Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Shahidi wa nne katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia, leo Septemba 8, 2026 ataendelea kutoa ushahidi wake wa utetezi dhidi ya Tundu Lissu.


Jana Septemba 7, 2026, shahidi huyo alianza kutoa utetezi wake, ambapo Lissu alianza kwa kumuongoza kujibu maswali kwamba mkutano wa tarehe 3 Aprili ulihusu nini na nani aliyeuandaa. Katika majibu yake, shahidi alieleza kuwa mkutano huo ulilenga kuwakutanisha watia nia wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ili kuzungumzia msimamo wa chama wa "No Reforms No Election".

Alisema kwamba uamuzi wa kufanyika kwa mkutano huo ulifanywa na Katibu Mkuu wa chama, John Mnyika, pamoja na Sekretarieti, wala haukuandaliwa na Tundu Lissu kama inavyodaiwa.

Shahidi huyo aliongeza kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano iliyopo chini yake (Brenda Rupia) ndiyo iliyoandaa taarifa kwa umma na kuwaalika waandishi wa habari bila kuwapa maelekezo yoyote ya kikazi au ya kurusha matangazo moja kwa moja kuhusu mkutano huo wa mwezi Aprili 2025.

Katika ushahidi wake, Brenda Rupia alisisitiza kuwa Lissu alihudhuria mkutano huo kama mzungumzaji mkuu kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Taifa na hakuwa na uhusika na ualikaji wa vyombo vya habari.

Rupia alieleza zaidi kwamba hata umiliki wa maudhui yote ya habari yaliyorekodiwa siku hiyo ulikuwa chini ya vyombo husika vilivyohudhuria na sio Chama wala viongozi wake.

Update kutoka Mahakamani

Shahidi no 4 na Mkurugenzi wa mawasiliano, Brenda Rupia pamoja na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Saidi Mzee na Mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema katika ukumbi wa Mahakama Septemba 8, 2026.

Tundu Lissu amefikishwa mahakamani muda huu.

Mwenyekiti wa kanda ya Pwani Mh Boniface Jacob akiwasili mahakamani


Mwenendo wa Kesi, Septemba 8, 2026 tuliishia sehemu ya 364 sasa leo tunaendelea na sehemu ya 365 ambapo Shahidi wa 4, Brenda Rupia anaendelea kutoa ushahidi wake kutokea alipoishia jana.

Mahakama inaanza.

Majaji wameshaingia Mahakamani muda huu.

Mwenyekiti Tundu Lissu pia ameshaingia.

Jaji anasema tuendelee

Anasimama Karani anasema Criminal session No. 19605 kati ya Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.

Ajuaye kama kawaida Wakili wa Serikali anatambulisha wenzake na kusema tuko tayari kuendelea.

Brenda anapanda kwenye kizimba ambacho kinatumika kwa ajili ya Ushahidi.

Jaji Ndunguru anamwambia nakukumbusha kwamba upo chini ya kiapo.

Lissu: Naomba waeleze Majaji uwepo wako katika mkutano huo wote.
Brenda: Waheshimiwa Majaji nilikuwepo katika mkutano huo wote
Lissu: Waeleze Majaji watu waliokuwa wazungumzaji katika Mkutano huo.
Brenda: Wazungumzaji walikuwa ni wale viongozi 6 wakuu niliowataja jana.
Lissu: Mzungumzaji mkuu katika mkutano huo alikuwa nani?
Brenda: Mzungumzaji mkuu wa mkutano huo alikuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Tundu Lissu
Lissu: Mkutano huo ulichukua muda gani?
Brenda: Masaa matatu hadi matatu na nusu
Lissu: Mzungumzaji mkuu unakumbuka alizungumza kwa muda gani?
Brenda: Mzungumzaji mkuu ndio aliongea kwa muda mrefu kuliko wote masaa mawili hadi mawili na nusu
Lissu: Nashtakiwa kwa maneno yasemayo (Lissu anasoma maneno ya kwenye hati ya mashtaka yanayodaiwa ya uhaini). Waeleze majaji haya maneno niliyoyasoma nimetumia muda gani kuyasoma
Brenda: Sio zaidi ya dakika mbili
Lissu: Waeleze majaji hotuba yangu ilichukua muda gani katika mkutano huu?
Brenda: Masaa mawili mpaka mawili na nusu
Lissu: Shtaka dhidi yangu linasema haya maneno niliyoyasema Jamhuri wanasema nilikuwa na lengo la kuitishia serikali, waeleze majaji uwepo wa maneno Serikali ya JMT
Brenda: Hakuna neno Serikali ya JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa neno Rais wa JMT
Brenda: Hakuna uwepo wa neno Rais wa JMT
Lissu: waeleze Majaji katika maneno niliyokusomea uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT
Brenda: Hakuna maneno Makamu wa Rais JMT
Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Waziri Mkuu wa JMT
Brenda: Hakuna maneno Waziri Mkuu wa JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Baraza la Mawaziri wa JMT
Brenda: Hakuna uwepo wa maneno Baraza la Mawaziri wa JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT
Brenda: Hakuna maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya JMT
Brenda: Hakuna maneno Mkurugenzi wa Mashtaka wa serikali JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Halmashauri, Manispaa au Serikali ya Mtaa
Brenda: Hayo maneno yote hayapo
Lissu: waeleze majaji uwepo wa maneno Mkuu wa Mkoa, au kiongozi mwingine yeyote wa serikali
Brenda: Hayo maneno hayapo
Lissu: Mtu akikuambia haya maneno niliyokusomea yanaitishia Serikali ya JMT wewe unasemaje?
Brenda: Mimi naona sio kweli hayaitishii serikali ya JMT
Lissu: Katika hayo maneno niliyokusomea waeleze majaji uwepo wa maneno yoyote yanayohusu jeshi lolote nchi hii
Brenda: Hayo maneno hayapo
Lissu: Nikisema Jeshi lolote nina maana ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Magereza, Jeshi la akiba, Jeshi la Mgambo, Mgambo wa Jiji, Idara ya Usalama wa Taifa
Brenda: Yote hayo hayapo.

Sehemu ya 366

Lissu anaendelea kumuongoza shahidi wake ambae ni Mkurungenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA, Brenda Rupia.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji hayo maneno niliyokusomea yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, kuna maneno tutakwenda kuvunja sheria za nchi

Brenda: Hayo maneno hayapo

Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno tutaenda kupiga watu wanaoenda kupiga kura au kuwakata vidole

Brenda: Hayo maneno hayapo

Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno mkachome vituo vya mwendokasi, daladala au mabasi yenyewe

Brenda: Hayapo kabisa

Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno tutawapiga wasimamizi wa uchaguzi na kuchoma vituo hivyo

Brenda: Hayo maneno hayapo

Lissu: Kuna maneno yamesemwa kwamba polisi 16 waliuwawa wakati wa uchaguzi wa Okt 29, 2025, waeleze majaji uwepo wa maneno tutakwenda kuua polisi wakati wa uchaguzi

Brenda: Maneno hayo hayapo

Lissu: Kwa ufahamu wako shahidi, mtu akisema msimamo huu unaashiria uasi anakuwa ametenda kosa gani?

Brenda: Mtu akisema msimamo huu unaashiria uasi sio kosa kwasababu uasi ni kupinga pamoja na kukataa jambo

Lissu: Mtu akisema tutazuia uchaguzi anakuwa ametenda kosa gani kwa ufahamu wako?

Brenda: Sio Kosa mtu akisema tutazuia uchaguzi

Lissu: Kwa ufahamu wako mtu akisema tutavuruga uchaguzi anakuwa ametenda kosa gani ?

Brenda: Kwa ufahamu wangu sio kosa

Lissu: Kwa ufahamu wako mtu akisema tutahamasisha uasi anakuwa ametenda kosa gani katika nchi hii?

