WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 18.
Job Mrema: Na tamko hilo umelitoa kupitia chombo gani cha habari?
Brenda: Nimefanya Live TikTok kupitia kamera ya simu yako, na mtu yeyote aliyepo TikTok anaweza kukusikiliza.
Job Mrema: Ni sahihi kwamba ulilenga umma?
Brenda: Ni sahihi.
Job Mrema: Ilikuwa tarehe ngapi?
Brenda: Sikumbuki, ila ilikuwa kati ya Aprili mwaka jana hadi sasa, baada ya Mwenyekiti kukamatwa.
Job Mrema: Ni sahihi kuwa kutojua sheria siyo kinga?
Brenda: Ni sahihi.
Job Mrema: Na ni kweli kwamba jinai haiozi?
Brenda: Sahihi.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba tamko ulilotoa ni kinyume na sheria?
Brenda: Sifahamu.
Job Mrema: Waheshimiwa Majaji, naomba kumalizia hapa ili niwaruhusu wenzangu waendelee na maswali.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, naomba kabla sijaendelea nimkabidhi kwanza Mshtakiwa nyaraka mbalimbali, ni cases mbalimbali.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, unazihitaji?
Lissu: Nashangaa zimefikaje huko.
Nassoro Katuga: Mawakili wake ndiyo wametupatia, wakijua hawana locus katika hii kesi.
Lissu: Mawakili wa Serikali hawana mamlaka yoyote ya kugusa nyaraka zangu na hawana mamlaka ya kufanya clearance ya nyaraka zangu. You should never touch my documents again.
Nassoro Katuga: Na sisi hatutogusa nyaraka zake.
Dr. Nshala: Niliwapa Magereza, wakaomba nipitishe kwa Mawakili wa Serikali.
Nassoro Katuga: Hii sasa ni fujo. Huyu anayeongea hana locus ya kuzungumza.
Jaji Ndunguru: Naomba tuendelee, lakini siku nyingine tumia muda wa break kama unahitaji nyaraka zako, au iombe Mahakama ndiyo itatoa amri nani apewe nini wakati mwingine. Isitupotezee muda.
Lissu: Sawa.
Jaji Ndunguru: Tuendelee.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, naomba kupata mwongozo wa Mahakama hii. Nina maswali zaidi ya 50 na hayajirudii hata swali moja. Hata nikipewa saa moja sitamaliza.
Jaji Ndunguru: Malizia kwanza dakika 5 mlizopoteza wakati wa kujibizana kuhusu nyaraka, na nusu saa ya asubuhi tuliyopoteza.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba tuendelee. Asubuhi haiwezi kuwa kosa la Magereza kuanza saa 3:30, sababu Magereza walinifikisha saa 3 asubuhi.
Jaji Ndunguru: Tuendelee kidogo.
Nassoro: Nitakuwa sahihi kwamba wewe, ndugu yangu, kama kaka na dada, kwa maana Rupia ni Mnyamwezi?
Brenda: Huwezi kuwa kaka yangu wakati unataka Mwenyekiti wangu anyongwe.
Jaji Ndunguru: Tuendelee, mnapoteza muda.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, tarehe 29 Oktoba 2025 ulikuwa wapi?
Brenda: Nilikuwepo nyumbani.
Nassoro Katuga: Nyumbani wapi?
Brenda: Nyumbani Basihaya.
Nassoro Katuga: Tuambie cheo chako kingine kwa hapa Pwani.
Brenda: Katibu wa BAWACHA Mkoa wa Kinondoni.
Nassoro Katuga: Ulitaja hapo mwanzo?
Brenda: Nilitaja.
Nassoro Katuga: Ulisema kwamba uliangalia social media inayoitwa Jambo TV?
Brenda: Ni kweli.
Nassoro Katuga: Kuna social media inaitwa Jambo TV?
Brenda: Ni YouTube channel.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo, mwanzo haikuwa sahihi kusema social media ya Jambo TV?
Brenda: Ndiyo, kwa sababu unani-confuse.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba unaniconfuse.
Brenda: Yeah, unani-confuse.
Nassoro Katuga: Si umesema mimi siyo kaka yako?
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, uliposema slang ni lugha ambayo siyo rasmi.
Brenda: Utakuwa sahihi.
Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisema maana ya slang na inatumika na group gani.
Brenda: Nilisema maana yake, ila sikusema inatumika na group gani.
Nassoro Katuga: Kama nilikusikia ukisema kwamba kukinikisha ni kukifanya kinukie, ni slang au Kiswahili rasmi?
Brenda: Kukinukisha siyo Kiswahili rasmi.
Nassoro Katuga: Nikifanya hiki kinuke, nitakuwa sahihi kusema nakinukisha?
Brenda: Both.
Nassoro Katuga: Kwa kuwa hujataja ni kundi gani, kwa sisi watoto wa mjini, kukinikisha ni slang inayotumika na vijana wengi.
Brenda: Utakuwa sahihi.
Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema kukinikisha ni kwenda kufanya jambo fulani?
Brenda: Kwenda ni sawa, ila kufanya jambo sina hakika.
Nassoro Katuga: Hebu waambie Waheshimiwa Majaji, kwa cheo chako...
Jaji Ndunguru: Hilo litakuwa swali la mwisho.
Nassoro Katuga: Hebu waambie Waheshimiwa Majaji, kwa cheo chako, kama nimekusikia umesema Rais wa Serikali ya Muungano hajatajwa.
Brenda: Nilisema katika paragraph aliyonisomea Mwenyekiti.
Nassoro Katuga: Sasa waambie Waheshimiwa Majaji, Serikali ya Muungano ni kitu gani?
Brenda: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nassoro Katuga: Serikali ya Muungano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni kitu sawa?
Nassoro Katuga: Naomba ni-pause hapo. Niliambiwa ni swali la mwisho.
MAHAKAMA: Shauri linaahirishwa mpaka kesho saa 3:00 asubuhi.
MAHAKAMA: Shahidi hujamaliza kutoa ushahidi wako. Utatakiwa kuwa hapa kesho saa 3:00 asubuhi.
MAJAJI WANATOKA.
TUKUTANE KESHO ASUBUHI.