Napenda kuwapa taarifa za nyongeza kuhusu tiba ya Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda ambaye leo amefanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.
1. Nimepokea taarifa kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Hussein Bashe kwamba tayari Mwenyekiti wetu, Kibanda ametoka theater alikokuwa akifanyiwa upasuaji. Hata hivyo taarifa mbaya ni kwamba Madaktari wameshindwa kuokoa jicho lake la kushoto hivyo wamelingoa.
2. Wamechukua hatua hiyo ya kitatibu baada ya kuwa tayari jicho hilo lilikuwa limepondeka kwa ndani hivyo lisingeweza tena kuona. Atawekewa jicho la bandia la plastiki ambalo hata hivyo halitakuwa likiona.
3. Jambo la kumshuruku Mungu ni kwamba kwa ujumla upasuaji huo uliochukua saa 5 na dakika 30 umefanyika kwa ufanisi mkubwa na ulikuwa ukiongozwa na madaktari bingwa watatu. Wawili kati yao ni wataalamu wa kichwa na mmoja ni mtaalamu wa macho.
4. Katika upasuaji huo, hakukuwa na madhara ya ndani katika kichwa chake, hivyo kichwa kiko salama. Sura yake imejengwa upya kutokana na majeraha ambayo yalikuwa yametapakaa baada ya kupigwa na watu wasiojulikana.
5. Changamoto kubwa waliyokutana nayo madaktari walionfanyia upasuaji ni kurejesha katika sehemu yake baadhi mifuma midogo inayozunguka jicho pia kurejesha taya la kushoto ambalo lilikuwa limeathiriwa na tukio la kupigwa kwake. Hata hivyo hatimaye walifanikiwa.
6. Ripoti kamili kuhusu upasuaji huo inatarajiwa kutolewa kesho Jumapili na madaktari hao.
Tuendelee kumwombea Mwenyekiti wetu Kibanda ili Mungu amponye. Kwaniaba ya Bodi ya Wakurungezi ya Jukwaa la Wahariri, kwa mara nyingine tunampa pole Kibanda pamoja na familia yake na tunamtakia uponyaji wa haraka.
--
[FONT=tahoma,sans-serif]Neville C. Meena,[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif]Secretary General,[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif]Tanzania Editors Forum - TEF,[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif]Dar es Salaam - Tanzania.[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif]Cell: +255 - 787 - 675555[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif] +255 - 753 - 555556[/FONT]