Sheikh Bura alikutwa amekufa ndani ya ofisi yake. Afande Muroto anasema sababu ya kifo ni moyo wa Sheikh Bura " kufeli. " Taarifa za watu wengine zinadai mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha matatu.
Zaidi, soma: Polisi: Mmiliki wa shule ZamZam amefariki kwa matatizo ya moyo, hakuna viashiria vya mauaji. Familia yatofautiana na Polisi
Mkuu JokaKuu
kuna msemo usemao '' ni bora kukaa kimya, unaweza kuongea na kuwatoa watu mashaka''
Kuna umuhimu wa viongozi kuchunga kauli zao, na si lazima waongelee kila jambo
Ukimsikiliza kamanda Muroto kuna maswali yanayochagiza udadisi badala ya uelewa
Wasaidizi wanaomshauri hawakumtendea haki kwa kuandaa huu mkutano
1. Kamanda anashambulia Nipashe na JF badala ya kujibu hoja za 'Wanafamilia'' waliokaririwa na magazeti mengine kama mwananchi wakizungumzia uwepo wa majeraha.
Ni muhimu kuijibu Familia, vinginevyo anashambulia messenger na si Message
2. Kamanda anadai wana simu watakazoziangalia kama zina kitu kinachohusiana na kifo Kamanda keshatoa conclusion kwamba kilichomuua ni kufeli kwa moyo.
Simu zitaleta majibu gani tofauti?
3. Kamanda kasema, aliporudi Dodoma alielekea Ofisini kwake.
Wakati huo hakuwa na mawasiliano, je, nani alimuona akielekea Ofisini?
4. Kamanda anasema, kilichomua Bura ni kufeli kwa moyo kulikosababisha ''circulation ya damu'' kukosekeana.
Hiyo ni taarifa inayotolewa na Daktari aliyefanya uchunguzi
a)Kulikuwa na postmortem na kama ilikuwepo kwanini kamanda hakueleza hilo kuondoa utata
b)Kwanini Daktari hakutoa taarifa za kitaalamu ?
Taarifa ya kamanda si ''professional' kwa kuzingatia haya
Kufeli kwa moyo (Heart Failure) si lazima iwe tukio la ghafla. Watu wanaishi na Heart Failure wakipata matibabu. Heart Failure ina maana moyo unashindwa lakini haina maana ni ghafla
Kinachoweza kutokea katika Heart Failure ya ghafla ni Heart attack ambayo huwa ni dharura
Kamanda hajaeleza kama Bura alikuwa na historia ya maradhi ya Moyo. Kama hilo lipo kuna possibility ilisababisha heart attack. Kama hakuna basi inaweza kuwa ni heart attack tu ilitokea
Yote hayo yanaelezwa kwa taarifa ya postmortem ambayo kwa nchi nyingine hutolewa na wataalam kwa kujua suala likienda mahakamani ni Dr tu anayeweza kutetea uchunguzi
Haya ni mambo yanayoelezwa na wataalam na ni magumu sana mbele ya sheria.
Kauli za kamanda mbele ya sheria zitamkwaza. Hivi akiulizwa aeleze patient history, Cardiac anatomy and physiology and pathology of heart failure ataeleza nini?
Akiulizwa Forensic ya kifo hadi kutoa conclusion ya heart failure, ataeleza nini?
Si suala a kusema kufeli kwa moyo.
Heart Failure ni topic pana sana ambayo Kamanda angepaswa kukaa mbali nayo.
Kwahiyo unaweza kuona kauli za kamanda zinavyozidi kuchanganya badala ya uhalisia
kamanda anasema waandishi waende kwa right source ambazo ni Polisi
Pengine kamanda ajiulize kwanini watu wanashaka na taarifa zao
Watu kutafuta habari za mitaani ni dalili ya kupoteza imani na right source.
Pascal Mayalla
Mkuu Nguruvi3,
Kwanza naunga mkono hoja.
Kunapotokea kifo cha utata, taarifa ya polisi ilipaswa kuishia kwenye kuthibitisha mwili umepatikana, ukiwa amekufa na daktari amethibitisha kifo .
Baada ya hapo taarifa ya kifo kimesababishwa na nini haikupaswa kutolewa na police bali daktari, tena kwa vile mwili ulifanyiwa post mortem, hata familia walipaswa kushauriwa wasizungumzie mwili umekutwajwe (bila nguo, na majeraha, umejaaje) kabla ya forensic report ambayo familia ndio hupewa na kuwa na disclosure liberty.
Marehemu kukutwa bila nguo sio uthibitisho wa crime wala mwili kukutwa na majeraha hayo matatu kwa mujibu wa mtoto wa marehemu pia sio uthibitisho wa crime kama uchunguzi wa forensic ungethibitisha hayo majeraha ni ya nini na ya lini maana mwili umekutwa ukiwa umekaa 3 days dead body in a room, hivyo there is a chance majereha hayo yalikuwa inflicted on dead body baada ya kufariki natural death.
Kitu ambacho sijasikia kikitajwa kwenye kifo hiki ni ambacho mimi nakihisi ni kuwa huyu Marehemu alitoka Dar kwenye mkutano ule ule wa CAG Mstaafu. Ulikuwa ni mkutano wa nini, ulijadili nini, waliohudhuria mkutano ule wajitokeze waseme marehemu alichangia nini kwenye mkutano ule ili tuweze ku connect the dots kama kilikuwa ni kifo cha kawaida or else.
Kwenye uwezo wa polisi wetu na serikali yetu kufanya baadhi ya mambo, unafahamika na niliisha wahi kuuzungumza hapa
WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?
Wanabodi Hili ni bandiko la kuhamasisha uzalendo miongoni mwetu sisi wana JF, pale inapotokea serikali yetu imeshindwa jambo fulani, kwa wale wenzetu wenye uwezo, jee tuwajibike kuisaidia serikali yetu au kusubiri mpaka ishindwe, halafu kazi yatu iwe ni kuikosoa tuu, kuibeza na kuizomea kuwa...www.jamiiforums.com
Haya mambo ya Ma RPC kutoa taarifa za urongo kwenye media na kutuona sisi wananchi wote kama ni watoto wa darasa la pili, pia niliisha wahi lizungumza humu kwa kumshauri IGP Sirro asiwaache ma RPC waropokaji kama hawa kulichafua jeshi letu safi la polisi
IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.
Wanabodi, Hii ni kama barua ya wazi kwa mkuu mpya wa jeshi letu la Polisi, IGP, Kamanda Simon Sirro, kutoka kwa raia mwema, anayemtakia mafanikio mema katika majukumu yake kama IGP mpya, nikimsisitiza karma ya shedding an innocent blood under any circumstances, haijawahi kumwacha mtu salama...www.jamiiforums.com
Hili la kifo hiki linahitaji maelezo ya ziada ili lieleweke.
Kwa vile Jamiiforums tumetajwa kwa kushutumiwa kwa uzushi, nashauri uongozi wa jf usikubali na tusikae kimya, hata kama aliyeleta taarifa hizo mwanzo ni just an ordinary member, lakini baada ya tuhuma kwa jf, ni ama huyo member awe equipped kwa kuwa linked na members humu wenye uwezo wa kufanya IJ wamuelekeze cha kufanya ili kuisafisha jf, au jf imtume member mwingine mwenye credentials za kufanya hayo makitu na ukweli ukibainika, ni kamanda Muroto kumpumzishwa tuu kwa uropokaji.
P
Lakini kinachonishangaza ni hiki:
Polisi Tanzania wanao utaalam wa kujua kilichosababisha kifo na kukitangaza?
Au maiti ilishafanyiwa uchunguzi na wataalam husika, na huko ndiko alikotoa taarifa hiyo?
Je, yeye ndie mwenye mamlaka ya kutoa taarifa hiyo?
Ndugu wa marehemu hawakushirikishwa katika uchunguzi uliofanyika? Kwa maana wangeshirikishwa pasingekuwepo na sintofahamu kutoka kwao.
Mimi nadhani kuna umhimu mkubwa kwa Tanzania kurudi kwenye taratibu zinazotambulika katika kufanya mambo kama haya.
Polisi hawezi kujisemea tu chochote anachoona inafaa kisemwe.
"Atawafikeni malaika wa mauti hata mkiwa ktk ngome madhubuti" quran
Rest in peace sheikh Bura
BURA NI NANI
Akimzungumzia marehemu Bura, Mkurugenzi mwenza wa Taasisi ya Dalai Islamic Centre, Abdillah Mboryo, alisema enzi za uhai wake aliwahi kufanya kazi Jeshi la Polisi Kitengo cha Upelelezi katika mikoa mbalimbali.
Mbali na hilo, pia alikuwa Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pia amewahi kuwa mlinzi wa Rais katika utawala wa awamu ya kwanza wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alisema alizaliwa miaka 60 iliyopita katika Kijiji cha Dalai wilayani Kondoa mkoani Dodoma ambapo ameacha mjane aitwaye Kuruthumu Mohammed na watoto watano.
Alisema mpaka mauti yanamfika alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Dalai Islamic Centre ambayo ilikuwa ikijihusisha na kusafirisha mahujaji kwenda nchini Makka pamoja na kuwa mmoja wa wamiliki wa shule za Zamzam.
Allah amsamehe makosa yake na kumuingiza katika rehema na pepo yake tukufu
Aamiyn
اللهم اغفر له وارحمه وعافه واعف عنه ووسع مدخله واكرم نزله وثبته بالقول الثابت
Zaidi, soma: Polisi: Mmiliki wa shule ZamZam amefariki kwa matatizo ya moyo, hakuna viashiria vya mauaji. Familia yatofautiana na Polisi