Brenda: Anakuwa hajatenda kosa lolote

Lissu: kwa ufahamu wako mtu akisema tutakinukisha, anakuwa ana maana gani?

Brenda: kwa ufahamu wangu tutakifanya kinukie, tukipika pilau inanukia pia

Watu kicheko😂😂😂😂

Lissu: Kufanya kitu kinukie ni kosa gani kwa sheria za nchi hii?

Brenda: Sio Kosa

Lissu: Kufanya kitu kinuke ni kosa gani kwa mujibu wa sheria za nchi hii?

Brenda: Sio Kosa

Lissu: Waeleze majaji usahihi wa maneno kukinukisha ni maneno ya mtaani / slang yaani sio neno rasmi

Brenda: Ni neno la mtaani sio neno rasmi hivyo ni slang

Lissu: Nimekuuliza juu ya maana ya neno mojamoja kwenye yote yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, sasa nakuuliza kwa ujumla wake, haya maneno yanaonyesha kosa gani?

Brenda: Hayo maneno hayaonyeshi kosa lolote

Lissu: ushahidi umetolewa hapa mahakamani kuwa haya maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, yalichapishwa kwenye YouTube ya Jambo TV

Brenda: Niliona hiyo video kwenye mtandao wa Jambo TV

Lissu: Hiyo video uliyoiona kwenye mtandao wa jambo TV ina urefu kiasi gani?

Brenda: Masaa mawili na nusu hadi masaa matatu

Lissu: waeleze majaji katika hayo masaa mawili na nusu hadi matatu, haya maneno ndio pekee yaliyopo kwenye hiyo video?

Brenda: Sio hayo maneno pekee kwasababu Mwenyekiti alizungumza kwa masaa mawili na nusu hadi matatu

Lissu: Waeleze majaji uwepo wako wakati mashahidi wa Jamhuri wakitoa ushahidi

Brenda: Nimekuwepo kwa sehemu kubwa wakati mashahidi wa upande wa mashtaka wakitoa ushahidi wao

Lissu: Waeleze majaji kama uliona hiyo video ikionyeshwa mahamamani

Brenda: Hapana sijaiona.

Mhe. Lissu: waeleze majaji, uwepo wa ushahidi mwingine wowote zaidi ya maneno yao tu matupu hawa Jamhuri

Brenda: Hakuna zaidi ya maneno matupu tu

Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wa Jamhuri wamesema hiyo video uliyoiona Jambo TV mimi ndio niliichapisha kwenye mtandao wa Jambo TV

Brenda: That is impossible kwasababu Tundu Lissu sio mfanyakazi wa Jambo TV

Mhe. Lissu: ushahidi umetolewa kwenye Mahakama hii kuwa baada ya mimi kufunguliwa mashtaka, kulikuwa na kamatakamata sana juu ya viongozi wa chama, waeleze majaji ufahamu wako juu ya hii kamatakamata

Katuga: Tunapinga hilo swali kwasababu ni leading, tunaomba lisiulizwe

Sehemu ya 367

Lissu anaendelea kumuongoza shahidi wake ambae ni Mkurungenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA Hq, Brenda Rupia.

Mhe. Lissu: Swali langu sio leading kwasababu a leading question attracts a yes or no answer. Suala la whether kumekuwa na kamatakamata limejitokeza kwa pande zote, extensively defense witnesses wamezungumza extensively na Jamhuri waliuliza maswali mengi ya dodoso.

Katuga: hakuna sheria inayosema a leading question ni lile swali ambalo lina suggest answer. Ingawa kifungu cha 160 cha Sheria ya Ushahidi kinasema Mahakama inawezs kuruhusu leading question lakini leading question imekuwa defined under section 159 of the Evidence Act.

Jaji Ndunguru: Kanuni za ushahidi in chief, ni kuwa shahidi anapaswa kusimulia anachokifahamu. Hivyo tuongozwe na msingi huo. Twendelee.

Mhe. Lissu: Shahidi nini kilitokea baada ya mimi kukamatwa?

Brenda: Chama kilifungiwa tarehe 10/06/2025 na viongozi walianza kukamatwa na mimi nilikamatwa tarehe 12/07/2025 Namanga Border Stop nikiwa naelekea Nairobi kwaajili ya kutembelea ndugu na baadae nianze safari kuelekea Ujerumani lakini sikufanikiwa kuvuka border.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji ulikuwa unaenda Ujerumani kufanya nini?

Brenda: Nilikuwa naenda kwaajili ya training ya communication skills

Mhe. Lissu: Ielezee hiyo training

Brenda: Kabla ya chama hakijafungiwa Katibu Mkuu aliniappoint Mkurugenzi wa Mawasiliano kwenda Ujerumani kwenye training lakini sikufanikiwa baada ya kukamatwa na nilisafirishwa kwenye gari aina ya probox kwa speed ya 120 na kuendelea na stop ya kwanza ilikuwa Longido ambapo niliingizwa kituo cha polisi bila kuandikisha, hawakuniambia kwanini tulisimama pale hata nilipouliza hawakuniambia chochote na kulikuwa na confusion na kelele baina yangu na hao majamaa ambao walinipeleka pale.

Mhe. Lissu: Kitu gani kilitokea baada ya hapo?

Brenda: Baada ya kupiga kelele nyingi sana wakaniambia sasa tunakupeleka Central Police Arusha na wakaniambia niko salama niko mikononi mwa polisi. Nilikuwa na hofu kubwa sana kwasababu gari ilikuwa inatembea speed isiyo ya kawaida kuelekea Arusha.

Mhe. Lissu: Ilikuwaje mlipofika Arusha?

Brenda: RPC wa Arusha alikuja kuonana na mimi parking. RPC alitukabidhi gari nyingine aina ya VX yenye plate number ya Zanzibar. Wakaongezeka pia wanaume wawili na wakasema tunaenda Dar es Salaam kuanzia saa nne usiku. Hii gari ilitembea kwa speed kubwa sana na kila tuliposimamishwa walikuwa wakisema ni kazi maalumu na tunaruhusuwa kupita.

Mhe. Lissu: Mliposimamishwa na wakina nani?

Brenda: Traffic wa barabarani.

Mhe. Lissu: Mlifika Dar es Salaam saa ngapi ?

Brenda: Tulifika Dar es Salaam saa kumi alfajiri na tulifika Oysterbay. Wakawa wanamtafuta mtu niliyepaswa kuonana nae wakaambiwa nendeni Central Police, baada ya kwenda Central na kufika. Walimpigia simu George Bagyemu na aliwaambia anakuja na alikuja majira ya saa kumi na moja na nusu

Mhe. Lissu: Baada ya George Bagyemu kufika kitu gani kilitokea?

Brenda: Neno lake la kwanza alisema nilikuwa nakusubili nitakuweka ndani zaidi ya wiki mbili. Na wakaniambia walikuwa wananitafuta kwasababu ya taarifa kwa umma niliyoitoa kwa umma 2/7/2025

Mhe. Lissu: Waeleze majaji hiyo taarifa ilikuwa inahusu kitu gani?

Brenda: Inahusiana na Mbunge wa Bunge la Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje kwenye Bunge la EU anaitwa David McAllister, kuhusiana na ripoti kuwa kuna mpango wa Mwenyekiti kupewa sumu akiwa kizuizini gerezani. George Bagyemu akakabidhiwa passport yangu yenye namba TAE481364 ambayo mpaka leo hii sijawahi kurudishiwa passport yangu wala simu yangu.

Mhe. Lissu: Baada ya hapo kilitokea kitu gani?

Brenda: Waliniambia wanaenda kunipekua nyumbani na tulielekea nyumbani Basihaya nikiwa kwenye karandinga la polisi.

Sehemu ya 368

Lissu anaendelea kumuongoza shahidi wake ambae ni Mkurungenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA Hq, Brenda Rupia.

