofisi tena yya Katibu mkuu wa CHAMA ?

Mengine nimekuelewa .

Nafikiri hilo la masaa 24 kabla ni coincidental. Wangelijua anakufa wasingeusambaza wakati huo. Wangeutoa baada ya kifo ili uwe na impact kubwa. Labda na wenyewe wawe wageni kwenye spins. Angelikuwa Kingunge, timing ni kitu muhimu mno kwenye spins lakini kwa Makamba, sidhani ana uwezo mkubwa.

Nafikiri hapa tunajaribu kutengeneza storm in a tea cup.
 
Jamani hebu tuwekee hapa ka-Cv ka huyu Mallya tumjue vizuri yaelekea dogo ana viji-mambo fulani...

kwa kweli mtusaidie kwasababu umri wa huyu jamaa na matukio yake hayaendani mfano habari moja ilieleza kua mwaka 1994 akiwa chuo nairoba alijifunza gari ila akaacha kwa kua aliumia, kwa mtu mwenye miaka 27 leo hii 2008 mwaka 1994 alikua na miaka........14 je chuo gani? au ni darasa la ngapi huko nai?
mara mwaka gani alikua libya? alienda na wabunge na sheikh kama nani wa ccm?n au interested observer wa mambo ya Afrika?
jamani msitutanie nyie..... sisi ni watu wazima loooo
 
kwa kweli mtusaidie kwasababu umri wa huyu jamaa na matukio yake hayaendani mfano habari moja ilieleza kua mwaka 1994 akiwa chuo nairoba alijifunza gari ila akaacha kwa kua aliumia, kwa mtu mwenye miaka 27 leo hii 2008 mwaka 1994 alikua na miaka........14 je chuo gani? au ni darasa la ngapi huko nai?
mara mwaka gani alikua libya? alienda na wabunge na sheikh kama nani wa ccm?n au interested observer wa mambo ya Afrika?
jamani msitutanie nyie..... sisi ni watu wazima loooo

Kwa mujibu wa baba yake,

malya kazaliwa mwaka 1983.Huu ni mtaji wa kisiasa kwa ajili ya kampeni zao,ila wasipoangalia..wote wanaweza kukosa
 
Jamani badala ya kutafuta majibu muhimu kwa ajiri ya kupata ukweli tunabisha kwenye vitu ambavyo vitatulazimu kufikia wrong conclution, kabla ya kujump kwenye conclution please tupate majibu ya msingi kutoka kwa mallya then we can conlude based on the fact.

tunapiga kelele yule kijana anaweza kufia ndani tukakosa majibu ya msingi, please people mwenye access naye na amuuliize maswali yasiyokuwa na majibu halafu hatuwekee hapa.
 
Hadi sasa naamini kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufuatilia nyendo zote za Marehemu Chacha Wangwe kwa muda wa wiki mbili ama hata mwezi kabla ya "ajali" ilipomkuta. Ni muhimu kujua kila aleye ongea naye na kama kuna link na hizi siasa zinazoendelea ni muhimu kuwabana kujua waliyokuwa wakiongelea, nini mantiki ya makutano yao na nini kilijiri baadaye

Vilevile ni muhimu kuangalia account za Mallya na hata za Marehemu. Kwa Mallya ni kudetect fedha zisizoeleweka lakini pia kujua mahusiano yao ya Marehemu yalianza lini na yalikuwa katika hali gani. Maana nasikia kuwa Marehemu alikuwa na tabia ya kuamini sana watu na kuingia nao ubia wa kibiashara. Kwake yeye zaidi ilikuwa kuwawezesha wahangaikaji wenzake.

Vilevile kama CCM walikuwa wameshamshawishi kuingia huko kitu ambacho sikiamini kwa kujua mazingira ya kisiasa ya TARIME na chuki yao dhidi ya CCM na Serikali...lakini pia CCM kuna utamaduni wa kuwapatia wanaoasi vyama vyao TAKRIMA ambayo mara nyingi huwa kuanzia millioni 20 kuenda mbele. Mzee Wassira, Msabaha aliyekuwa CUF, Kaborou ni ushahidi mzuri katika hili.

Kwa wanaohoji ni kuhusu RASTA za WAngwe hapo zamani ni kweli alikuwa nazo na alikuwa ana tabia ya kutembea na picha akiwa na RASTA na kule Tarime ni maarufu kama CHACHA Rasta. Marehemu alilazimika kuondoa Rasta kwa ushauri ama shinikizo la MWALIMU NYERERE alipokuwa anataka ushauri wake ili yeye ajiunge na harakati za siasa.....Hata hivyo marehemu alibaki kuwa muumini mkubwa wa falsafa za Kirasta wakati wote na hiyo ndiyo naweza kusema kuwa ilikuwa msingi mkubwa wa fikira na matendo yake daima.....

