Hivi Sheria na taratibu za Uchaguzi wa viongozi ndani chama Chadema, haziruhusu mtu kuchukua form mbili au tatu kugombea nafasi tofauti tofauti?..
Je, ina maana mtu anayegombea Uenyekiti haruhusiwi kugombea Ukatibu au nafasi nyingine yaani akishindwa nafasi moja ndio basi imetoka hiyo..
Naomba kuelemishwa kwani yaonyesha wazi kuwa uchaguzi huu ndani ya Chadema umechukuliwa kama ndio kielelezo cha Uchaguzi mkuu wa 2010..
Kibanda ametoa maoni yake binafsi, ni mbaya kwa mwandishi wa habari kuwa biased kiasi hiki. Tueche demokrasia ichukue mkondo wake.
mzee hizi data umezipata wapi?profile inaonyesha amezaliwa mwaka 1950 na alikuwa naibu waziri mwaka 1988...kwenye profile inaonyesha kuwa alikuwa Executive Functionary/Officer wa TANU ndo unaibu katibu mkuu?Kibanda kwenye makala hii umekuwa upande mmoja wa Mbowe,unasema kuwa Zitto ni kijana na unakubali amesimamia mambo makubwa ya kisiasa nchini, pia amekuwa naibu Katibu mkuu kwanini ashindwe kusimamia kazi ya uenyekiti wakati Mtendaji mkuu wa chama ni katibu mkuu? Zitto awe na subira kwani hujui kuwa muda uliopo ndio wako na muda ujao si wako? una maana vijana ni taifa la Kesho? JK amekuwa naibu Katibu mkuu wa CCM akiwa na miaka 25.
amekuwa naibu waziri kwenye wizara nzito ya nishati akiwa na miaka 33.kama ZITTO ana SHINE bungeni kwanini ashindwe uenyekiti wa Chadema?
Nemesis,
Mkuu nimekupata, sasa inakuwaje ktk nafasi au niseme orodha zilizotolewa. Mtu anaruhusiwa kugombea nafasi zaidi ya moja au!..
Pasco,unafikiri kwa nini Zitto,of all the wadau wa jf wanaofuatilia hii thread,kakushukuru kwa post yako hii?
Naomba 'conclusions' ziwe kwenye ukweli. Kwamba miezi mitatu sijawa makao´makuu ni uwongo. Viongozi wote wa chama tulikuwa Biharamulo kwenye kampeni mwezi uliopita tu na baada ya hapo kuwa na vikao kadha wa kadha nje na ndani ya makao makuu.
Nadhani sio uungwana kutoa maoni katika masual ambayo huna uhakika na ukweli wake. Tusiwe emotional.
Hakuna kambi ya Zitto wala ya Mbowe katika CHADEMA. Kwa hakika uchaguzi utakwisha na chama kitakuwa imara zaidi. Mimi binafsi sigombei kwa sababu nina chuki na Mbowe au mtu yeyote wa karibu yake. Nagombea kwa sababu ni lazima chama kibadilike na kisonge mbele. Kwanini uchaguzi uonekane ni chanzo cha kuvunja chama? Mazingira ya NCCR ndio mazingira ya CHADEMA? Huu ni upotoshaji tu.
CHADEMA ina historia ya uchaguzi na chama kubaki kimoja. Mwaka 1998 Bob Makani aligombea na Ndesamburo uenyekiti wa Taifa na chama hakikupasuka. Kumekuwa na Matatizo kwamba Mbowe alipoteza makamu wake wawili kwa tofauti za mtazamo ie Dkt. Kabourou na Chacha Wangwe ambae hivi sasa ni marehemu. Hii ni sehemu ya historia ya chama, kwamba katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi wa awamu ya tatu ya CHADEMA Makamu 2 wawili wa wenyeviti waligombana na Mwenyekiti na mmoja kuondka na mwingine kusimamishwa na kisha kufariki dunia. Kipindi hicho hicho pia Naibu katibu Mkuu Bara Akwilombe akaondoka.
Vinginevyo kuna maisha baada ya uchaguzi. Sote Mbowe na Mimi tutakiwa kuendelea kujenga chama baada ya uchaguzi. Sasa woga wote huu unatoka wapi na kuanza kuweka mahitimisho hasi? Baada ya uchaguzi kama nikishindwa nitaendelea kuwa Mbunge wa chama, Katibu wa Wabunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama. Baada ya uchaguzi Mbowe akishindwa ataendelea kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kama ilivyo Mtei na Makani. Sote hatuna ujanja zaidi ya kujenga chama na kukiimarisha.
Baadhi ya Watanzania tuna tabia ya mawazo mgando kwamba uchaguzi ni chuki, kutukanana nk. Sasa mkishatukanana, mtajenga tena chama baada ya uchaguzi? Cheo ni dhamana inasema moja ya ahadi ya mwana TANU...............
- Haya ni maneno ya Zitto toka blog moja huko pembeni, saafi sana hebu msome kidogo:-
Baada ya uchaguzi kama nikishindwa nitaendelea kuwa Mbunge wa chama, Katibu wa Wabunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama. Baada ya uchaguzi Mbowe akishindwa ataendelea kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kama ilivyo Mtei na Makani. Sote hatuna ujanja zaidi ya kujenga chama na kukiimarisha.
Baadhi ya watu wanafikiri Siasa ni "Chuki"...Watz hawana culture hio..Zitto kuwashukuru hao Mafisadi haimaanishi basi nae fisadi...Kutetea Ununuzi wa Mitambo ni sababu ya Msingi, kila mtu anafikra zake kupima SIASA vs Hali ya Uchumi wakati husika. Ndio maana watu hukaa vikao....ktk Vikao kuna kutafautiana na ndio Ubinaadamu...!!!..otherwise turudi ktk system za Udikteta!!!
I who loses?
Mr. Chuma
Tusiwe wepesi wa kusahau, Mh. Zitto kwenye Mitambo ya Dowans akubali kabisa kwamba alichemsha, mpaka Mwakyembe akasema hivi ni Zitto ninaye mfahamu au ni mwingine!
NITASEMA UKWELI DAIMA