Mhe. Lissu: waeleze majaji mlipofika nyumbani nini kilitokea?

Brenda: Walipekua kila chumba, nguo zote, hawakuniambia wanatafuta nini lakini nadhani hawakukikuta walichokuwa wanakitafuta

Mhe. Lissu: Waeleze majaji Mapolisi waliokupekuwa walikuwa na search warranty or search order.

Brenda: Sikumbuki maana nilikuwa na stress nyingi sana.

Mhe. Lissu: Baada ya hapo nini kilitokea?

Brenda: Tulirudi central polisi na nilikaa central siku nne na nusu lakini sikufikishwa mahakamani wala sikupewa mashtaka yoyote.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji ulikuwa under police custody kwa siku ngapi kuanzia Namanga hadi central?

Brenda: Siku nne na nusu

Mhe. Lissu: Waeleze majaji tangu siku hiyo mpaka leo ulipelekwa mahakamani?

Brenda: Sijawahi kupelekwa mahakamani mpaka leo

Mhe. Lissu: Waeleze majaji wewe kutoa taarifa kwa umma kuhusu chapisho la David McAllister Mbunge wa EU na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la EU alilochapisha kuwa Mwenyekiti anampango wa kuwekewa sumu gerezani, ulitenda kosa gani wewe?

Brenda: Sikutenda Kosa lolote

Mhe. Lissu: Nini kilitokea baada ya wewe kuachiwa?

Brenda niliendelea na maisha yangu kama kawaida.

Mhe. Lissu: waeleze majaji nini kilitokea kwa viongozi wenzako wengine wa chama

Brenda: Wakati siku hiyo nakamatwa Namanga usiku wa Tarehe 12/7/2025 Mtaalamu wa Rasilimali za Chama Leonard Magere nae alikamatwa Julius Nyerere Airport alipokuwa anaelekea London.

Mhe. Lissu: Alishikiliwa kwa muda gani?

Brenda: Sikumbuki ila nilikutana nae Mahabusu Central Police Dar es Salaam. Nakumbuka Amani Golugwa nae alikamatwa Airport akiwa anaelekea Belgium na pia kulikuwa na mwendelezo wa ukamataji maana Makamu nae alikamatwa na kukaa mahabusu muda mrefu.

Mhe. Lissu: Wewe ulikamatwa, Magere alikamatwa, Makamu alikamatwa , waeleze majaji nani alifunguliwa kesi mahakamani?

Brenda: Hakuna aliyefunguliwa kesi mahakamani

Mhe. Lissu: Nataka nikuulize maswali machache nimalizie

Jaji Ndunguru: Amechomekea Machache mangapi?

Watu kicheko: 😂😂😂😂😂

Mhe. Lissu: Hayatafika kumi.

Mhe. Lissu: Hotuba yangu ya tarehe 3/4/2025 ilihusu mambo gani makuu?

Brenda: Waheshimiwa Majaji Mwenyekiti Lissu alieleza matatizo ya mifumo ya uchaguzi, sheria zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho, matatizo yaliyotokea chaguzi zilizopita, kwanini Nchi inahitaji electrol reforms, kwanini tunapaswa kuwaelimisha wananchi kuhusu msimamo wa No Reforms, No Elections. Alisema, bila reforms ni ngumu kupatikana kwa democratic elections. Hayo maneno ya uasi yalitokana na msimamo wa G-55.

Mhe. Lissu: G-55 ni watu gani?

Brenda: G-55 ilikuwa ni kikundi cha watu ndani ya chama waliotaka kushiriki uchaguzi. G-55 waliandika kwenye social media kuwa msimamo wa no reforms no election unaashiria uasi kwahiyo Mwenyekiti alikuwa anaelezea huo uasi kuwa ni kupinga uchaguzi ambao sio huru na sio wa haki.

Hapa Brenda ameleta ushahidi mzuri wa hii G-55 ambao mashahidi waliopita hawakuusema.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa nia ya kuitishia serikali katika hotuba yote hiyo ya masaa mawili na nusu hadi matatu

Brenda: Sioni nia ya kuitishia Serikali katika hotuba ile.

Mhe. Lissu: waeleze majaji umenifahamu kwa muda gani na unanifahamu kuwa mimi ni mtu wa aina gani?

Brenda: waheshimiwa majaji namfahamu Mwenyekiti kwa miaka 13 kama kiongozi anayepigania demokrasia, anayepigania haki haki, kama mgombea wa Urasi 2020, Mwenyekiti wa chama na kama mpiganaji aliyeumizwa na serikali ya Tanzania kwa kutokupewa mafao yake ya kibunge kwa kuwa harassed na kukamatwa mara kadhaa na kuwekwa mahabusu na kutolewa kwasababu ya misimamo yake ya kupigania haki na pia namfahamu kama Mwenyekiti wa Chama Kikuu Tanzania CHADEMA.

Sehemu ya 369

Lissu anaendelea kumuongoza shahidi wake ambae ni Mkurungenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA Hq, Brenda Rupia.

Mhe. Lissu: Waambie majaji mtu akikuambia kwamba huyo mtu uliyemuelezea hivyo ni mhaini wewe utasemaje?

Brenda: Kwa maneno yangu inaonyesha ni mzalendo, very patriotic mwenye mapenzi makubwa na nchi yake na mtu ambaye anapenda haki ni ngumu kuwa mhaini

Mhe. Lissu: nimemaliza waheshimiwa majaji.

Sasa ni zamu ya mawakili wa Serikali kuuliza maswali ya Dodoso.

Baada ya Mheshimiwa Tundu Lissu kumaliza Examination in Chief sasa yanaanza maswali ya Dodoso na anasimama Ajuaye anasema ataanza Wakili Winniwa Kuuliza maswali.

Anasimama Winniwa.

Winniwa: Habari ya asubuhi na pole kwa ushahidi mrefu

Brenda: Ahsante.

Winniwa: Ni sahihi nikisema kwamba hujaelezea kuhusu elimu ya uandishi wa habari?

Brenda: Sijaeleza.

Winniwa: Ni sahihi nikisema katika utendaji wako kama Mkurugenzi wa Habari unafanya kazi kimazoea?

Brenda: Hapana.

Winniwa: Ni sahihi hujasema una uzoefu wa muda gani?

Brenda: Nina uzoefu wa mwaka mmoja na miezi mitano. Nilisema kuwa nilichaguliwa Mwezi March 2025.

Winniwa: Ni sahihi hujasema kuwa majukumu yako ni yapi kama Mkurugenzi?

Brenda: Ni sahihi

Winniwa: Ni sahihi ulisema uliandaa matangazo kwa ajili ya kualika watia nia?

Brenda: Sahihi

Winniwa: Hujataja hizo pages ni sahihi ulikopost?

Brenda: Ni sahihi.

Winniwa: Unaelewa maana ya live streaming?

Brenda: Is to show something by live broadcast.

Winniwa: Ni sahihi Chama chenu kinafanya kazi bega kwa bega na Jambo TV.

Brenda: Sijui kuhusu kufanya kazi nao Bega kwa Bega. Sisi tunafanya kazi na vyombo vya habari vyote.

Winniwa: Siku ya Mkutano wa Tar. 03/04 Msemaji Mkuu alikuwa ni Mwenyekiti Tundu Lissu?

Brenda: Ni sahihi

Winniwa: Siku ya Mkutano huo kuna muda mlikuwa hamna control yoyote ya waandishi ni sahihi?

Brenda: Sio sahihi. Tulisema tumewaalika waje kufanya coverage ya tukio la Chama.

Winniwa: Kuna muda mliwaondoa watu watoke nje ya ukumbi wa mkutano?

Brenda: Kuna muda tuliwaondoa ndio.

Winniwa: Kuna maneno umetajiwa sana kuwa yalikuwa quoted. Sasa ni kweli ulikuwepo na ulisikia maneno kama kukinukisha na kuvuruga uchaguzi.

