Ni mshangao mkubwa haya kutokea kwa upande wa serikali yenye kupaswa kuupata uhalali wake kutokea kwa wananchi wanaoilipa kodi.
Ni mshangao mkubwa zaidi kuwa walioko huko serikalini tunaowalipa mishahara na marupurupu wanaweza kufikia kucheza na haki za wananchi kwa kiwango hiki.
Kwamba tumefikia kupageuza mahakamani kuwa mahali pa kuchezea mchezo wa Paka na panya (hide and seek) kinara wa mchezo akiwa serikali zikihusianishwa haki za watu ambao labda hata hawana hatia?
"Ya namna hii si ndiyo yaliyo msukuma Hamza kujichukulia sheria mikononi?"
Kwamba serikali haitaki nyendo za askari D/C Msemwa kuhakikiwa kwa mustakabala wa haki?
Haya yakitokea nchi zingine zinawavesha askari wake ma camera mwilini kurekodi matukio yanayowahusisha?
Kwamba serikali haitaki nyendo za maaskari Kingai, Mahita, Goodluck, Jumanne, nk zihakikiwe kuthibitisha uhalali wa madai yao dhidi ya watuhumiwa?
"Tangu lini askari hawa wakawa malaika?"
Kwamba kwenye mchezo wa Paka na panya huu kuna watu huenda hata wameuwawa, wamepotezwa, wamefanywa vilema, wameumia, wanaumizwa, wanateswa, nk?
"Kwamba haya yakitokea waratibu wa kadhia hizi mko majumbani mwenu mkila raha na kugongeana bilauri na wake au waume zenu kwa gharama zetu?
Hivi ni ndoto, au ndiyo jinamizi lenyewe?
Kwamba tulidhani ninyi na sisi tulihitaji kuujua ukweli ili kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe, lakini kumbe ninyi mna nia ya kuuficha?
Kwa hakika hatuwaelewi ni nini hasa mnachokitaka.
Kwa hakika kwa hali kama hizi itakuwa ni sahihi kutakana radhi wazi wazi:
"Tusije kulaumiana."