Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kuna haja ya kanisa katoliki kuangalia upya sheria za kanisa. Huyu mtu ni muuaji na jambazi halafu kanisa halikuwahi kumkemea hadharani kama maagizo ya biblia yanavyosema, alikaa labda viti vya mbele huku akishangiliwa leo hii anaingia nyumba ya mungu akiwa amekufa huku akiwa na damu za watu kibao je hii ni sawa mbele ya mwenzi mungu???

Mkapa nae kanisa lazima liangalie upya kama anahitajika kanisani yeye na chenge ni aibu tupu.
Chenge kasoma seminari ya katoliki halafu yale ni matunda ya kanisa ni aibu tupu. wanafundisha nini watoto wetu kule , biblia imeweka wazi kemea karipia. je ni lini Pengo alimkaripia mkapa ama chenge ama Balali na wengineo kwa majina baada ya kudhibitika wizi wao, hujuma zao, utawala wao mbovu na maamuzi yao ya kinyama. kweli hawa watu wanaiwakilisha jamii ya kikatoliki kweli ama kanisa linang'ang'ania michango yao ya kifisadi.

wakatoliki aamkeni kanisa limevamiwa, limekuwa kichaka cha kuficha majangili pigeni kelele. Salini novena hawa majangili na wahubiri wanaowakumbatia waondoke ama adhabu ya Mungu itakuwa juu yenu.

Pengo sema wazi mkapa umewakosea watanzania masikini hufai kwenye taifa la Mungu mpaka utubu hadharani na kuwarudishia masikini ulivyowaibia, ndivyo yesu alivyo sema na hayo ndio mafundisho ya yesu. vilele Chenge, balali na wengine wanachanga fedha haramu kila siku.........kila anayekufa kwa kukosa dawa, ajali za barabarani, elimu duni , maradhi ya kuambukiza damu yao juu ya mafisadi na wanaokumbatia mafisadi.
 
HIvi watu wamepata wapi hili wazo kuwa Balali atachomwa moto? Ndiyo mambo ya kusoma taarifa juu juu.

Nafikiri mkuu kuna watu wanautata katika kuelewa taarifa inapotolewa. Mimi binafsi nafikiri nimekupata vizuri sana baada ya kusema kwamba HAIJAJULIKANA kwa uhakika kama mwili wa marehemu utazikwa ardhini kama ilivyo desturi ya kiafrika au utateketezwa kwa moto kwani makaburi hayo yanatoa huduma hiyo pia.. JAMANI TUACHE KUKURUPUKA MAANA NENO KAMA NENO LIKIPINDISHWA KIMAANA LINAWEZA KULETA ATHARI KATIKA JAMII.

Source: Michuzi

Naamini JF ndio mahala pekee pakupata Uchambuzi na Habari za Kwanza zenye Hoja jenzi kwa manufaa ya wanajf wenye na Taifa kwa ujumla wake.
 
Jamaa hakufika kwao miaka 30? Kwi kwi kwi!!!!! Mtu kama huyu hana uzalendo na alikotoka, je anaweza kuwa na uzalendo na nchi?

Ballali�s home village mourns ex-BoT chief

By Bernard James and Mkinga Mkinga

Residents of the home village of the former Bank of Tanzania (BoT) governor, Dr Daudi Ballali, are mourning his death despite having not seen for more than 30 years.

In another development, Dr Ballali�s wife, Anna Muganda, said he was leaving his husband�s death �in the hands of God�.

�There is nothing I can say. We�re leaving this matter in God�s hands,� he said by telephone from Washington DC when asked to state what had killed Dr Ballali.

Elsewhere, scores of mourners congregated in the quiet and sleepy Liganga Village in Mufindi District, Iringa Region, following Dr Ballali�s death in the United States last Friday.

They said they would go ahead and perform all burial rituals in accordance with Hehe tradition even if Dr Ballali would not be buried there.

Reports said about 20 relatives were present at the home of the former governor�s parents and were joined by neighbours and friends who came to offer their condolences. They were meeting at a fairly decent village house in which Dr Ballali reportedly grew up.

Dr Ballali�s relatives, like most other Tanzanians, learnt of the death of Liganga�s foremost scholar through the media.

They said Dr Ballali, who will be buried thousands of kilometres away, probably in Washington DC, last set foot in the village over 30 years ago.