Brenda: Yapo kwenye hati ya mashitaka na yapo kwenye maneno aliyoyazungumza Mwenyekiti.

Winniwa: Nina uhakika nikisema Chama kilisusia uchaguzi?

Brenda: Hatukususia uchaguzi. Ingawa fomu hatukuchukua.

Winniwa: Unaelewa nini ukisema No Reforms: No Election

Brenda: HAKUNA MABADILIKO HAKUNA UCHAGUZI.

Winniwa: Mabadiliko gani mlikuwa mnataka?

Brenda: Electoral Reforms yaani Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asiwe mtu wa kuchagua mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi.

The President should not be able appoint delegate of the commission of the electoral committee, wasimamizi wa Uchaguzi wa Kata wasiwe watendaji wa Kata.

Winniwa: Kwa hayo uliyosema ndio uliona ndio njia ya kuwafanya msusie uchaguzi?

Brenda: Sisi tulikuwa huru Serikali ya wakati huo iendelee hata miaka 3 ili tuwe na mabadiliko ya sheria ndio tufanye a democratic election.

Winniwa: Nchi yoyote chaguzi zipo kisheria?

Brenda: Ndio ziko kisheria lakini chaguzi huru na haki lazima ziwe hivyo.

Winniwa: Kwahiyo mtu akitaka kuvuruga uchaguzi atakuwa anatenda kosa?

Brenda: Sio kweli.

Winniwa: Umesema scenario ndefu kuhusu kukamatwa kwako na ulikuwa unaenda safari ya German. Umeleta uthibitisho wowote kuhusu mwaliko wako wa kwenda German?

Brenda: Sijaleta uthibitisho.

Winniwa: Umesema kama umewahi kupeleka malalamiko yako yoyote kuhusu wewe kukamatwa na kuzuiwa kufanya safari?

Brenda: Sijawahi kufanya hivyo.

Sehemu ya 371

Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Shahidi no. 4 wa Mhe. Lissu, Brenda Rupia ambae ni Mkurungenzi wa Mawasaliano wa CHADEMA HQ.

Thawabu: Huyo mwamba hapo Ameshitakiwa kwa kukiuka kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu. Hiyo ni sheria na Mahakama imepewa mamlaka ya kutafsiri sheria na ibara ya 107 ya Katiba ndio inasema hivyo isome.

Anaisoma Brenda. Sasa Swali langu ulipokuwa unasema hayo kwamba hajafanya kosa una hayo mamlaka?

Brenda: Ibara ya 107 inasema mwenye mamlaka ya mwisho. Mimi nina mamlaka ya kusema ila mahakama wanayo mamlaka ya mwisho.

Thawabu: Uhaini ni nini?

Brenda: ku betray your country kutaka kupindua Serikali huo ndio uhaini.

Thawabu: Kuhusu kuhamasisha uasi kamusi ya kiswahili inasemaje kuhusu neno uasi?

Brenda: Ni kitendo cha uvunjaji wa sheria lakini B inasema kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka

Thawabu: Kwahiyo tafsiri mojawapo ni kuvunja sheria?

Brenda: Tafsiri mojawapo ni hiyo pia.

Thawabu: Nchi yetu ni nchi ya utawala wa ki imla?

Brenda: Kwa sasa ni nchi ya ki imla inavyoendeshwa.

Thawabu: Yanayofanyika hapa Mahakamani ni mambo ya kiimla?

Brenda: Hapa ni mambo ya kisheria.

Thawabu: Ulisema unaweza kufanya miujiza?

Brenda: Hapana.

Thawabu: Uliwezaje kupanda kwenye gari ambalo halina milango

Brenda: Magari ya polisi yanaeleweka yalivyo.

Thawabu: Walikutesa sana kwenye ile Probox?

Brenda: Hawakunitesa.

Thawabu: Ulikuwa upande wa kulia au kushoto nyuma ya Probox?

Brenda: Upande wa kushoto.

Thawabu: Watu wangapi walikuwepo kwenye gari?

Brenda: Ni watu wawili na mimi watatu.

Thawabu: Nitakuwa sawasawa nikasema ushahidi ulioutoa hauhusiani kabisa na hii kesi?

Brenda: Sijui.

Thawabu: Ile hati yako ya kusafiria ilikuwa inahusiana nini na yeye kukamatwa?

Brenda: Ulikuwa ni mwendelezo wa ukandamizaji wa viongozi wa Chadema. Vyombo vya dola kuendelea kukandamiza watanzania.

Thawabu: Hicho kifungu cha 39 cha Penal Code kinahusiana nini?

Brenda: Huo ni mwendelezo wa kukandamiza viongozi wa upinzani na shitaka hilo ni la uongo. Mwenyekiti sio muhaini. Anamsomea Kamusi hapa Brenda.

Thawabu: Unaweza kusoma kingereza au kiswahili?

Brenda: Anasoma hapa kifungu cha 39. A person who being allegiance to the united republic

Thawabu: Maana yake nini hiyo

Brenda: Mtu mwenye utii kwa Jamhuri ya Muungano

Thawabu: endelea

Brenda: In the united or elsewhere murders or attempt to murder na haya yote Mwenyekiti hajafanya hata moja.

Watu wanacheka😂😂😂

Thawabu: Sijakuuliza useme amefanya au hajafanya.

Brenda: Umesema nisome na kutafsiri. Tulia nifanye hivyo Mwenyekiti hajaua Rais.

Anasimama Mheshimiwa Lissu muda umeisha tayari.

Kesi imehairishwa kwa muda wa saa moja na nusu, Tunaenda break.

Sehemu ya 372

Mahakama imerejea muda huu. Saa tisa kasoro 5 alasiri.


Mhe. Lissu yupo,

Upande wa Jamhuri wanasema wapo kama walivokuwa asubuhi.

Shahidi anaelekea kwenye kizimba.

Jaji Ndunguru anamkumbusha Shahidi kwamba yupo chini ya kiapo.

Wakili wa Jamhuri Thawabu ameanza kumfanyia Cross examination Shahidi no. 4 wa Mhe. Lissu

Thawabu: Mshitakiwa anasema anashitakiwa kwa kurusha matangazo Jambo TV. Amekupitisha kuhusu mashitaka anayokabiliwa nayo?

Brenda: Amenipitisha nikiwa hapa kizimbani.

Thawabu: alichapisha kupitia jambo TV hapa ipo au haipo?

Brenda: Jambo TV haijatajwa hapa na mimi nilikuwa natetea hiyo hiyo hati ya mashitaka.

Thawabu: Umemtaja John Heche kwenye sekretarieti?

Brenda: Huyo sio sekretarieti.

Thawabu: John Pambalu, John Kitoka, John Mnyika ili uwe sekretarieti ni lazima uitwe John?

Brenda: Mimi naitwa Brenda.

Thawabu: Jibu swali sasa

Brenda: Nimeshajibu. Obvious kwa vile naitwa Brenda mimi sio John. Unasemaje wajumbe wa sekretarieti.

Thawabu: Unamjua Diamond, Mboso, Harmonize?

Brenda: Nawasikia.

Thawabu: Wanachoimba kikichezwa kwenye chombo kinakuwa sio chakwao?

Brenda: Kawaulize wao sasa.

Thawabu: Anachosema Lissu kikirushwa na Jambo kinakuwa cha nani?

Brenda: Kinakuwa cha kwao. Ndio wamiliki wa hiyo content waliyoipandisha.

Thawabu: Kipimo cha kuyasema maneno hayo sio kosa ni kipi? Angeyasema kwa muda mrefu ingeathiri nini?

Brenda: Sio kosa hata angesema muda mrefu.

Thawabu: Kuna maneno Rais wa Jamhuri ya Muu gan, Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Mashitaka. Ukasema hakuwataja. Wewe ni nani kati ya hao?

Brenda: Mimi sio Rais, sio Mkurugenzi wa Mashitaka. Sio Mwanasheria Mkuu wa serikali.

Thawabu: Unajuaje kutishika kwa Serikali ya Jamhuri

Brenda: Mimi sijasema hayo mambo. Nashangaa ukisema mambo ya serikali kutishika.

Thawabu: Tusomee tena kuhusu maana ya neno uasi?

Brenda: Kitendo cha kupinga au kuwa kinyume na mambo yanayofanywa na serikali

Thawabu: Soma maana ya kwanza

Brenda: Ni kitendo cha kutaka kuiondoa serikali iliyoko madarakani......

Thawabu: Kufanya kitu kitoe halafu mbaya ni kosa au sio kosa?

Brenda: Sio kosa

Thawabu: Kufuga kuku halafu zikatoa harufu ni kosa au sio kosa?

Brenda: Inategemea utakuwa unafugia wapi?

Jaji Hebu tuendelee mambo ya kufuga Kuku hayo.

Thawabu: Unajua kuhusu Baraza la Kutunza mazingira?

Brenda: Najua NEMC sasa inahusiana nini na kesi hii.

Thawabu: Wewe ni mtaalamu wa hesabu?

Brenda: Mimi nimesoma Accounting.

Thawabu: Tar. 10/06 Tar. 17/06 ulikuwa unatumia calendar gani?

Brenda: Nilikuwa nasema tarehe hadi mwaka na aina za Calendar sijui kabisa.

Thawabu: Hapa Tanzania kuna vyama vingine?

Brenda: Najua Chadema, ACT Wazalendo, Chaumma.

Thawabu: Uliposema Mwenyekiti wa Chama ulisema ulikuwa unasema Mwenyekiti wa Chama ulikuwa unamaanisha Chaumma?

Brenda: Nilipokuwa nasema nilisema mimi ni mkurugenzi wa Chadema. Niliposema hivyo ni Chadema.

Thawabu: Unapokuwa Mkurugenzi unaweza kujua Mwenyekiti analipwa na nani?

Brenda: Sijui

Thawabu: Kwahiyo huwezi kujua analipwa na jambo ndio asiwe mfanyakazi wa jambo tv?

Brenda: Hilo siwezi kujua na nyie mmeleta ushahidi wowote kuwa Mwenyekiti ni mfanyakazi wa Jambo Tv.

Thawabu: Kwenye mkutano wenu G55 waliongea saa ngapi?

Brenda: Hawakuongea na tusingewalazimisha kuongea pia.

Thawabu: Hii sio mahakama ya hisia?

Brenda: Ndio.

Thawabu: Ukimaliza kesi hii wakiona wanataka kukupeleka Mahakamani kwenye ile kesi yako uko tayari?

Brenda: Niko tayari.

Thawabu: Nimemaliza naomba aendelee mwenzangu.

Anasimama Job Mrema nae kuuliza maswali.

Sehemu ya 373

Upande wa Jamhuri wanaendeleaje kumfanyia Cross examination Brenda Rupia

Job: Ni sahihi ulishiriki kwenye mkutano wa Tarehe 03/04?

Brenda: Nilishiriki

Job: Mwenyekiti wa CHADEMA wakati anaongea na wajumbe alipotamka haya maneno aliungwa mkono au hakuungwa mkono?

Brenda: Hakukuwa na hilo swali kwenye mkutano.

Jaji jibu tu swali sasa.

Brenda: sasa sijui.

Job: Majukumu yako ni yapi?

Brenda: Kusimamia itifaki asipokuwepo Naibu Katibu Mkuu

Job: Sehemu ya mawasiliano unafanya nini?

Brenda: Mimi nakuwa incharge wa kuwaalika waandishi wa habari kuja kufanya coverage kwenye matukio ya Chama. Na kupitia hao waandishi wa habari Chama kinawasiliana na Umma. Mimi pia nina oversee utendaji wa kazi ambazo zinafanywa na watu waliopo chini yangu.

Job: kwahiyo wewe ni afisa mualikaji na sio afisa mawasiliano?

Brenda: Hauko sahihi, I have people work under me, on behalf.

Job: Hao watu walioko chini yake wanatekeleza majukumu yangu?

Brenda: Wanawasiliana na watu kupitia mitandao, wanaalika waandishi wa Habari pia. Wanawasiliana na umma kupitia vyombo vya habari, wanatoa pia taarifa.

Job: Wewe kama Mkurugenzi wa habari unaitumia?

Brenda: Naitumia.

Job: Wewe una elimu gani?

Brenda: Accounting

Job: Wewe una taaluma ya habari?

Brenda: Sina.

Job: Umewahi kusikia neno Kishoka?

Brenda: Hiyo Kishoka kingereza maana yake ni nini?

Job: Hatuongei Kingereza hapa.

Job: Mtu yeyote ambae anatoa huduma ya habari na sio mwanahabari kwa sheria za Tanzania

Mhe. Lissu: Mheshimiwa Wakili anapiga sana kelele hapa Mahakamani, nuisance. Hayo sio maswali kabisa.

Job Mrema: Wewe unayefanya kazi katika idara unafanya kimakosa na uko pale kimakosa?

Brenda: Idara sio mtu mmoja.

Job Mrema: Kumbe hukupaswa kwahiyo kuwa kwenye hiyo kurugenzi hebu fafanua?

Brenda: Kwani Katibu wa Itikadi wa CCM nae amesomea habari wapi?

Jaji: Hayo sasa yaache kwanza.

Brenda: Sasa asiniambie nifafanue.

Job: kwahiyo mtu anayefanya hizo kazi za habari bila sheria ni Kanjanja?

Brenda: Kwa kingereza hiyo maana yake nini?

Job: Huko usiende

Lissu: Anasimama anasema Mh. Jaji hilo neno Kanjanja amelitoa kwao huko anakuja kuuliza. Maana kwenye Kamusi halipo. Asilete maneno ya kikabila chao ayalete hapa.

Job: Sasa shahidi umeelewa

Brenda: Sijaelewa.

Job: Mtu yeyote anayetoa habari kinyume na sheria ambae hana sifa hapaswi kutoa hiyo huduma.

Brenda: Sijui.

Job Mrema: Umekuwa mwanachama wa Chadema toka lini?

Brenda: 2013

Job: Miaka mingapi uko nayo Chadema.

Brenda: Ndio uhesabu.

Job: Falsafa ya Chama ni nini?

Brenda: Ni nguvu ya umma

Job: maana yake nini hiyo falsafa ya umma

Brenda: Kushirikisha umma katika maamuzi ya vikao vya Chama, Kushirikisha umma kuhusiana na Uchaguzi kuchagua viongozi ambao umma unataka, kushirkisha umma katika matumizi ya rasilimali za nchi na kushirikisha umma kwenye jambo linalohusu nchi yao na Chama chao.

Job: Kwahiyo hiyo ndio tafsiri ya Katiba?

Brenda: Hiyo ndio tafsiri yangu.

Job: Soma hiyo ibara ya 3.3

Brenda: anasoma kuhusu Nguvu ya Umma na wananchi kuwa ndio msingi huo wa nguvu ya umma katika kila kitu.

Job: Wakati mshitakiwa anatamka maneno yale Tar. 03/04 ulimuunga mkono?

Brenda: Nilimuunga mkono na Mpaka leo nakubaliana nae kwa hayo maneno.

Job: Tunakubaliana kuwa nchi hii ina Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Brenda: Sahihi

Job: Ibara ya 3.1 ya Katiba ua Chadema inakielekeza Chama kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sehemu ya 374 ya Kesi itaendelea.....
Hizi sub za Barcelona ni hatari.
Kama hawataweka mpira kwapani basi tutarudi kulekule kwenye kiwanja cha dikiteta uchwara.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 17.

