Mantissa
JF-Expert Member
- Jul 24, 2010
- 876
- 168
Uko sahihi Mkuu! Safari ya kifo huanza mara tu mbegu ya kiume iunganapo na ya kike. So, suala la kifo sio suala la mjadala bali suala la muda tu; kwa wale wana-hisabati, death = f(time) where time is very unpredictable - hapa hakuna cha uzee, ujana, wala utoto - at any time (age) death is a sure event.
Kwa maana hiyo, mwanadamu (mwanasiasa) mwenye busara huchunga sana kauli zake akijua muda asiotarijia, kifo huja kama mwivi ajapo. Tuisjitungie sheria (Katiba) na kanuni nyingine za kulinda ka-kikundi ketu kana kwamba tutaishi milele humu duniani. Badala yake tufanye mambo kwa maslahi mapana ya taifa, kwa maslahi ya maskini walio wengi, kwa maslahi ya wananchi.
Hebu tuandae mabango yetu vizuri ili tuyabebapo wengine waone sifa njema kwenye mabango hayo ili ijapo siku ile tusiyoitajia wananchi watukumbuke kwa sifa nje badala ya kushukuru na kusema "afadhali". Hivi utapata faida gani kwa kuacha mabilioni ya ufisadi kwenye mabenki huku ukiondoka na sanda na jeneza tu wananchi wakishukuru kwa kuondoka kwako? Marehemu Komba alijaaliwa kipaji lakini kwa nyakati tofauti alitumia kipaji chake vibaya - hakuwa na sababu ya kuwatukana na kuwadharau wapinzani kiasi kile! Kwamba kama sio CCM wewe sio mtanzania!? CCM na wanasiasa wajifunzi siasa za staha na kuvumiliana
Kwamba Mzee Warioba na tume yake ni wazee wanaokaribia kufa hizo ni kauli za akina Komba, Ridhiwani, Paul Makonda, Kibajaji, na Nape. Kwa hakika Mungu akiamua mtatangulia wote mtawaacha wazee hawa; bahati nzuri wao wanalo bango lililo jema; ninyi mtapotea kama mbwa asiyekumbukwa tena baada ya kifo chake.
Hiyo nyekundu nimeikubali mtabe. It's real. Probability yake huwa ni kitu kizima siyo sehemu tena kama sikosei. safi sana kamanda.
Mimi huwa siwaelewi watu wanaosema eti mtu akishaaga dunia, basi hajadiliwi, mapokeo mabaya kabisa. Mtu sema upuuzi wake tu hata anapokuwa anazikwa. Alikuwa mwizi, sema sifa hizo, sio mbaya maana alikoandikiwa mtu baada ya kufa, hata ukimpamba vipi, hubadili mawazo ya aliye hai milele. Sasa sisi tunadanganyana tu. Unafiki tuache kwa kweli, suala la kufa kila mtu analijua kuwa lzima afe siku moja tu. But unakufaje? ndo swali