Mnyika kutamka kwamba rais wetu ni dhaifu halikuwa tusi. Sema ni tusi gani Mnyika alimtukana rais? au wewe unaona rais wetu ni tough? Umemsikia akisema kitu chochote kukemea mauaji ya Albino tangu kila mtanzania anavyohuzunika na kulia? Wakati wa matatizo mie nakumbuka baba wa nyumba ndio anapanda pipa kwenda kusalimia rafiki zake ulaya,marekani na uarabuni. Huo ndio udhaifu. Anawatuma wasaidizi wake kazi kuifanya akijua kuwa ni bomu, likilipuka baadaye anawaacha njia panda kama kina Mramba na wenzie. Tegeta ESCROW si umeona anavyoongea wakati anasemwa kunufaika Bilioni 10 katika familia yake lakini anakuwa kama hasikii vile, anatetea kwamba ni hela yao sio ya serikali. Anafanya hivyo kwa sababu anajua watanzania wanajua lakini anataka wazibe midomo. Kama baba anafaidi pesa chafu, watoto wafanyeje? NSKANSKA limekuwa bomu tangu yeye akiwa waziri wa madini na umeme ndani yake, moja kwa moja anahusika nalo lakini watu hawamsemi kwa heshima ya kiti chake tu. Subiri akitoka utasikia mengi. Bora Mnyika alisema wakati mhusika anayo nafasi ya kujiosha. Unataka angesema kama anavyosemwa Komba hivi sasa na hana nafasi ya kujifunza uhalisia wa mambo na kunawa uso? Tusiwe wanafiki watanzania. Ukimpenda mtu mwambie ukweli ili anawieishe historia yake, ni unafiki wa kutisha kumwambia mfalme wako kavaa vizuri sana wakati unaona kabisa yuko uchi, basi tu kusudi akupatie ukuu wa wilaya au mkoa Fulani. Akitoka kwenye kiti nawe unang,olewa kwa uzandiki wako.