Job Mrema: Shahidi, ni sahihi sasa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo inaweka msingi wa utungwaji wa sheria zote nchini?

Brenda: Ni sahihi.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba sheria ya uchaguzi ipo hapa nchini Tanzania na ni moja ya sheria ambayo imetungwa kwa msingi wa Katiba?

Brenda: Nakubaliana na wewe.

Job Mrema: Katika msingi huo, waambie Majaji pale kwamba suala la kuvuruga uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba 2025 ni ukiukwaji wa Katiba.

Brenda: Siyo sahihi.

Job Mrema: Katiba inaruhusu kuvuruga uchaguzi?

Brenda: Sijui.

Job Mrema: Ukiwa kama Mwenezi, nchi hii Katiba yake hairuhusu kuvuruga uchaguzi?

Brenda: Sijui.

Job Mrema: Waambie Waheshimiwa Majaji, kabla ya uchaguzi Mkuu kufanyika, nikimaanisha Rais, Wabunge na Madiwani, Tume ya Uchaguzi imekuwa na utaratibu wa kutoa Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa kusaini kabla ya uchaguzi?

Brenda: Ni sahihi.

Job Mrema: Umewahi kusikia CHADEMA kusaini hizo Kanuni mwaka 2020?

Brenda: Sikumbuki.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi sasa kwamba mwaka 2020 CHADEMA ilisaini Kanuni?

Brenda: Sikumbuki.

Job Mrema: Hukumbuki nini?

Brenda: Ulichouliza ni kilekile. Relax.

Job Mrema: Nani a-relax?

Job Mrema: Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, kuna mahali pale sheria inaruhusu kuharibu uchaguzi Mkuu?

Brenda: Sifahamu.

Job Mrema: Kwa kuwa kwenye majibu yako umeieleza Mahakama hii kwamba wewe unaunga mkono maneno yote yaliyo katika mashtaka, nakwambia kuwa kuyaunga mkono ni ukiukwaji wa Katiba ya CHADEMA, Ibara ya 3.1.3.

Brenda: Siyo sahihi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Brenda: Ulichouliza ni kilekile. Relax.

Job Mrema: Nani a-relax?
😃😃😃
 
Achana na hilo jinga. Unapoteza muda tu kujibishana nalo. Liweke kwenye ignore list

Kwaiyo nyinyi kusikia kweli ndio hamtaki

Mnataka kudanganyana tu ❗️

Lissu kaonewaa ❗️

Lissu kasingiziwa ❗️

Basi wkt wenyewe mnaona upande wa Lissu unagomea maneno yake mwenyewe kwamaana ya wao wanataka iwe maana tofauti

mfano neno kukinukisha‼️

Chadema kupitia Mashahidi wake wanataka kuleta tafsiri yao ni kutoa harufu 🤔🤔
sio kukinukisha lengo kufanya fujo kama zile tumeziona

Kwaiyo yale meneno ya mh Lissu ni wazi nikosa kisheria kwa kuzingatia na yale ya Mo29

Chadema chini ya Viapo wanasema uwongo kwa kutoa Tafsiri tofauti ya kile kimo kwenye maneno ya Mh Lissu
Ambayo ndio mashtaka yake✍️
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 11.

Cuthbert: Na kuhusu ushahidi wa kutetea mwanachama au kiongozi yeyote ambaye ameshitakiwa hapa Mahakamani?

Brenda: Hii ni mara ya kwanza.

Cuthbert: Utakubaliana na mimi nikisema kwamba wewe ni shahidi ambaye una interest?

Brenda: Utakuwa hujakosea. Mimi ni shahidi mwenye interest ya haki kutendeka.

Cuthbert: Utakubaliana na mimi kwamba kwa kuwa wewe ni shahidi mwenye interest, basi ushahidi wako uchukuliwe kwa tahadhari?

Brenda: Mimi siyo mtaalamu wa sheria.

Cuthbert: Kama hujui sema sijui.

Brenda: Sijui.

Cuthbert: Kama nilikusikia ukisema mshtakiwa siyo mmiliki wa Jambo TV na hivyo hana hizo content?

Brenda: Ndiyo.

Cuthbert: Kuna ushahidi wowote ulioleta hapa Mahakamani unaoonyesha umiliki wa Jambo TV?

Brenda: Sijaleta, Waheshimiwa Majaji.

Cuthbert: Waheshimiwa Majaji, kwa upande wangu ni hayo. Naomba nikaribishe wenzangu.

Ajuaye Zegeli: Mheshimiwa Jaji, atafuata Tawabu Issa.

Tawabu: Rupia, nitaanzia alipoishia Cuthbert.

Kama shahidi anayependa haki, Waheshimiwa Majaji, namuonyesha kamusi ya Kiswahili atuonyeshe tafsiri ya neno haki.

Brenda:
(a) Stahili ya mtu, swala ambalo mtu anastahiki.
(b) Utendaji wa mambo kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni.

Tawabu: Kumbe haki ni kumpa mtu kitu anachostahili?

Brenda: Ndiyo.

Tawabu: Sasa Mwamba anashitakiwa kwa kukiuka kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu. Nikufafanulie, Kanuni ya Adhabu ni sheria, Sura ya 16.

Na ili nisikulishe maneno, nisomee Katiba hii, Ibara ya 107.

Brenda: (Anasoma Ibara ya 107)

"Mamlaka yenye kauli ya mwisho kwenye utoaji wa haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama."

Tawabu: Mamlaka hiyo sasa unayo?

Brenda: Mamlaka ya kauli ya mwisho sina, ni Mahakamani.

Tawabu: Katika kupita pita huko, umewahi kujua uhaini ni nini?

Brenda: Ni kusaliti nchi yako au kutaka kupindua Serikali.

Tawabu: Kwa hiyo kama ikitokea tafsiri nyingine ya uhaini na Mahakama ikaitumia kwa mujibu wa sheria, wewe upo tayari?

Brenda: Ndiyo.

Tawabu: Kuna kitu kimerudiwa sana na ukaulizwa sana kuhusu neno uasi. Kwa kamusi uliyo nayo hapo, uasi ni nini?

Brenda:
(a) Kitendo cha uvunjaji wa sheria kinachofanywa na kikundi cha watu chenye lengo la kubadili mfumo wa nchi yao.
(b) Kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka, kupinga kwa nguvu.

Tawabu: Nchi yetu ina utawala wa aina gani?

Brenda: Ina utawala wa kiimla.

Tawabu: Yanayofanyika hapa ni mambo ya aina gani?

Brenda: Kimahakama.

Tawabu: Yanafanyika katika nchi gani?

Brenda: Tanzania.

Tawabu: Wakati unatoa ushahidi wako ulisema hapa una uwezo wa kufanya miujiza?

Brenda: Hapana.

Tawabu: Nilisikia kwamba unasema ulipanda katika gari ambayo haina milango. Ulipandaje?

Brenda: Hiyo ni human error.

Tawabu: Ulipokuwa unatoka Namanga, kwa maelezo yako hawakuwa maafisa wa Polisi. Walikupakia katika eneo gani la Probox?

Brenda: Nyuma ya viti.

Tawabu: Walikutesa sana?

Brenda: Sijasema hivyo.

Tawabu: Ulipokuwa nyuma ulikuwa upande gani wa gari?

Brenda: Upande wa kushoto.

Tawabu: Kwenye lile gari palikuwa na watu wangapi?

Brenda: Watu watatu, mimi nikiwemo.

Jaji Ndunguru: Samahani, kwenye gari mlikuwa wangapi?

Brenda: Watatu.

Jaji Ndunguru: Kwa maana wasiojulikana wawili na wewe ndiyo watatu?

Brenda: Ndiyo.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nilimsikia akisema walikuwa wanne.

Brenda: Ni watatu, Mheshimiwa. Nimerekebisha.

Tawabu: Nitakuwa sahihi nikisema kwamba ushahidi ulioutoa hauhusiani na hii kesi?

Brenda: Sijui.

Tawabu: Kwenye hati yako ya kusafiria TAE 481364 inahusiana na nini na kesi ya uhaini ya Tundu Lissu?

Brenda: Nilisema kwamba kesi ya Tundu Lissu ni ya kubambikiwa na ni mwendelezo wa ukandamizaji wa viongozi wa CHADEMA kukamatwa na kunyanyaswa.

Tawabu: Ukimaliza kuongea, tuambie passport yako inahusiana nini na kesi ya uhaini ya Tundu Lissu?

Brenda: Nimesema viongozi wa chama wanakandamizwa na dola.

Tawabu: Unaposema shitaka la uongo, ni kwamba shitaka halipo au...?

Brenda: Shitaka lipo, ila ni la uongo.

Tawabu: Hebu soma kamusi utuambie maana ya uongo.

Brenda: (Anasoma kamusi)

"Uongo ni hali au tabia ya kuzungumza kinyume na ukweli."

Tawabu: Upo fluent kwa Kiingereza?

Brenda: Ndiyo.

Tawabu: Naomba nimuonyeshe atusomee Kanuni ya Adhabu.

Brenda: (Anasoma)

Kifungu cha 39(1):
"Mtu mwenye utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..."

"Mtu amuue au atake kumuua Rais..."

Hapo hakuna hata kimoja Mwenyekiti amefanya.

MAHAKAMA: (Kicheko)

Lissu: Waheshimiwa Majaji, naambiwa saa 7 imefika. Tunge-break. (Akiwa anacheka jibu la Brenda)

Jaji Ndunguru: Ngoja amalizie kusoma kwanza hapo.

Tawabu: Waheshimiwa Majaji, swali langu ni refu. Naomba tukirejea niendelee.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka.

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, tunakubali break tupate saa 1.

Lissu: Utaratibu wetu ni uleule, saa moja na nusu.

Jaji Ndunguru: Kwa nini saa moja na nusu?

Lissu: Ndiyo napata nusu saa ya kuzungumza na mashahidi wangu. Sina muda mwingine zaidi ya huu.

Jaji Ndunguru: Haya, tuonane saa 8 na nusu.

TUKUTANE SAA 8:30 MCHANA
Leo wanapokezana mpira harakaharaka,hakuna dribbling kwani wanajua aina ya mkabaji aliye ingia uwanjani,watu wanapiga pasi mbili na kurudisha kwa kipa.
 
Kwa wenye ulewa mdogo
Hii kesi ipo ivi

Chadema kupitia Mashahidi wake wote wanalengo moja tu kukataa maana ya aya meneno

Kisha wanakili kweli yametamkwa maneno ayo chini na Mwenyekiti wao❗️

lkn kwao wana Tafsiri yao tofauti na ile tunayoijua Watanzania
wote ❗️

Kiasi wengine wakafanya Fujo kumbe ndio kusema hawakumuelewa Mwenyekiti wa Chadema ❗️

yeye hakuwa na maana ile kukinukisha kwao nikutoa harufu kali sana 👈

Sijaongeza maoni yangu
nimeweka jinsi ilivyo pale Mahakamani
kinachobishaniwa👇
 

Attachments

  • 6381504-457b5131fdfe1ba30241f5952f4311e0.mp4
    1.5 MB
Kwa wenye ulewa mdogo
Hii kesi ipo ivyo

Chadema kupitia Mashahidi wake wote wanalengo moja tu kukataa maana ya aya meneno

Kisha wanakili kweli yametamkwa maneno ayo chini na Mwenyekiti wao❗️

lkn kwao wana Tafsiri yao tofauti na ile tunayoijua Watanzania
wote ❗️

Kiasi wengine wakafanya Fujo kumbe ndio kusema hawakumuelewa Mwenyekiti wa Chadema ❗️

yeye hakuwa na maana ile kukinukisha kwao nikutoa harufu kali sana 👈

Sijaongeza maoni yangu
nimewekwa jinsi ilivyo pale Mahakamani
kinachobishaniwa👇
 
Kwaiyo nyinyi kusikia kweli ndio hamtaki

Mnataka kudanganyana tu ❗️

Lissu kaonewaa ❗️

Lissu kasingiziwa ❗️

Basi wkt wenyewe mnaona upande wa Lissu unagomea maneno yake mwenyewe kwamaana ya wao wanataka iwe maana tofauti

mfano neno kukinukisha‼️

Chadema kupitia Mashahidi wake wanataka kuleta tafsiri yao ni kutoa harufu 🤔🤔
sio kukinukisha lengo kufanya fujo kama zile tumeziona

Kwaiyo yale meneno ya mh Lissu ni wazi nikosa kisheria kwa kuzingatia na yale ya Mo29

Chadema chini ya Viapo wanasema uwongo kwa kutoa Tafsiri tofauti ya kile kimo kwenye maneno ya Mh Lissu
Ambayo ndio mashtaka yake✍️
Nina wasiwasi na kiwango chako cha elimu na akili alafu nashangaa watu wanaojibizana na wewe ambae hata hueleweki unaandika nini humu upo kama zezete unadandia treni kwa mbele mwisho ubakwe.
 
Kwa wenye ulewa mdogo
Hii kesi ipo ivyo

Chadema kupitia Mashahidi wake wote wanalengo moja tu kukataa maana ya aya meneno

Kisha wanakili kweli yametamkwa maneno ayo chini na Mwenyekiti wao❗️

lkn kwao wana Tafsiri yao tofauti na ile tunayoijua Watanzania
wote ❗️

Kiasi wengine wakafanya Fujo kumbe ndio kusema hawakumuelewa Mwenyekiti wa Chadema ❗️

yeye hakuwa na maana ile kukinukisha kwao nikutoa harufu kali sana 👈

Sijaongeza maoni yangu
nimewekwa jinsi ilivyo pale Mahakamani
kinachobishaniwa👇

..Ndio maana Mama Abduli anatakiwa aende mahakamani akathibitishe jinsi maneno hayo yalitishia kumpindua, kumuondoa madarakani, kumuua, na kusimika utawala mwingine.

..lakini pia atarejeshwa ktk mazungumzo ya maridhiano na jinsi alivyoyakwamisha, na kusaliti falsafa yake ya 4R. Mojawapo ya R hizo ni REFORMS jambo ambalo Lissu na Chadema wamekuwa wakilipigania.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 18.

Job Mrema: Na tamko hilo umelitoa kupitia chombo gani cha habari?

Brenda: Nimefanya Live TikTok kupitia kamera ya simu yako, na mtu yeyote aliyepo TikTok anaweza kukusikiliza.

Job Mrema: Ni sahihi kwamba ulilenga umma?

Brenda: Ni sahihi.

Job Mrema: Ilikuwa tarehe ngapi?

Brenda: Sikumbuki, ila ilikuwa kati ya Aprili mwaka jana hadi sasa, baada ya Mwenyekiti kukamatwa.

Job Mrema: Ni sahihi kuwa kutojua sheria siyo kinga?

Brenda: Ni sahihi.

Job Mrema: Na ni kweli kwamba jinai haiozi?

Brenda: Sahihi.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba tamko ulilotoa ni kinyume na sheria?

Brenda: Sifahamu.

Job Mrema: Waheshimiwa Majaji, naomba kumalizia hapa ili niwaruhusu wenzangu waendelee na maswali.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, naomba kabla sijaendelea nimkabidhi kwanza Mshtakiwa nyaraka mbalimbali, ni cases mbalimbali.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, unazihitaji?

Lissu: Nashangaa zimefikaje huko.

Nassoro Katuga: Mawakili wake ndiyo wametupatia, wakijua hawana locus katika hii kesi.

Lissu: Mawakili wa Serikali hawana mamlaka yoyote ya kugusa nyaraka zangu na hawana mamlaka ya kufanya clearance ya nyaraka zangu. You should never touch my documents again.

Nassoro Katuga: Na sisi hatutogusa nyaraka zake.

Dr. Nshala: Niliwapa Magereza, wakaomba nipitishe kwa Mawakili wa Serikali.

Nassoro Katuga: Hii sasa ni fujo. Huyu anayeongea hana locus ya kuzungumza.

Jaji Ndunguru: Naomba tuendelee, lakini siku nyingine tumia muda wa break kama unahitaji nyaraka zako, au iombe Mahakama ndiyo itatoa amri nani apewe nini wakati mwingine. Isitupotezee muda.

Lissu: Sawa.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, naomba kupata mwongozo wa Mahakama hii. Nina maswali zaidi ya 50 na hayajirudii hata swali moja. Hata nikipewa saa moja sitamaliza.

Jaji Ndunguru: Malizia kwanza dakika 5 mlizopoteza wakati wa kujibizana kuhusu nyaraka, na nusu saa ya asubuhi tuliyopoteza.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba tuendelee. Asubuhi haiwezi kuwa kosa la Magereza kuanza saa 3:30, sababu Magereza walinifikisha saa 3 asubuhi.

Jaji Ndunguru: Tuendelee kidogo.

Nassoro: Nitakuwa sahihi kwamba wewe, ndugu yangu, kama kaka na dada, kwa maana Rupia ni Mnyamwezi?

Brenda: Huwezi kuwa kaka yangu wakati unataka Mwenyekiti wangu anyongwe.

Jaji Ndunguru: Tuendelee, mnapoteza muda.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, tarehe 29 Oktoba 2025 ulikuwa wapi?

Brenda: Nilikuwepo nyumbani.

Nassoro Katuga: Nyumbani wapi?

Brenda: Nyumbani Basihaya.

Nassoro Katuga: Tuambie cheo chako kingine kwa hapa Pwani.

Brenda: Katibu wa BAWACHA Mkoa wa Kinondoni.

Nassoro Katuga: Ulitaja hapo mwanzo?

Brenda: Nilitaja.

Nassoro Katuga: Ulisema kwamba uliangalia social media inayoitwa Jambo TV?

Brenda: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Kuna social media inaitwa Jambo TV?

Brenda: Ni YouTube channel.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo, mwanzo haikuwa sahihi kusema social media ya Jambo TV?

Brenda: Ndiyo, kwa sababu unani-confuse.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba unaniconfuse.

Brenda: Yeah, unani-confuse.

Nassoro Katuga: Si umesema mimi siyo kaka yako?

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, uliposema slang ni lugha ambayo siyo rasmi.

Brenda: Utakuwa sahihi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulisema maana ya slang na inatumika na group gani.

Brenda: Nilisema maana yake, ila sikusema inatumika na group gani.

Nassoro Katuga: Kama nilikusikia ukisema kwamba kukinikisha ni kukifanya kinukie, ni slang au Kiswahili rasmi?

Brenda: Kukinukisha siyo Kiswahili rasmi.

Nassoro Katuga: Nikifanya hiki kinuke, nitakuwa sahihi kusema nakinukisha?

Brenda: Both.

Nassoro Katuga: Kwa kuwa hujataja ni kundi gani, kwa sisi watoto wa mjini, kukinikisha ni slang inayotumika na vijana wengi.

Brenda: Utakuwa sahihi.

Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema kukinikisha ni kwenda kufanya jambo fulani?

Brenda: Kwenda ni sawa, ila kufanya jambo sina hakika.

Nassoro Katuga: Hebu waambie Waheshimiwa Majaji, kwa cheo chako...

Jaji Ndunguru: Hilo litakuwa swali la mwisho.

Nassoro Katuga: Hebu waambie Waheshimiwa Majaji, kwa cheo chako, kama nimekusikia umesema Rais wa Serikali ya Muungano hajatajwa.

Brenda: Nilisema katika paragraph aliyonisomea Mwenyekiti.

Nassoro Katuga: Sasa waambie Waheshimiwa Majaji, Serikali ya Muungano ni kitu gani?

Brenda: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nassoro Katuga: Serikali ya Muungano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni kitu sawa?

Nassoro Katuga: Naomba ni-pause hapo. Niliambiwa ni swali la mwisho.

MAHAKAMA: Shauri linaahirishwa mpaka kesho saa 3:00 asubuhi.

MAHAKAMA: Shahidi hujamaliza kutoa ushahidi wako. Utatakiwa kuwa hapa kesho saa 3:00 asubuhi.

MAJAJI WANATOKA.

TUKUTANE KESHO ASUBUHI.
 
Kwa wenye ulewa mdogo
Hii kesi ipo ivyo

Chadema kupitia Mashahidi wake wote wanalengo moja tu kukataa maana ya aya meneno

Kisha wanakili kweli yametamkwa maneno ayo chini na Mwenyekiti wao❗️

lkn kwao wana Tafsiri yao tofauti na ile tunayoijua Watanzania
wote ❗️

Kiasi wengine wakafanya Fujo kumbe ndio kusema hawakumuelewa Mwenyekiti wa Chadema ❗️

yeye hakuwa na maana ile kukinukisha kwao nikutoa harufu kali sana 👈

Sijaongeza maoni yangu
nimeweka jinsi ilivyo pale Mahakamani
kinachobishaniwa👇
Waliofanya fujo ni chadema au wananchi dogo hujielew
 
Nina wasiwasi na kiwango chako cha elimu na akili alafu nashangaa watu wanaojibizana na wewe ambae hata hueleweki unaandika nini humu upo kama zezete unadandia treni kwa mbele mwisho ubakwe.
Akichanganya ntamwekea dude langu akimbie nalo matkon
 
Kwa wenye ulewa mdogo
Hii kesi ipo ivyo

Chadema kupitia Mashahidi wake wote wanalengo moja tu kukataa maana ya aya meneno

Kisha wanakili kweli yametamkwa maneno ayo chini na Mwenyekiti wao❗️

lkn kwao wana Tafsiri yao tofauti na ile tunayoijua Watanzania
wote ❗️

Kiasi wengine wakafanya Fujo kumbe ndio kusema hawakumuelewa Mwenyekiti wa Chadema ❗️

yeye hakuwa na maana ile kukinukisha kwao nikutoa harufu kali sana 👈

Sijaongeza maoni yangu
nimeweka jinsi ilivyo pale Mahakamani
kinachobishaniwa👇
Swali ni kwamba,ni kosa kuzuia uchaguzi?
Kama ni kosa leta hicho kifungu cha sheria kinachotamka hivyo.
 
Kwa Msingi wa haki sisi Wananchi ndio tunapaswa tujue kile kimeongelewa Je kilikuwa na maana gani

Baada ya apo ndio tuseme mh Lissu
Anaonewa ❓️
au

Mh Lissu kwa maneno yale maana yake
yalikuwa kile na kile Jamhuri Inachosema ❓️

kimetokea au
Hakuwa na maana nyengine zaidi ya ile kakisema❓️

Mh Lissu anajaribu kukataa kupitia
Viapo yeye pamoja na Mashahidi wake
pale Mahakamani ✍️
 
Uzi umeanzishwa mapema sana kiasi cha kujikuta nimekosa kukaa siti ya mbele. Manyanza, imekaaje hii. Updates ni muhimu.
Inaonekana utaratibu haueleweki na wengi hapa.
'Role' za wakuu Manyanza na mwanzisha mada , mkuu 'Waufukweni' na wakati mwingine 'Mawele', ni ''complimentary'; ya hao wawli wa mwisho ni comprehensive; na kila kitu kiko mahala pamoja.
 
Back
Top Bottom