Kifo cha Kapt. Komba, funzo kwa wanasiasa

Kifo cha Kapt. Komba, funzo kwa wanasiasa

Mzaha mzaha hutumbua usaha na dalili ya mvua ni mawingu,chondechonde watawala msifanye maskhara hali ni mbaya."TAFAKARINI MCHUKUE HATUA"
 
hata mwass wa tuzo za nobel, cku moja akiwa kwenye ndege akielekea kwenye msiba wa mdogo wake, akisoma gazeti alikuta habari iliyo ikisema yule aliyetengeneza bunduku na yy amekufa, kupitia hiyo abar alijifunza kuwa cku akifa watu watasema aliyekuwa akitengeneza bunduki za kuulia watu na yy amekufa ndo akamua kuanzisha tuzo ya nobel, mpaka leo anakumbukwa kwa tuzo hiyo. komba tutamkumbuka kwa upuz wake alio kuwa akionge bungen
 
mtu mwenye machungu akiona kuwa wale ambao anahisi wamesababisha machugu wamefariki ufurahi maana anajua mateso yanapungua
 
Mimi niko bado najiuliza, Captain Komba aliwezaje kutunga nyimbo za kuombeleza kifo cha baba wa taifa ndani ya muda mfupi tu tangu kifo kitokee, au alikuwa ni mnajimu aliyetabiri kuwa Baba wa Taifa atakufa na akaanza kutunga nyimbo na kuifundisha band yake?? Looh, kafa kabla hajatupatia majibu ya swali la kitendawili hiki!!! Vile vile alisema atakwenda msituni, hakufafanua kama angeenda msituni kujificha ili katiba asiyoipenda kama itapitishwa, au kwenda msituni kuongoza mapambano ya kijeshi kutetea katiba anayoipenda. Looh, kafa kabla hajatupatia majibu ya swali la kitendawili hiki kingine!!!
Huenda alikuwa na kipaji kikubwa cha utunzi ha haraka haraka, au alikuwa ameshafanya maandalizi ya tungo bila kumlenga mtu hivyo ilipotokea ni mwalimu basi akazibadilisha kumwelekezea mwalimu.
 
Ma jibu ya watu kutoitaka katiba ilopendekezwa ndy hayo ndy kero za wananchi mwenyez mungu anaanza kuzipokea bado wengine na walompiga mzee warioba wajiandae kudadadeki, wamefufa vipenz vya mung sembuse yy nan tumbo tu ela za wizi kudadadek.
 
Bado Sita na hili zee katuaribia kabisa katiba yetu kudadadeki kaa mkao wa kwenda kuitikia nyimbo za komba motoni.
 
Amekwenda msituni huyo kujipanga akiludi huko mzee wtu akimbie kudadadeki kweli mwenyez mungu anapokea dua za wananchi masikin na km mungejua dua tunayoimba tena kabla hamjazika huko cijui ngoja tuendelee kutia ubani, ewee mwenyez mungu wee wasiludi huko wale wote wa katiba wale pokea dua hii sir god.
 
Mimi niko bado najiuliza, Captain Komba aliwezaje kutunga nyimbo za kuombeleza kifo cha baba wa taifa ndani ya muda mfupi tu tangu kifo kitokee, au alikuwa ni mnajimu aliyetabiri kuwa Baba wa Taifa atakufa na akaanza kutunga nyimbo na kuifundisha band yake?? Looh, kafa kabla hajatupatia majibu ya swali la kitendawili hiki!!! Vile vile alisema atakwenda msituni, hakufafanua kama angeenda msituni kujificha ili katiba asiyoipenda kama itapitishwa, au kwenda msituni kuongoza mapambano ya kijeshi kutetea katiba anayoipenda. Looh, kafa kabla hajatupatia majibu ya swali la kitendawili hiki kingine!!!

Mama mdogo hapo kwenye suala la kwenda msituni hata mimi kaniachia utata sana. yaani aende msituni akafanye nini? anyway nimechelewa
 
Nimebahatika kupata taarifa za misiba za watu wengi tu nikiwa harusini...

Wakati Wa kifo cha Nyerere watu hawakuona raha ya harusi lakini nikushuhudie Jana watu pamoja na kusikia Komba kafa Harusi iliendelea na masham sham Kama kawaida.....

Halafu wachawi na majahili tu ndo huheshimu Sana vifo kwa unafiki wao lkn kwa wengine ni jambo la kawaida kwani huwapata binadamu wote....

Komba angemjua Mungu unaemsema asingemnenea Warioba ufedhuli ule....

Nanyi mnemjua Mungu msingeacha wajawazito wateseke kulala chini na wagonjwa kufa kwa kukosa dawa huku mapesa mkipeleka kwenye katiba isiyo na Tija...

Siku hizi lusungo unajipanga kunena vitu vya maana, hongera mkuu
 
Ujumbe ni mzuri sana wenye kuwakumbusha WanaSiasa na Sisi wote (Binadamu).
Pia wasimsahau Mungu aliyeumba Mbingu na Nchi na Vyote viijazavyo Dunia.

Wanabodi salamu kwenu,

Natanguliza kutoa pole kwa familia,ndugu, jamaa na Marafiki wa familia ya kapt Komba bila kuwasahau wananchi wa Mbinga ambao marehemu alishawakimbia muda mrefu anaishi dar Kwenye kiyoyozi muda wote leo wanapata mshtuko mkubwa kuambiwa mbunge wao amewatoka hakika ni majonzi makubwa sana.

Hapa nawalenga wanasiasa wetu, ni vema kila mwanasiasa akajitathmini, msisahau siasa ni Karama tulizogawiwa na M/Mungu kama zilivyo karama zingine.

Ndugu zangu Mwenyzi Mungu ametupa utashi wa kupambanua mambo tofauti na wanyama.....
Lakini pia mkumbuke kila mtu hapa duniani atakumbukwa tu Mara baada ya kututoka but style za kukumbukwa huwa zinatofautiana, either utakumbukwa kwa mabaya yako ulipokuwa hai au kwa mazuri yako.

Ndugu wanasiasa wengi wenu mmekuwa mkijisahau sana kwamba pia kuna maisha out of politics but ukweli ni kwamba wew kufa hakukuondolei ukweli wa yale uliyokuw ukiyafanya kipindi cha uhai wako.

Hapa ninachokilenga ni kwamba kifo cha Kapt Komba kimeibua hisia tofauti ndani ya jamii, wengi wamekuwa wakiona ni sahihi huyu Mzee kupunzika, wengine wakisema kauli zake zilikuwa za kuudhi na kutaka kuchafua nchi..... Lakini kundi la pili likidai watu kumsema marehemu siyo sahihi inajenga image mbaya kwa jamii....

Ukweli ni kwamba kifo isitumike kama mwavuli wa kuficha mabaya ya mtu, hii ni dalili ya uwoga watu kuogopa kuhukumiwa baadae huko ahera kwa kusema mabaya ya marehemu... Ukweli hauwezi kubadilishwa kwani hakuna binadamu asiyejua kuwa kuna kifo na maandalizi ya maisha ya mtu ni yake mwenyewe tuache uwoga usiokuwa na maana, tutakukumbuka na kuyasema kwa yale uliyokuwa ukiyafanya enzi za uhai wako, mazuri yako tutayasifia na mabaya pia tutayasema na kuyalaani.

Ushauri wangu.

Wanasiasa wetu mmekuwa mkijisahau sana as if vifo haviwahusu nyie, please kila mmoja wenu ayatafakari maisha yake ya kisiasa na kujiuliza Je utakumbukwa kwa lipi??? Tumieni ndimi zenu vyema huku mkitambua kuwa kauli zenu zina impact kubwa sana kwa jamii.

KUMBUKENI KILA MMOJA HAPA DUNIANI ATAKUMBUKWA KWA STYLE YAKE.

THANKS
Ni hayo tu.
 
mbona kuna wanasiasa kibao tu wakifa raia watakua wanashangilia.....
yani wale wanaoona kua kufurahia kifo cha huyu mzee sio sawa wajiandae kisaikolojia...maana kwa hali hii nchi ilipofikia ....kuna watu wakifa...hadi party zinafanyika...
 
Makonda, Nape na Lusinde fanyeni toba ya kweli. Kutukana wazee kuwa wanasubiri kufa tuu ni jambo baya sana maana mnaingilia kazi ya Muumba. Wote tutaondoka,lakini sio vema uondoke huku ukikejeliwa kwa yale uliyoyasema ukiwa hai. Unaachia familia yako majonzi zaidi.
 
siku zote marehem hasemwi wala hatajwi kwa mabaya, wahenga walikuwa na hekima kubwa sana, sababu merehmu keshafumba mdomo hana uwezo wa kujitetea kwa kwa kusemwa vibaya na kushutumiwa ingawa inahisiwa anasikia na kuona kila kitu.

Hivyo kutosema mabaya ya marehem haimaanishi watu hawajui mabaya na maovu yake ua wamesaahu la asha, bali wanataja mazuri yake tu ili mwenyewe marehemu asikie na aone akitajwa kwa mazuri.

Mwisho kumbuka kila mtu atakufa na hata ww na mimi tutakufa tu, hatujui mwisho wetu kama utakuwa ni mwema au utakuwa ni mwisho mmbaya, vyovyote iwavyo hautajisikia viuri kama tukitajwa kwa mabaya na ili hali tukishindwa kujitetea.
 
Kama wewe unamsifu Osama ni wewe......

Shetani ni shetani tu awe mzima ama mfu.
 
Back
Top Bottom