Kuhusu Prof Wangwe ni kweli yeye ni mwanachama wa CCM na pia aliwahi kugombea ubunge wa Afrika Mashariki kupitia CCM ambapo yeye pamoja na mama KABAKA walikuwa wanamlaumu Marehemu CHACHA kwa kitendo chake cha kuungana na wenzake wa CUF na kina Zitto kususia uchaguzi ule kama sababu ya yeye Prof Wangwe kushindwa. Hivi sasa ni mjumbe wa NEC ya CCM na pia kuna madai kuwa kuingia kwake kwenye siasa kulichangiwa na siasa za Marehemu Wangwe ambaye ni mdogo wake kwa UBINAMU.

Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa Prof Wangwe na Marehemu CHACHA RASTA Hawakuwa karibu kama watu wanavyodai hapa lakini Prof Wangwe naweza kusema ndio mtu pekee aliyeweza kutumia vizuri busara zake kupunguza jazba na propaganda zilizokuwa zinaitafuna familia kidogokidogo.

Kuna madai kuwa msimamo wa sasa ni kujitahidi kuendana na muono wa baadhi ya wanafamilia ambao walifikia kumshambulia kuwa amepewa hongo kusema kuwa kifo cha CHACHA RASTA kilikuwa cha ajali ya kawaida. Wapo wafanyao hivyo kwa maslahi ya kisiasa na ya binafsi na wapo wafanyayo hivyo kwa mashaka halisi kabisa yaliyojengeka katika fikira zao ambao mimi pia naungana nao mkono.

Tanzanianjema

Kwa jinsi ninavyowafahamu RASTA...Sidhani kama wana nia mbaya na mwafrika.
We'll see when we get some facts...Lakini maelezo yako ni mazuri na ninashukuru.
Sasa hii issue kweli kazi.
 
Naona mzee umeenda kwenye archive!...

Kwa kusema hivyo sijamdharau Zitto, yeye kaleta opinion yake.. I brought up mine, except mine was short and clear thats it!...

Ndugu ukubali tu wewe ni mdini! hata hapo uliposema;



Sijui point unataka kuleta hapa!

Kutaja CCM na CUF tu! haina maana nimeidharau CHADEMA!....

Na hiyo sio mada ya hapa!

Hamis GOGO ambaye alikuwa cuf...Na baadae kuwa recruited maybe na RA...Huyu ni nani?
Wewe unafikiri mimi sina na sijawahi kuwa na marafiki wasilam?
Mimi sikufichi...Too much of anything is harmfull...Hata dawa zenye kukutibu uki overdose zinakuuwa...Ukuiwa na msimamo mkali...Uwe mkristo ama muislam...NI TATIZO KWENYE JAMII.
Mungu ataikombowa Tanzania kwasababu kuna generation itakayaosimamia UMOJA WAKE.
 
Asante Mushi sikuiona bana duh!! nimechemsha

Don't worry comrade...NOT A BIG DEAL AT ALL...We all do mistakes...Lakini hii yako ni honest mistake kwasababu nia yako ni kuhabarisha...Na Mods watafanya kazi hiyo ama wewe mwenewe unaweza kwenda kuitowa ukipenda.
Hata hivyo umeonyesha BUSARA.
 
nimezungumza na anton komu, mkurugenzi wa chadema, ambaye amehojiwa na polisi jana kuhusu kijana mallya, anchoeleza ni kuwa mallya ni mbangaizaji, misheni town. yeye alikuwa anshinda pale chadema kama mbangazizaji, na akabahatika kwenda kwenye hiyo tripu ya libaya. namna alivyoweza kuwa karibu na wangwe ni kama viongozi wengine wanavyojipatia wapambe. kwa kadiri mnavyomkuza huyu kijana ni kadiri muda ambao ni dhahabu unapotea bure.

huyu pia ni mkazi wa huko manushi kibosho, ni mbangaizaji kwenye ile dizaini ya kutumwa kabandike matangazo ya mkutano, maara kakodishe kipaza sauti n.k
anton komu 0713 615603

wabangaizaji, misheni town ndo hao hao wazuri kwa ujasusi....na hiyo habari ya kubahatika kwenda libya.... mi siiiti ni bahati .... kunawatu wanaijua, wameindaa na lazma ilikuwa na shuguli nyingine ya ziada....
if scotland yard wakidig on this boy watatoka na mengi sana lkn si jeshi la police la tanzania
 
Don't worry comrade...NOT A BIG DEAL AT ALL...We all do mistakes...Lakini hii yako ni honest mistake kwasababu nia yako ni kuhabarisha...Na Mods watafanya kazi hiyo ama wewe mwenewe unaweza kwenda kuitowa ukipenda.
Hata hivyo umeonyesha BUSARA.

Jmushi asante nshatoa mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom