Usisubiri mafanikio yakufuate

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Kila mtu amejaliwa njia yake ya kupata mafanikio hapa duniani na kila njia ina changamoto zake na namna ya kuzitatua.

Kuna makundi mawili ya watu kwenye njia ya maisha na mafanikio, kundi la kwanza ni zao la walala hoi ambao walizaliwa hawana kitu wakatambua changamoto zao wakaamua kupambana ili kuyafikia mafanikio wameyapata au wanaendelea kupambana.

Pia kuna kundi lingine la watu ambao tangu wanazaliwa hawakupitia changamoto katika kuyafikia mafanikio.
Kwa kauli nyepesi kundi hili la pili ni kundi la watu waliozaliwa kwenye familia zenye unafuu wa maisha, wao walisubiri kupevuka tu umri kisha wakakabidhiwa mali, na fursa nyingine waziendeshe.

Kama wewe umezaliwa kwenye mazingira yanayofanana na kundi la kwanza basi tambua kuwa wewe ni mpambanaji ambae hukuanzisha vita bali unapaswa kupambana ili uweze kuishi na kupata mafanikio.

Inawezekana wazazi wako hawakuutaka umasikini walipambana sana ili wautokomeze lakini jitihada zao hazikuzidi mipango ya Mungu hivyo wakashindwa.

Pia inawezekana wazazi wako walipambana sana ili wayapate mafanikio lakini kwa bahati mbaya wakapata matatizo ambayo yaliwapelekea kifo, wakafa hawakuacha kitu kikubwa cha kurithiwa na familia ndio maana wewe ni yatima usiye na mafanikio.

Jifunze jambo kwenye picha iliyoambatana na andiko hili na uelewe kuwa "sio kila wakati mafanikio yatakufuata kuna wakati inakubidi uogelee kuyafuata mafanikio haijalishi unaona changamoto gani mbele yako wewe songa mbele"

Picha inatuonyesha kuwa kadri unavyosogea changamoto zinazidi kuwa nyepesi na mwisho utazishinda na kuyafikia mafanikio.

Usiogope changamoto, anza kupambana sasa Kuelekea njia ya mafanikio yako.

Peter Mwaihola

IMG_17025209299112924.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom