... mkumbuke kila mtu hapa duniani atakumbukwa tu Mara baada ya kututoka but style za kukumbukwa huwa zinatofautiana, either utakumbukwa kwa mabaya yako ulipokuwa hai au kwa mazuri yako.
Khaa!! Hivi nyie mna akili kweli? Kumsema vibaya marehemu kuna wasaidia nini?? Yule hayupo nasi tena wala hasikii tena. Hapa mnachokifanya hakuna zaidi ya kuwatia majonzi ndugu na wapendwa wake tu ambao ndiyo haohao wanaoipigia kura ccm, cuf, cdm etc Mnachoonesha ni utoto katika siasa. Eti wanasiasa wengine wajifunze, wajifunze nin? Nani asiyejua kifo? Ndiyo maana mtu akifa husemwa kwa mazuri hata kama ni ya uongo ili kuifariji familia na hata ukisema mabaya yake atajitetea vipi naye kisha kufa?
Jamani hata akili kidogo ya kuliona hili hamna? Ndiyo shida ya kuwa na wanasiasa njaa kali wengi kuliko wazalishaji
GJHariohay, I am in the same view. Kilinichonishtua ni Jamiiforums kuamua kufunga threads zote zilizokuwa zinamjadili John Komba kwa "mabaya" aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
Kuna msemo maarufu hapa JF unaosema "Ficha Upumbavu wako; Usifiche Hekima yako!" Lakini walichofanya JF ni kuficha "upumbavu" wake, bila kutuonyesha "hekima" zake.
Invisible na wenzako mmetunyima uhuru wa kuongelea mazuri na mabaya ya John Komba.
Kuna wanasiasa wengine ambao ni worse than Komba kwa kuharibu hii nchi kwa faida zao binafsi nao muda wao wa kukaa hapa duniani ukifika, mtafunga zile threads zao zote zilizokuwa zinajadili mabaya yao wakati wa uhai wake?
Ni kama vile mnaweka bad precedent na kama hamtazifunga thread za wengine pia, itabidi mtoe justification kutofanya hivyo. I thought here is "where we dare to talk openly".
Kuongelea mabaya ya Komba siyo kumnaga marehemu, bali ni kuwapa watu uhuru wa kujadili pande zote mbili za kuhusu yeye. Mfano, alipofariki Margaret Thatcher niliweka thread siku ya mazishi yake:
Margaret Thatcher funeral: a "fitting tribute?" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Watu walijadili openly including mabaya yake kama kumwita Mandela gaidi. Lakini thread haikufungwa. Sasa hii "rule" ya kutojadili mabaya ya marehemu ina-apply kwa marehemu wa Kitanzania tuu?
Labda mmeamua kufunga hizo threads kwa muda, I hope mtazifungua baadae ili watu wawe na uhuru wa kuendelea kuchangia siyo tuu kwa mazuri ya Komba, bali pia kwa mabaya yake if after all we all agree that we are not perfect.
Pia itawapa nafasi watawala wengine wajue ni jinsi gani they have lost touch na wananchi wanaodai kuwawakilisha kiasi kwamba hata ikifika ile siku yao itakuwa business as usual kwa wawakilishwa.
Vinginevyo tutakuwa tunatengeneza mazoea kwa baadhi ya wanasiasa kudhani kuwa mabaya waliyoifanyia hii nchi na watu wake yatasahaulika na kamwe hayatajadiliwa tena pale tuu watakapoiaga dunia.
Na mie siyo perfect, though siyo mwanasiasa, still I may have done what in the views of others is good and wrong na siku nitakapoiaga dunia ruksa kujadili mabaya niliyofanya na siyo mazuri tuu.