The relatives maintained that although they had not seen Dr Ballali since his childhood, they would perform all rituals in accordance with Hehe tradition because he was �our child and our brother�.

�No hymns are being sung here. Villagers are just passing by to comfort the bereaved,� one of the relatives said.

Dr Ballali died last Friday in the United States and his death was made a top secret by close family members even after rumors about his death had widely circulated.

The former BoT boss is expected to be buried today in Washington DC according to his wishes.

Meanwhile, a spokesperson of the task force appointed to probe BoT�s EPA scandal, in which Sh133 billion was lost, Mr Omega Ngole, said the team would not be issuing any statement on Dr Ballali at the moment.

�We are not ready to issue names of EPA suspects interrogated by the task force committee, including the late governor Daudi Ballali, it�s too early to comment,� Mr Ngole said in response to a query on whether investigators had talked to Dr Ballali before he died.

Mr Ngole added that for the time being the task force would pursue its activities as planned and present investigation results to the President.

Dr Ballali was in January this year sacked by President Jakaya Kikwete after he was accused of having a key role in the embezzlement of Sh133billion from the BoT�s External Arrears (EPA) Account.

He resigned several weeks before he was sacked and was allowed to leave the country for medical treatment in the US. He had since disappeared until the new about his death broke out on Tuesday.

He was at the center of the ongoing EPA investigations. There are reports suggesting that Balali may have been poisoned to avoid any word from his mouth that could have unearthed more about EPA scandal.

He last appeared at a news conference where he rejected call for resignation. Few weeks later he was reported to have left for US for medical treatment.

He was reported to have undergone stomach operation after he suffered severe abdominal pains few weeks before he flew to US.
 
Mchanga mwingine machoni, eti sasa wameonywa? Madaktari wa majuu wanaweza kugundua Polonium 210 kweli watashindwa kugundua sumu ya Dodoma? Ukitumia logic kwenye hii story unaweza kupata kichaa maana logics zote zinakataa.

Nduguze Ballali waonywa

na Mwandishi Wetu

DADA wawili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), waliokuwa wamepanga kuitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki ijayo, wameonywa kuhusu uamuzi wao huo.

Onyo hilo limetolewa kwao kwa njia ya simu na watu mbalimbali waliowasiliana nao wakiwa Washington, Marekani, uliko msiba wa Ballali ambaye anatarajiwa kuzikwa leo.

Aidha, onyo hilo pia lilitolewa jana kwa njia ya simu na watu waliojitambulisha kuwa ni wasomaji wa Tanzania Daima, ambao walieleza wasiwasi wao wa wazi kuhusu uamuzi wa ndugu hao wa Ballali ambao taarifa za wao kuja kuzungumza na waandishi wa habari ziliandikwa jana na gazeti hili pekee.

"Mhariri, mimi ni msomaji mzuri wa gazeti lako. Ninapenda kukuomba uwafikishie salamu zangu hao dada wawili wa marehemu Ballali. Wasije wakajikuta wakifikwa na matatizo, kwa sababu ya uamuzi wao wa kuitisha mkutano na waandishi wa habari kama mlivyoandika," alisema mwanamke mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.

Alipoulizwa ni kwa nini alikuwa akifikiria kuwa ni jambo la hatari kwa kina dada hao kuzungumza na Watanzania kuhusu kile kilichomfika ndugu yao Ballali, msomaji huyo alisema hali ya hewa kisiasa imechafuka, hivyo kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa wao kudhurika, hata kabla hawajafanikiwa kuzungumza kile walichokipanga.

Watu wengine wawili waliozungumza na Tanzania Daima nao walieleza wasiwasi kama huo, na mmoja wao akafikia hatua ya kuwataka wanawake hao ambao hivi sasa wako Washington wakiomboleza msiba wa kaka yao, wafikishe kila wanalofahamu kuhusu mazingira ya kifo hicho cha Ballali kupitia mtandao wa intaneti.

"Mhariri naomba uwataarifu dada zake Ballali kutothubutu kuzungumza na waandishi wa habari hapa Dar es Salaam. Kama wana lolote la kusema kuhusu mazingira ya kifo cha ndugu yao, hawana budi kufanya hivyo kwa njia ya mtandao ambao katika siku za karibuni, imekuwa njia muafaka zaidi na salama kuitumia kufikisha ujumbe," alisema muonyaji mmoja.

Tanzania Daima ilipowasiliana kwa simu na ndugu mmoja wa Ballali aliyeko Washington katika msiba wa gavana huyo wa zamani wa BoT na kumweleza kuhusu wasiwasi huo, naye alikiri kupokea simu kadhaa kutoka kwa watu mbalimbali waliosoma gazeti hili hapa nchini au kwa njia ya mtandao wa intaneti.

"Hata sisi hapa tumepokea simu nyingi zikitutahadharisha kuhusu hatua hiyo ya kuzungumza na waandishi wa habari. Kwa hiyo suala hilo bado linajadiliwa na uamuzi wa kuzungumza au kutozungumza na waandishi wa habari utaangaliwa na ikibidi unaweza ukabadilishwa," alisema.

Kuhusu uamuzi wa Ballali kuzikwa Washington, ndugu huyo wa Ballali alisema hata wao walifikia hatua ya kukubaliana na uamuzi wa yeye mwenyewe kutaka akifa azikwe huko kutokana na kuchafuka kwa jina lake, kutokana na kuhusishwa kwake na tuhuma mbalimbali za ufisadi.

Mwanafamilia huyo juzi aliieleza Tanzania Daima kwamba, Ballali alifikia uamuzi huo wa kuzikwa Marekani, kutokana na kufadhaishwa na namna jina lake lilivyokuwa likihusishwa na tuhuma nzito za ufisadi.

"Yeye mwenyewe ndiye aliyeamua azikwe huku Washington. Siku zote amekuwa akitueleza namna alivyokuwa akifadhaishwa sana kutokana na kuchafuliwa kwa jina lake, hata baada ya kuitumikia nchi yake kwa juhudi kubwa, moyo mkunjufu na kwa uadilifu wa hali ya juu.

"Alitueleza hapa kwamba hajapata kuiibia nchi yake hata senti moja. Hapo ndipo aliposema akifa angetaka azikwe huku huku Washington na si nyumbani, ambako alihusishwa na kila aina ya tuhuma," alisema mwanafamilia huyo juzi, kauli ambayo jana aliendelea kuisisitiza.

Akizungumza jana, alisema alimuona Ballali kwa mara ya mwisho akiwa hai, Alhamisi ya wiki iliyopita, ikiwa ni siku moja tu kabla ya kufikwa na mauti.

"Nilipomuona Alhamisi iliyopita nilimkuta akiwa amewekewa ‘drip' nyumbani kwake, ikiwa ni kama siku moja au mbili tangu alipotolewa hospitalini, baada ya madaktari kumweleza kuwa walikuwa hawana lolote la kufanya," alisema ndugu huyo.

Aidha, jamaa huyo wa Ballali alikanusha taarifa kwamba, Ballali alikufa baada ya mashine za kumsaidia kuishi kuzimwa kutokana na uamuzi uliofikiwa kwa pamoja kati ya wanafamilia na madaktari.

"Hapana, hakuwa katika mashine wakati akifariki. Alifia nyumbani kwake Washington na si Boston kama ilivyotangazwa na BoT," alisema.

Mbali ya hayo, ndugu huyo wa Ballali aliieleza Tanzania Daima kwamba, mke wa Ballali, Anna Muganda, alikuwa ameomba msiba wa mumewe ufanywe kwa faragha, ukiwahusisha ndugu, marafiki na jamaa zao wa karibu.

Alisema kutokana na hali hiyo, shughuli hizo za msiba zilikuwa zikifanyika pasipo kuwapo kwa shughuli zozote za wazi kama vile kuchukua picha za video au kupiga picha nyingine za kawaida.

Aliieleza Tanzania Daima kwamba, kwa muda wote huo wa msiba, Anna alikuwa mtulivu na alikuwa amezima simu zake zote na hakuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya kumzika mumewe leo hii.

Alisema pia kwamba, mama mzazi wa Ballali ambaye hivi sasa anaishi Boko, jijini Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 94 alikuwa ameshindwa kusafiri kutokana na uzee.

