Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

Manyerere Jacton, asante kwa taarifa.
Mwanajf mwenzetu. Abs K. Get well soon!.
P.
 
kama wahusika ni serekali ya Tanzania chini ya fast jet usitegemee wasika kukamatwa rejea kifo cha RPC wa mwanza wahisika walikamatwa ndani ya week .
 
pole sana ndugu yangu Kibanda, Mwenyezi
Mungu akujalie upone haraka
 
Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.


Huyu Baba ana maneno matamu zaidi ya asali, ana uwezo wa kuahidi hata kujenga Mbingu, tusubiri tuone sinema yaja sterring kishaanza!
 
Waliomshambulia inasemekana walikua wakimwita kiongozi wao 'afande'. Kama sio dola tuseme labda ni wanausalama wa dola wamekodishwa na watu binafsi? Au mnasemaje wana jf!! Wananchi tunafahamu askari wetu kwa kubobea kula rushwa siku hizi wanaweza kukodishwa!
 
Kauli za jk dhidi ya uhai hazina tija!
Na msitarajie wahusika kukamatwa.

Mheshimiwa ana list ndefu ya kuhakikisha wahalifu wanakamatwa, waliompiga kubenea,ulimboka,shehe znz,padri znz,padri aliyeuwawa znz na sasa kibanda, kazi kweli.
 
huyu jamaa hapa namnukuu "Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania." ni mnafiki sana.....kulikuwa na haja gani ya kuripoti upasuaji na kutuambia ya Jekey?.....ni heri wange kuumiza wewe Neville kwa kuwa ni mnafiki kuliko watu wote ninao wajua

kaka una point ya msingi sana
 
Bado ninatafakari hii elimu ya kutesa watu kwa KUNG'OA KUCHA, KUNG'OA MENO KWA PRISE KUPASUA VICHWA KWA NONDO, mimi ninafikiri lazima kipo chuo cha kufanya mambo haya kama kweli kuna nia thabiti ya uchunguzi waanzie hapo.
 
kama wahusika ni serekali ya Tanzania chini ya fast jet usitegemee wasika kukamatwa rejea kifo cha RPC wa mwanza wahisika walikamatwa ndani ya week .

wale simu ndo ilichangia kunaswa haraka,lakini hata hawa waliompiga sibanda kama makachero wako serious hawatachukua round.
 
Maswali mengi .... Taarifa ya hizi kamati zinazoundwa kila kukicha kutokeapo matukio kama hili .....zinaishia kwenye makabrasha? mwisho wake ni nini..... kulingana na hali halisi jambo kama hili litaendelea na litazoeleka na litakuwa la kawaida.. kawaida... kawaida... mimi naogopa kuuliza baada ya hao waliotendwa Kuanzia Kubenea na waliofuatia NANI ATAFUATA.....????

 
Mheshimiwa ana list ndefu ya kuhakikisha wahalifu wanakamatwa, waliompiga kubenea,ulimboka,shehe znz,padri znz,padri aliyeuwawa znz na sasa kibanda, kazi kweli.

kila mtu lazima achunge usalama wake.mtu kama kibanda anakosa hata mguu wa kuku wakati kazi yake ni ya hatari hadi watu wanafungua mlango wa gari na kumchomoa toka ndani ya gari.
.
 
Kikwete nae mara yupo south..
Ya kubenea ilimkutia huko na hii ya kibanda hukohuko. Sijui ni coincidence au ndo kutotulia nyumbani?
hivi hajaenda kwenye mazishi na jua kwasasa ameshanunua suti ya kujiandaa kwenda kesha..kama ni raisi tunae yaani ningekuwa polisi ningemkamata uzururaji..........
 
wale simu ndo ilichangia kunaswa haraka,lakini hata hawa waliompiga sibanda kama makachero wako serious hawatachukua round.
Ya kubenea alikuwa na meseji za wahusika mbona hawajakamatwa mpka leo...
 
kaka kuweni makini isije ikawa wamekuja kummalizia!
 
Taarifa kutoka South Africa, kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania

1.
Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.

3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.

4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.

5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.

--

Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556


mkuu tunashukuru sana kwa updates na tunamuomba MWENYEZI MUNGU AMPONYE NA KUMPUNGUZIA MAUMIVU NDUGU YETU KIBANDA. Hapo kwenye blue kwa upande wangu hata sitaki kusikia habari zao hao ,kuna matukio mangapi toka wawe madarakana yanayofanana na hili ambayo hatujaona huo uchunguzi wanaoutangaza ukifanya chochote au kuwapata watuhumiwa na kuwapeleka mahakamani. Tumechoka na hizo hila zao sisi.
 
Wapendwa, habari za uhakika zilizofika sasa hivi kutoka hospitalini Afrika Kusini alikolazwa Kibanda ni kwamba ameshatolewa jicho moja ambalo liliharibiwa kabisa na wavamizi. Tayari ameshatoka Theater.Tutaendelea kujuzana.
 
Back
Top Bottom