Kifo cha Kapt. Komba, funzo kwa wanasiasa

Kifo cha Kapt. Komba, funzo kwa wanasiasa

Marehemu huenziwa.Husifiwa na kukumbukwa kwa mema yake. Isiwe haramu kusema na alipoteleza pia.Aliposema au kufanya tofauti ya matarajio ya wengi au wote. Maneno ya tahadhari au ya mafunzo wakati wa msiba si kwa ajili ya marehemu.Yeye hausiki tena.Kusema na kutenda.

Alichoposti mtandaoni J.J.Mnyika ni kukumbusha tu kauli ya Hayati Kapteni John Damian Komba aliyoitoa katika Bunge la Katiba. Kauli ya kumsimanga na kumtabiria kifo Waziri Mkuu Mstaafu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Jaji Joseph Sinde Warioba. Hayati Komba alimwita Warioba 'mzee anayekaribia kufa'. Haikuwa kauli rafiki.Ilikera na kukwaza kwelikweli.

Kukumbusha kauli hiyo wakati wa msiba wa mtoa-kauli si matusi wala kejeli.Ni mafunzo kwa sisi tuliobakia.Tunaaswa kusema na kutenda kwa mipaka hata pale tunapoghadhibika.Tujitahidi sana kuzuia kughafilika. Kifo ni fumbo. Kujua haiwezekani. Tunaaswa kuwa makini na kauli na matendo yetu hasa kuhusu masuala ya kifo.

Tukimtetea Hayati Komba kwa kauli yake,Mzee Warioba atajisikiaje? Misiba itufunze zaidi ya kuhuzunika na kuomboleza kwetu. R.I.P. Captain (Rtd.) John Damian Komba!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Tuondolee umasabiri hapa
 
nadhani kati ya watanzania wote, kauli chafu kwa marehemu imetoka kwa mnyika mnatetea ujinga ili iweje? Mnyika anajua yeye atalazwa wapi? anakumbuka alivyomtukana rais?

Hakumtukana raisi zaidi ya kumwambia kuwa udhaifu wake ndio uliopelekea taifa kuwa hapa.
Komba alitamka dhahiri kuwa Warioba anatutengenezea katiba ambayo anajua wazi atakuwa amekufa.Sasa Warioba anapumua na kafa yeye.Muuguzi kafa mgonjwa kapona
 
Kati ya Watanzania zaidi ya mil. 45 Mnyika tu ndiye ameona muda huu ambao Komba haongei tena ndiyo wa kumkosoa? Alikuwa wapi wakati angali hai? Huyu Mnyika atakuwa na matatizo ya akili, kwanini kila kauli chafu itoke kwake tu?

Mnyika kafanya vyema sana kutukumbusha waTz mil. 45 mawazo ya Komba muda huu. Sawa Komba katangulia lakini mawazo yake aliyoyatoa in public hayafi; yataishi vizazi na vizazi. Yatakumbukwa daima.
 
Tuondolee umasabiri hapa
Mkuu, humu jf kuna watu wa ajabu sana, eti wanashangilia mtu kufa? Mambo ya ajabu sana, sijawahi kuona kwa kweli. Malipo ni hapahapa duniani, hivi kesho tukiamka na kuambiwa MNYIKA kafa tutasema amelogwa au Mungu kasikia fedheha zake kwa kiumbe ambacho hakina uhai tena.
 
  • Thanks
Reactions: PPM
Sijawahi kusikia kuambiwa unakaribia kufa ni tusi, au haujui maana ya tusi?

Kwa hiyo kwako ni sawa sawa kwa kuwa kwako sio tusi? Na kama hayo maneno hayana matatizo mnachong'aka humu kwamba marehemu aachwe ni nini? Kuna njia nyingi za kumkumbuka marehemu na njia mojawapo ni kupitia kauli na mawzo yake alipokuwa hai. Kweli magamba mna matatizo sio bure.
 
Nimeambiwa tatizo la mnyika ni elimu yake ya kuunga unga, nikachanganya na zangu nikagundua mnyika ana uwezo mdogo wa kufikiri.

AAAH KWELI USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA KIZA, KWA ELIMU YAKE TU ALIYO NAYO mnyika FUATILIA PERFORMANCE YAKE ILIKUWAJE??, REAL NATHUBUTU KUKUITA WEWE UNA AKILI ZA PANZi
 
Mnyika kafanya vyema sana kutukumbusha waTz mil. 45 mawazo ya Komba muda huu. Sawa Komba katangulia lakini mawazo yake aliyoyatoa in public hayafi; yataishi vizazi na vizazi. Yatakumbukwa daima.
Mnazidi kumzidishia Mnyika Dhambi. Muombeeni aondokane na roho ya mavi hiyo siku moja naye atalala kama Komba kwenye jeneza.
 
nadhani kati ya watanzania wote, kauli chafu kwa marehemu imetoka kwa mnyika mnatetea ujinga ili iweje? Mnyika anajua yeye atalazwa wapi? anakumbuka alivyomtukana rais?

Mnyika ameongea lipi baya...kwani komba aliyekufa hakutamka hayo maneno? Rest in Hell Komba...Utakumbukwa kwa Uccm wako
 
AAAH KWELI USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA KIZA, KWA ELIMU YAKE TU ALIYO NAYO mnyika FUATILIA PERFORMANCE YAKE ILIKUWAJE??, REAL NATHUBUTU KUKUITA WEWE UNA AKILI ZA PANZi
Tatizo siyo performance, tatizo ni performance ya kiwango gani cha elimu? Hata kindergaten wanaperform wonders
 
Mnazidi kumzidishia Mnyika Dhambi. Muombeeni aondokane na roho ya mavi hiyo siku moja naye atalala kama Komba kwenye jeneza.

Kwani kutamka kwamba komba alisema kuwa mzee warioba anakaribia kufa amekosea nini?
 
Nadhani unafiki na ujinga unawatesa watu wengi saaana. Wanaomshambulia JJ Mnyika ni wajinga na wanafiki kwa sababu alichofanya JJ Mnyika ni qoutation ya alichokiongea hayati Komba. Kitu cha msingi hapa na kwetu sote as human being ukifa leo, this minute and second je wanaobaki nyuma yako watakukumbuka kwa lipi? Matendo yetu, utu wetu, Lugha zetu, na upendo kwa ujumla. Tujifunze kupitia haya matukio na kuhakikisha tunaweka records zetu sawa kabla ya mauti. RIP Capt Komba.
 
Mnyika ameongea lipi baya...kwani komba aliyekufa hakutamka hayo maneno? Rest in Hell Komba...Utakumbukwa kwa Uccm wako
Tatizo nabishana na watu ambao hawajui mlango wa Kanisa au msikiti uko wapi. Hii akili yakou astahili huruma ya Muumba ndugu yangu.
 
Msiba gani kumegeuka kuwa ni sehemu ya kupigia picha?
 
Mkuu, humu jf kuna watu wa ajabu sana, eti wanashangilia mtu kufa? Mambo ya ajabu sana, sijawahi kuona kwa kweli. Malipo ni hapahapa duniani, hivi kesho tukiamka na kuambiwa MNYIKA kafa tutasema amelogwa au Mungu kasikia fedheha zake kwa kiumbe ambacho hakina uhai tena.

Na wewe nawe...sasa kuna watu wengine ambao ni "Sheeedah" kwenye jamii yetu wakifa lazima tushangilie

Sasa mtu kama chenge akifa nani atachukia

Watu wengine ni bora wafe tu
 
Tatizo nabishana na watu ambao hawajui mlango wa Kanisa au msikiti uko wapi. Hii akili yakou astahili huruma ya Muumba ndugu yangu.

Kwani mlango wa kanisa au msikiti unaruhusu unafiki....kusema marehemu alikua mtu mwema na mtakatifu...wakati alikua lofa flani tu wa CCM
 
Mkuu TataMadiba,tafadhali weka kauli ya Mnyika na uoneshe 'uchafu' wa kauli hiyo

Mzee Tupatupa

Mzee Tupa Tupa, TATA MADIBA na akina SHONZA wana tatizwa na kauli ya Mnyika juu ya udhaifu wa Rais aliyoitoa Bungeni. Hicho ndicho kinachoprevail akilini mwao. Komba siyo wa kwanza kutolewa salamu za rambirambi za aina hiyo.Kaa nao hapo Lumumba waeleweshe mambo haya. Kuna mtu aliweka picha humu muda mfupi baada ya tangazo la Kofi cha Capt. Komba, akiwa anacheza mziki na mwanamke, na akaandika kuwa amekufa akiwa anachungulua Mahalia hapo, mbona jambo lile halikuonekana kashfa?
 
Nadhani unafiki na ujinga unawatesa watu wengi saaana. Wanaomshambulia JJ Mnyika ni wajinga na wanafiki kwa sababu alichofanya JJ Mnyika ni qoutation ya alichokiongea hayati Komba. Kitu cha msingi hapa na kwetu sote as human being ukifa leo, this minute and second je wanaobaki nyuma yako watakukumbuka kwa lipi? Matendo yetu, utu wetu, Lugha zetu, na upendo kwa ujumla. Tujifunze kupitia haya matukio na kuhakikisha tunaweka records zetu sawa kabla ya mauti. RIP Capt Komba.
Wajinga ni nyie mnaomtetea mtu aliye hai na anayedhihaki kiumbe ambacho kimetwaliwa na Muumba. Nyie na Mnyika mnahitaji kuombewa.
 
CHADEMA mmezidi kudhihaki maiti. ni juzi tu Lissu alikuwa anamtukana Nyerere. inawasaidia nini kwenye siasa hapa duniani?

Mkuu naona unatiririka kama fiati zakizamani vile sasa isiyo na breki vile.
 
Back
Top Bottom