Pamoja na hilo, aliieleza Tanzania Daima kwamba, taarifa walizokuwa nazo ni kwamba Katibu wa Gavana wa Benki Kuu, jana alikuwa amekwenda Boko kuhani, ikiwa ni pamoja na kutoa ubani kwa ajili ya msiba huo.

Habari kutoka Boston na Washington ambazo Tanzania Daima imeshapata kuziandika, zinaeleza kwamba, kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikisema kwamba, Ballali alikuwa akisumbuliwa na aina moja ya saratani kwa muda mrefu.

Hata hivyo wakati kukiwa na taarifa hizo, baadhi ya ndugu, marafiki na jamaa zake wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kwamba, Ballali alilishwa aina fulani ya sumu isiyojulikana, siku kadhaa kabla hajakimbizwa Marekani kwa matibabu.

Taarifa hizi za kulishwa sumu zimekuwa zikienea kwa haraka katika maeneo tofauti na baadhi ya watu tayari wametaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina kujua ni kitu gani hasa kilikuwa kimempata.
 
Tahariri-Tanzania Daima leo
LILE sakata la wizi wa mabilioni ya fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti ya madeni ya nje (EPA), limeingia katika sura mpya na ya kukanganya kutokana na kifo cha aliyekuwa gavana wa benki hiyo, Daudi Ballali.

Mkanganyiko huu unatokana na jambo moja kuu, kwamba mtu huyu aliyekuwa mkuu wa taasisi inayosimamia taasisi zote za fedha nchini amekufa bila kueleza umma alichokijua juu ya sakata lote la uchotaji wa kiasi cha sh bilioni 133 zilizoripotiwa kuchotwa ndani ya benki hiyo na makampuni 22 ya kitapeli.

Kifo cha Ballali, iwe kilipangwa au ni mipango ya Mungu, kimeiacha serikali katika mtihani mgumu kwa sababu nyingi, kubwa kuliko yote kwamba ilishindwa kupata kauli yake kuhusu sakata la wizi wa mabilioni ya fedha tangu kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya Ernst & Young ilipowasilisha taarifa yake na kusababisha Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa Ballali.

Bila shaka rais alichukua hatua ya kutengua uteuzi wake kwa sababu aliamini kwamba kiongozi huyo alishindwa kuwajibika vilivyo hadi kuifikisha BoT katika aibu ya kutisha ya upotevu wa fedha za umma kiasi cha sh bilioni 133. Kwa maana hiyo ama kwa kusema au kutokusema, Ballali alikuwa ni mtu wa kuisaidia timu ya rais ya kuchunguza wizi wa fedha hizo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Tunajua kwamba baada ya kifo cha Ballali wapo watu wanaoshangilia kwamba sasa wamesalimika kutokana na kutoweka kabisa kwa uwezekano wa taarifa za kuhusika kwao na sakala la wizi huu.

Ingawa watu hawa watashangilia kwamba wamesalimika kutokana na mtu mwenye siri zao kutangulia mbele ya haki, sisi tunasema kwamba serikali ina maswali mengi ya kujibu kuhusu suala lote la Ballali, kuanzia kuandika barua yake ya kujiuzulu, kufukuzwa kazi, kuugua, kukimbilia Marekani hadi kifo chake.

Kwa mwenendo serikali ilionyesha kufunika hali ya mambo katika sakata lote hili tangu awali. Serikali ilikataa kusema alikokuwa amekwenda kutibiwa mtumishi wake, lakini kibaya zaidi hata baada ya kutengua uteuzi wake haikusema iliwasiliana naye kwa njia gani ili kumpa taarifa. Kwa maneno mafupi, serikali ilijivua wajibu wa sakata la EPA kupitia kwa Ballali kiujanja.

Tunasema serikali inajitoa kiujanja kwenye suala hilo kwa sababu katika akili ya kawaida, ni lazima ilijua kwamba itafika wakati Ballali angekuwa mtuhumiwa namba moja wa suala la EPA, na kwa maana hiyo ilikuwa na kila sababu ya kujipanga kujua aliko mtuhumiwa huyo mtarajiwa na kwamba suala la afya yake lingekuwa la umuhimu wa kipekee kwao.

Ndiyo maana katika hali hii, umma unahitaji kujua kutoka serikalini chanzo cha kifo cha Ballali; maradhi aliyougua, waliokuwa wanamuuguza ni akina nani, kwani katika hali ya kawaida hiwezekani watu wasadikishwe kwamba eti kiongozi huyo alikuwa huru kwenda kokote kufanya lolote bila serikali kufuatilia nyendo zake.

Kuna uvumi kwamba kuna watu wana mkono katika kifo cha Ballali. Kwa mwenendo mzima wa kadhia hii tangu mwanzo, serikali ilionyesha kukosa umakini. Ni kukosa umakini tu kunaweza kueleza mtu kufukuzwa kazi wakati alikwisha kuandika barua ya kujiuzulu, lakini pia ni kukosa umakini tu serikali iliyokuwa ikimlipia gharama za matibabu Marekani, iseme kwamba haijui hospitali aliyokuwa akitibiwa. Lakini pia ni kukosa umakini tu kwa serikali nzima kuthubutu kutamka kwamba, eti ilikuwa haina shida naye wakati ikihaha usiku na mchana kusaka watu waliokwapua fedha za EPA.

Katika sura hii, serikali inaweza kujivua lawama za kifo cha Ballali kwa kukubali kuundwa kwa tume huru ya kimataifa ambayo itachunguza na kuweka wazi chanzo cha ugonjwa na kifo chake.
 
Haya sasa hii ndio serikali yetu wajibu sasa tuhuma hizi zinazowakabili badala ya kuingia mitini...Pinda upo??Luhanjo vp hapo?Mwema je?
 
Hata mtu ambaye anaweza kureason kidogo lazima atatilia mashaka kifo hiki kwani kinaonekana kama sio cha kawaida na trend ya matukio yanayofuatia nayo inaendelea kuchanganya kwani tulitegemea watu wakiona maiti watasema kweli amekua lakini sasa wanazidi kulikoroga, waje watwambie watanzania tunataka kujua yaliyotokea kutoka kwa serikali na inategemea kuendeleaje na uchunguzi wa EPA.
 
Nduguze Ballali waonywa

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

DADA wawili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), waliokuwa wamepanga kuitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki ijayo, wameonywa kuhusu uamuzi wao huo.

Onyo hilo limetolewa kwao kwa njia ya simu na watu mbalimbali waliowasiliana nao wakiwa Washington, Marekani, uliko msiba wa Ballali ambaye anatarajiwa kuzikwa leo.

Aidha, onyo hilo pia lilitolewa jana kwa njia ya simu na watu waliojitambulisha kuwa ni wasomaji wa Tanzania Daima, ambao walieleza wasiwasi wao wa wazi kuhusu uamuzi wa ndugu hao wa Ballali ambao taarifa za wao kuja kuzungumza na waandishi wa habari ziliandikwa jana na gazeti hili pekee.

“Mhariri, mimi ni msomaji mzuri wa gazeti lako. Ninapenda kukuomba uwafikishie salamu zangu hao dada wawili wa marehemu Ballali. Wasije wakajikuta wakifikwa na matatizo, kwa sababu ya uamuzi wao wa kuitisha mkutano na waandishi wa habari kama mlivyoandika,” alisema mwanamke mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.

Alipoulizwa ni kwa nini alikuwa akifikiria kuwa ni jambo la hatari kwa kina dada hao kuzungumza na Watanzania kuhusu kile kilichomfika ndugu yao Ballali, msomaji huyo alisema hali ya hewa kisiasa imechafuka, hivyo kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa wao kudhurika, hata kabla hawajafanikiwa kuzungumza kile walichokipanga.

Watu wengine wawili waliozungumza na Tanzania Daima nao walieleza wasiwasi kama huo, na mmoja wao akafikia hatua ya kuwataka wanawake hao ambao hivi sasa wako Washington wakiomboleza msiba wa kaka yao, wafikishe kila wanalofahamu kuhusu mazingira ya kifo hicho cha Ballali kupitia mtandao wa intaneti.

“Mhariri naomba uwataarifu dada zake Ballali kutothubutu kuzungumza na waandishi wa habari hapa Dar es Salaam. Kama wana lolote la kusema kuhusu mazingira ya kifo cha ndugu yao, hawana budi kufanya hivyo kwa njia ya mtandao ambao katika siku za karibuni, imekuwa njia muafaka zaidi na salama kuitumia kufikisha ujumbe,” alisema muonyaji mmoja.

Tanzania Daima ilipowasiliana kwa simu na ndugu mmoja wa Ballali aliyeko Washington katika msiba wa gavana huyo wa zamani wa BoT na kumweleza kuhusu wasiwasi huo, naye alikiri kupokea simu kadhaa kutoka kwa watu mbalimbali waliosoma gazeti hili hapa nchini au kwa njia ya mtandao wa intaneti.

“Hata sisi hapa tumepokea simu nyingi zikitutahadharisha kuhusu hatua hiyo ya kuzungumza na waandishi wa habari. Kwa hiyo suala hilo bado linajadiliwa na uamuzi wa kuzungumza au kutozungumza na waandishi wa habari utaangaliwa na ikibidi unaweza ukabadilishwa,” alisema.

Kuhusu uamuzi wa Ballali kuzikwa Washington, ndugu huyo wa Ballali alisema hata wao walifikia hatua ya kukubaliana na uamuzi wa yeye mwenyewe kutaka akifa azikwe huko kutokana na kuchafuka kwa jina lake, kutokana na kuhusishwa kwake na tuhuma mbalimbali za ufisadi.

Mwanafamilia huyo juzi aliieleza Tanzania Daima kwamba, Ballali alifikia uamuzi huo wa kuzikwa Marekani, kutokana na kufadhaishwa na namna jina lake lilivyokuwa likihusishwa na tuhuma nzito za ufisadi.

“Yeye mwenyewe ndiye aliyeamua azikwe huku Washington. Siku zote amekuwa akitueleza namna alivyokuwa akifadhaishwa sana kutokana na kuchafuliwa kwa jina lake, hata baada ya kuitumikia nchi yake kwa juhudi kubwa, moyo mkunjufu na kwa uadilifu wa hali ya juu.

“Alitueleza hapa kwamba hajapata kuiibia nchi yake hata senti moja. Hapo ndipo aliposema akifa angetaka azikwe huku huku Washington na si nyumbani, ambako alihusishwa na kila aina ya tuhuma,” alisema mwanafamilia huyo juzi, kauli ambayo jana aliendelea kuisisitiza.

Akizungumza jana, alisema alimuona Ballali kwa mara ya mwisho akiwa hai, Alhamisi ya wiki iliyopita, ikiwa ni siku moja tu kabla ya kufikwa na mauti.

“Nilipomuona Alhamisi iliyopita nilimkuta akiwa amewekewa ‘drip’ nyumbani kwake, ikiwa ni kama siku moja au mbili tangu alipotolewa hospitalini, baada ya madaktari kumweleza kuwa walikuwa hawana lolote la kufanya,” alisema ndugu huyo.

Aidha, jamaa huyo wa Ballali alikanusha taarifa kwamba, Ballali alikufa baada ya mashine za kumsaidia kuishi kuzimwa kutokana na uamuzi uliofikiwa kwa pamoja kati ya wanafamilia na madaktari.

“Hapana, hakuwa katika mashine wakati akifariki. Alifia nyumbani kwake Washington na si Boston kama ilivyotangazwa na BoT,” alisema.

Mbali ya hayo, ndugu huyo wa Ballali aliieleza Tanzania Daima kwamba, mke wa Ballali, Anna Muganda, alikuwa ameomba msiba wa mumewe ufanywe kwa faragha, ukiwahusisha ndugu, marafiki na jamaa zao wa karibu.

Alisema kutokana na hali hiyo, shughuli hizo za msiba zilikuwa zikifanyika pasipo kuwapo kwa shughuli zozote za wazi kama vile kuchukua picha za video au kupiga picha nyingine za kawaida.

Aliieleza Tanzania Daima kwamba, kwa muda wote huo wa msiba, Anna alikuwa mtulivu na alikuwa amezima simu zake zote na hakuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya kumzika mumewe leo hii.

Alisema pia kwamba, mama mzazi wa Ballali ambaye hivi sasa anaishi Boko, jijini Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 94 alikuwa ameshindwa kusafiri kutokana na uzee.

Pamoja na hilo, aliieleza Tanzania Daima kwamba, taarifa walizokuwa nazo ni kwamba Katibu wa Gavana wa Benki Kuu, jana alikuwa amekwenda Boko kuhani, ikiwa ni pamoja na kutoa ubani kwa ajili ya msiba huo.

Habari kutoka Boston na Washington ambazo Tanzania Daima imeshapata kuziandika, zinaeleza kwamba, kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikisema kwamba, Ballali alikuwa akisumbuliwa na aina moja ya saratani kwa muda mrefu.

Hata hivyo wakati kukiwa na taarifa hizo, baadhi ya ndugu, marafiki na jamaa zake wamekuwa wakieleza wasiwasi wao kwamba, Ballali alilishwa aina fulani ya sumu isiyojulikana, siku kadhaa kabla hajakimbizwa Marekani kwa matibabu.

Taarifa hizi za kulishwa sumu zimekuwa zikienea kwa haraka katika maeneo tofauti na baadhi ya watu tayari wametaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina kujua ni kitu gani hasa kilikuwa kimempata.

Tumeona viongozi mbalimbali wanaenda kuhudhuria na kuto rambirambi kwenye msiba wa Ditto ambaye alikuwa ni muuaji na case yake ikiwa mahakamani.

Inakuwaje watu kama JK, baraza lake, akina Mkapa, Mkono na wengine hakuna hata mmoja aliyeenda hata Boko kutoa salaam za rambirambi?

Jamani nisaidieni, hivi ni mimi tu naanza kupata ukichaa kwenye hili jambo au watu wengi wana michanga machoni kama mimi?

Kuna kitu kikubwa sana kinafichwa, kinafichwa na familia ya Ballali na kinafichwa pia na serikali, je ni kitu gani hicho?

Itabidi kutunga kitabu cha kuanguka kwa Ballali.
 
kwi kwi kwi,

inabidi uoshe macho ndugu yangu kabla ya kufungua. Au nunua miwani myeusi na mikubwa ya kufunika macho. Sasa hivi michanga inarushwa kwa kasi ya maili 500 kwa saa na sidhani kama unaweza kuhimili bila kinga.

Hii ni kali na haijawahi kutokea kokote kule... wewe hadi mkapa amesita kwenda kumuona fisadi mwenzake unadhani mchezo?!!
 
Hawa ndugu nao wameona vyombo vya habari ndo mahara pekee pa kuanika hayo mambo yao si wayaanike apa JF dunia nzima watajua yote
 
let us be frank. hakuna bomu la kulipuliwa hapa. everything that we need to know we already know! serikali inawajua vizuri tu mafisadi wa EPA. inasita kuwakamata...and we also know why! kwa hiyo hawa dada zake balali wao watulie , waomboleze kifo cha kaka yao.
 
Ballali Alikuwa USA akaogopa kutoboa siri, hawa dada waje TZ kuja kutoboa siri? Hiki ni kiini macho kingine.

Labda hawa dada ni mashujaa kama Mwafrika wa Kike. Hata Mwafrika wa Kike alipoenda TZ, alishuka airport kimya kimya.

Wacha tuendelee kuwasubiri. Baadaye tutaambiwa wamezuiwa airport. Conspiracy theories zitaendelea tu.

wewe mtanzania wewe...

Mbona nilivaa bonge la tisheti ina labels kubwa sana za mwafrika wa kike zenye rangi ya njano na blue (if you know what i mean) ili kuwatisha wale vilaza wa immigration, TISS, na TRA pale airport.

nilipata mapokezi ya VIP.... hii nembo kubwa sana.... next time ukienda bongo jaribu kuwa na nembo ya mwanakijiji uone vile utapokewa kwa mikono miwili na vijana wa APSON huku wakizuia magari yote kukupisha upite........ lol
 
CCM na serikali ya mabwanyenye mafisadi washamla mshikaki huyo!!! Ndo faida ya kutmikia chama cha siasa badala ya watu. yeye alikuwa anawaidia CCM na wao wamemtumia kama napkin au CONDOM!! ukishamaliza hufui condom. Unaitupa na uchafu wake.
CCM wamemtumia balali kama CONDOM ili wasipate ukimwi wa kisiasa

Usicheze na CCM
 
Thats deep....
 
Wewe si msemaji wa familia wala hukuwapo kumuuguza mgonjwa na siku zote ulikuwa kimya kuhusu kilichomsibu Ballali, kama unakifahamu zaidi basi tumegee Watanzania, vinginevyo iache familia yake kama wataamua kuongea watasema kulikoni hadi akafikwa na umauti.

