Kesi yenye utata: Binti adai kuzaa na baba yake watoto 3 lakini akana mahakamani

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,847
18,254
Kesi ya baba kuzaa na mwanaye watoto 3 imechukua sura mpya baada ya binti huyo aliyekimbilia polisi kufungua kesi kukana mashtaka baada ya kesi kufikishwa mbele ya hakimu huko Rufiji.

Awali binti huyo alidai kuwa baba yake alianza kumgegeda tangu mwaka 2019 na kufanikiwa kuzaa naye watoto 3 na watoto wote wamepewa ubini wa baba yake mzazi kudhihirisha kuwa yeye ndiye aliyemzalisha watoto hao.

Soma zaidi:

Tatizo lilianzia hapa:
1. Polisi wamdaka baba anayedaiwa kuzaa na bintiye

2. Baba anayedaiwa kuzaa na bintiye afikishwa mahakamani, arudishwa tena polisi

Utata wa kwanza:
Kesi hii inadhihirisha udhaifu uliopo kwenye jeshi letu la polisi hasa kitengo cha upelelezi. Polisi wanadai upelelezi umekamilika. Je, upelelezi utakamilikaje kabla ya kupima DNA? Ina maana wanafanya kazi kwa kusikiliza maneno ya watu? (rejea mwanzo wa sakata hili)

Utata wa pili:
Baba kumgegeda bintiye kwa muda wa miaka 4 na kuzaa naye watoto 3 huku jamii ikishuhudia, huu nao ni utata unaodhihirisha jinsi jamii yetu ilivyokengeuka. Inakuwaje baba amgegede bintiye kwa muda wote huo bila uongozi wa kitongoji, kijiji na kata kuchukua hatua? Kama ningekuwa na mamlaka ya kusimamia jambo hili, hawa viongozi wote ningewsukumia ndani ili liwe fundisho kwa wengine.

MAONI YANGU
Natoa wito kwa jeshi la polisi kufanya kazi kiuweledi badala ya kutumia mbinu za ujima kuwafungulia watu mashtaka (ya kweli au ya uongo). Polisi kufanya kazi kwa mazoea kunasababisha watu kufungwa kwa makosa wasiyotenda au wenye makosa kuachiwa huru kwa sababu ya kutokuwepo ushahidi wa kutosha.

Najiuliza: Ina maana polisi walishindwa hata kuomba vyeti vya kuzaliwa hawo watoto ili vitumike kama ushahidi? Kwenye vyeti vya kuzaliwa jina la baba huandikwamo na pia baba hutakiwa kuhudhuria kliniki. Je, polisi walishindwa hata kuwaomba manesi wawape ushahidi kuhusu baba halisi wa watoto aliyekuwa akihudhuria kliniki?

Ifike mahali jeshi la polisi lijithathmini upya katika utendaji wake ili kuepuka kuabika hadharani kiasi hiki.

Nawasilisha.
 
Wapi wamesema DNA haikufanyika!! Unajuaje mashahidi wanaofuata atakuja shahidi toka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali, maana victim kawaida huwa shahidi wa kwanza na mashahidi hawaji siku moja na kesi haisikilizwi siku moja, sioni utata hapo,
 
Back
Top Bottom