Kifo cha Dk. Ballali ni kazi ya Mungu - JK

Waandishi Wetu
Daily News; Friday,May 23, 2008 @17:01

Rais Jakaya Kikwete leo alitoa mkono wa pole kwa familia ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Ballali, huku akiwaambia kwamba kifo chake kilichotokea Marekani wiki iliyopita ni kazi ya Mungu.

Alisema katika salamu hizo kwamba amesikitishwa na taarifa za kifo cha Dk Ballali, ambaye alitengua uteuzi wake Januari mwaka huu baada ya kuibuka kwa kashfa ya kuchotwa kwa zaidi ya Sh bilioni 130 kutoka Benki Kuu.

Katika kauli yake hiyo ya kwanza kuhusu kifo cha Dk. Ballali, Rais Kikwete aliitakia familia yake maziko mema yaliyotarajiwa kufanyika jana huko Washington. Taarifa kamili ya rambirambi za Rais Kikwete ilisomeka kama ifuatavyo;

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Daudi Ballali kilichotokea tarehe 16 Mei, 2008 huko Boston, Marekani. “Wakati huu mkijiandaa kwa mazishi yake baadaye leo, napenda kutumia nafasi hii kutoa mkono wa rambirambi kwenu na kwa ndugu zenu wote.

“Naungana nanyi katika wakati wenu huu mgumu na wa majonzi makubwa kutokana na msiba mkubwa uliowakuta. Tunaelewa machungu mliyonayo kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu na kiongozi wa familia. Ni kazi ya Mungu haina makosa.

“Tunawatakia mazishi mema. Tuzidi kumuombea marehemu apate mapumziko mema. Amin.” Ballali (65) alitarajiwa kuzikwa leo jioni kwa saa za Washington (usiku kwa saa za Afrika Mashariki) katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven, baada ya misa ya kumwombea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Stephen Shahidi.

Taarifa zilizokuwa zimepatikana awali zilisema ibada hiyo ya mazishi ilipangwa kwenda sambamba na kuuaga mwili wa marehemu kuanzia asubuhi ambazo zingeihusu familia yake, ndugu, jamaa, na marafiki wa karibu tu. Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Ombeni Sefue alitarajiwa kuiwakilisha Serikali katika maziko hayo.

Dk. Ballali ambaye amefariki dunia akiwa amezungukwa na wingu kubwa la kashfa dhidi yake na taasisi aliyoiongoza, inasemekana aliacha wosia uliotaka atakapokufa azikwe Marekani.

Tangu kutangazwa kwa kifo chake zimekuwapo tetesi mbalimbali kuhusu kifo na maziko yake, huku wengi wakihoji sababu za kuzikwa kwake Marekani na baadhi ya wanasiasa na nduguze wakidai maiti yake irejeshwe nyumbani.

Hata hivyo, yalikuwapo matanga mengine shambani kwake Boko Dar es Salaam ambako mama yake mzazi anayekadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 90 anaishi. Kutokana na kuitumikia BoT, Benki hiyo ilikuwa ikijihusisha kwa karibu na msiba huo na kutoa misaada inayohitajika na viongozi wake kadhaa tayari wamefika nyumbani hapo, akiwamo Gavana wa sasa, Dk. Benno Ndulu.

Ballali alitumia sehemu kubwa ya uhai wake akifanya kazi au kupokea maagizo kutoka Washington, Marekani kwa mwajiri wake Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Ni huko Marekani pia ambako alisoma Chuo Kikuu.

Baadaye alirudi nyumbani ambako mwaka 1967-1976 alifanya kazi kama mtumishi wa Benki Kuu kwa nyadhifa mbalimbali lakini kabla ya kurudi IMF ambako alifanya kazi katika nchi mbalimbali hadi mwaka 1996 alipoombwa na Rais Benjamin Mkapa kurudi nchini na kuwa mshauri wake wa masuala ya uchumi na mwaka uliofuata akateuliwa Gavana. Kuanzia mwaka 2006-2008 alifanya kazi pia kama mjumbe wa bodi za magavana wa IMF akitokea Tanzania.
 
Back
Top Bottom